Friday, January 31, 2014

WANAOTUHUMIWA KUMUUA DK SENGONDO MVUNGI WABANWA...

  
Washitakiwa wa kesi ya mauaji ya Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Edmund Mvungi wamesomewa mashitaka yao upya na baadhi yao kudai hawana imani na Mkuu wa Gereza la Segerea.

GAZETI LA SERIKALI YA RWANDA LAMKASHIFU RAIS KIKWETE...

Rais Kagame (kushoto) na Rais Kikwete wakifurahia jambo katika moja ya mikutano yao.
Rais Jakaya Kikwete, amesikitishwa na chokochoko zinazoendeshwa na gazeti la Serikali ya Rwanda, The News of Rwanda, lililomtuhumu kwa kusaidia vikundi vya waasi nchini humo.

TANZANIA YAULA UJENZI WA MIRADI MIKUBWA YA BARABARA, RELI NA BANDARI...

Matingatinga yakiwa eneo la ujenzi wa barabara.
Tanzania imeendelea kupata miradi mikubwa ya maendeleo ya kimataifa, ambapo sasa imeibuka mshindi kimataifa na kukubaliwa kuanzisha mradi mkubwa wa Kanda ya Kati wa uchukuzi.

BUNGE LATAKA UJENZI WA DARAJA LA KIGAMBONI UHARAKISHWE...

Daraja la muda Kigamboni.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imelitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuharakisha  kukamilisha ujenzi wa daraja la Kigamboni, ili kutoa nafasi kwa Rais Jakaya Kikwete kulifungua.

JICHO LA TATU...


Thursday, January 30, 2014

TICTS YAPIGWA MARUFUKU KULIPISHA WATEJA KWA DOLA...

Shehena ya makontena bandarini Dar es Salaam.
Wizara ya Fedha imeipiga marufuku Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini  (TICTS), kulazimisha wateja kulipia huduma kwa dola ya Marekani.

USHAHIDI DHAIFU WAWANUSURU ABSALOM KIBANDA NA WENZAKE...

Absalom Kibanda.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwachia huru aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima, Absalom Kibanda na wenzake baada ya kuwaona hawana hatia katika mashitaka ya uchochezi yaliyokuwa yanawakabili.

WABUNGE WAPINGA KIINGEREZA KUTUMIKA KUFUNDISHIA MASHULENI...

Wabunge ndani ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mjadala kuhusu lugha ya kutumia kufundishia shuleni umepamba moto, ambapo baadhi ya wabunge wamejitokeza kupinga Kiingereza kutumika kufundishia shule za msingi mpaka vyuo vikuu.

Wednesday, January 29, 2014

MDUNGUAJI AUA MWANAJESHI NA WATU WENGINE WANANE TARIME...

Mdunguaji akiwa mawindoni.
Jeshi la Polisi limeanzisha operesheni maalumu ya kumsaka mtu anayedaiwa kuwa jambazi, ambaye anaendelea kufanya mauaji wilayani Tarime.

HATIMA YA ZITTO KABWE CHADEMA KUJULIKANA HIVI KARIBUNI...

Zitto Kabwe (kushoto) na Dk Willibrod Slaa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, amesema hawaogopi kuita Baraza Kuu la Chama hicho,  kusikiliza rufaa ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

IKULU YAWAJIA JUU WANAOBEZA UTEUZI WA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI...

Salva Rweyemamu.
Mjadala kuhusu uteuzi wa Baraza la Mawaziri jipya lililotangazwa karibuni hauna maana na ni kupoteza muda, imeelezwa.

Tuesday, January 28, 2014

MWIGIZAJI MASHUHURI WA KUNDI LA FUTUHI AFARIKI DUNIA....

Marehemu Mzee Dude enzi za uhai wake.
Msanii maarufu wa kundi la Futuhi, Mzee Dude wa Bane amefariki dunia jana majira ya 11 jioni katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mjini Mwanza.

BEI YA KUUNGANISHIWA UMEME SASA NI SHILINGI 27,000 TU...

Moja ya miundombinu ya umeme.
Bei ya kuunganisha umeme katika vijiji ambavyo bomba la gesi linapita kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam, imeshushwa zaidi na kuwa Sh 27,000.

WAFANYABIASHARA WAPAMBANA KUZUIA UMEME USISHUKE BEI...

Moja ya vituo vya kuuzia umeme.
Wakati Watanzania wakilia ugumu wa maisha  pamoja na mambo mengine, kupanda kwa gharama za nishati ya umeme, imethibitishwa kuwa kuna wafanyabiashara wanapambana bei hiyo isishuke.

JWTZ KUJENGA KAMBI YA MUDA KILOSA...

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo (kushoto) na Mnadhimu wa Jeshi, Abdulrahman Shimbo wakikagua ukarabati wa reli baada ya kuharibiwa na mafuriko Kilosa.
Rais Jakaya Kikwete, ameagiza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kujenga kambi ya muda ya mahema na mabati katika kijiji cha Magole mkoani Morogoro, ili waathirika wote wa mafuriko wasio na nyumba, waishi kwenye kambi hiyo.

JICHO LA TATU...


Monday, January 27, 2014

MTUHUMIWA ATUNDIKWA MTINI NA KUBANIKWA KAMA NYAMACHOMA IRINGA...

Ezekiel Kaganga akiwa hospitalini.
Ezekiel akionesha majeraha sehemu ya mgongoni.
Vitendo vya uvunjaji wa sheria nchini, vinavyofanywa na baadhi ya wananchi kwa kujichukulia sheria mkononi kuwahukumu watuhumiwa, vimefikia hatua mbaya.

SHULE ZA MSINGI ZA SERIKALI SASA ZAGOMEA KISWAHILI...

Mwalimu akifundisha moja ya masomo kwa Kiswahili.
Wakati kukiwa na mjadala kuhusu lugha ipi itumike  kufundishia katika shule za msingi za Serikali, kati ya Kiingereza na Kiswahili, tayari baadhi ya shule hizo zimeshaanza kuacha kutumia Kiswahili kufundisha masomo yote na zingine zinajiandaa kufanya hivyo.

SASA MARUFUKU KUUZA KEMIKALI KWA WASIO NA LESENI...

Aina mbalimbali za kemikali.
Wakala wa maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imepiga marufuku uuzaji wa kemikali kwa mtu yeyote asiye na leseni kutoka kwake.

SERIKALI KUILIPA KNCU SHILINGI MILIONI 255 KUFIDIA HASARA...

Ofisi za KNCU.
Serikali imekubali kulipa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) 1984, Sh milioni 255. 1, kusaidia chama hicho kufidia hasara iliyotokana na mdororo wa uchumi duniani.

KIJEMBE CHA LEO...


JICHO LA TATU...


Sunday, January 26, 2014

MIMBA ZA WANAFUNZI ZAMTIA MATATANI OFISA MBEYA...

Serikali mkoani Mbeya imetoa muda wa siku saba kwa ofisa mtendaji wa kata ya Nanyala, Theofrida Hankungwe kuhakikisha amewasilisha taarifa zilizochukuliwa kwa wanafunzi watano waliopata mimba mwaka jana katika shule ya sekondari ya Shikula.

VIJIJI VYOTE LINAKOPITA BOMBA LA GESI KUPATIWA UMEME...

Moja ya vijiji lilikopita bomba la gesi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema njia pekee ya kuondokana na hujuma dhidi ya bomba la gesi linalosafirisha gesi Mtwara - Dar es Salaam ni kuviwekea umeme vijiji vyote bomba hilo linamopita.

JICHO LA TATU...


MLINZI WA KIONGOZI WA CHADEMA AMDHALILISHA MEYA KIGOMA...

Meya Bakari Beji.
Wakati mvua ikisambaratisha mikutano ya Chadema mkoani hapa, tafrani imezuka jukwaani kwa mmoja wa walinzi wa viongozi walio kwenye msafara wa chama hicho kumkunja shati na kumtoa kwenye kiti cha viongozi wakuu, Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Bakari Beji.

Saturday, January 25, 2014

BASI LA TAQWA LAGONGANA USO KWA USO NA LORI NZEGA...

Basi la Taqwa.
Dereva wa basi la kampuni ya Taqwa, Adam Ibrahim (50) amekufa papo hapo huku abiria kumi wakijeruhiwa baada ya basi alilokuwa anaendesha kutoka Dar es Salaam kwenda Bujumbura, Burundi kugongana na lori katika kitongoji cha Ngonho, Kata ya Miguwa wilayani Nzega.

BARABARA YA MOROGORO-DODOMA SAFI, MKULIMA AKWAMA JUU YA MTI KWA SAA SABA...

Magari ya mizigo kutoka pande zote barabara ya Morogoro- Dodoma, yakipita kwenye daraja la Mkundi - Magole, wilaya ya Kilosa Mkoa wa Morogoro, baada ya jana asubuhi kukamilishwa na kuruhusiwa kupita kwa zamu kila upande.
Magari yaliyokuwa yamekwama kwa siku tatu kuanzia Januari 22, kwenye barabara kuu ya Morogoro - Dodoma, baada ya daraja la Mkundi eneo la Magole, wilayani hapa kuharibiwa na mafuriko, yalianza kupita jana asubuhi baada ya matengenezo ya muda kukamilika.

KAGASHEKI AIPONDA RIPOTI YA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI...

Balozi Khamis Kagasheki akitangaza kujiuzulu wadhifa wake bungeni mjini Dodoma.
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amekosoa ripoti ya Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira akidai ilikuwa ya upande mmoja kwani haikuonesha mauaji ya  askari waliohusika katika Operesheni Tokomeza Ujangili.

PINDA ARIDHISHWA NA KAZI YA UTANDAZAJI WA BOMBA LA GESI...

Mafundi na wataalamu wa kigeni wakiendelea na kazi ya utandazaji bomba la gesi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema kazi ya kutandaza mabomba ya gesi itokayo Mtwara kwenda Dar es Salaam itakamilika mwishoni mwa mwaka huu.

MILIONI 10/- ZAKWAMISHA SHEKHE KWENDA INDIA KWA MATIBABU...

Shekhe wa Mkoa wa Mara, Athuman Magee, amelazwa katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam kwa takribani wiki moja sasa akisumbuliwa na matatizo ya pingili za uti wa mgongo huku shilingi takriban milioni 10 zikikosekana ili kumpeleka India kwa matibabu.

JICHO LA TATU...


WANAFUNZI WALIOFELI KIDATO CHA PILI KURUDIA DARASA...

Wanafunzi wa Kidato cha Pili wakiwa katika maandalizi ya mtihani wa Taifa.
Imeelezwa kuwa, licha ya matokeo ya kidato cha pili kutolewa 'kimyakimya'  kupitia ofisi za Elimu za Kanda na kubandikwa shuleni, hatua hiyo haimaanishi kuwa waliofeli wamenusurika kutorudia darasa.

Friday, January 24, 2014

KLABU YA YANGA YATOA TAMKO KUHUSU SUALA LA EMMANUEL OKWI...

Uongozi wa Yanga umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda, Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Yanga mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

MAHAKAMA YAAMURU BINTI WA MIAKA 20 ABAKWE NA KUNDI LA WANAUME...

KUSHOTO: Polisi wakiwa wamewakamata baadhi ya watuhumiwa. KULIA: Binti huyo akiwasili hospitalini.
Mwanamke mwenye miaka 20 ametelekezwa akiwa mahututi hospitalini jana baada ya mahakama moja ya kangaroo nchini India kumwamuru abakwe na kundi la wanaume kwa kuwa na mahusiano na kijana kutoka kijiji kingine.

TICTS YAKATAA MALIPO YA HUDUMA KWA SHILINGI KUANZIA JUMATATU IJAYO...

Huduma ya makontena bandarini Dar es Salaam inayofanywa na kampuni ya TICTS.
Kampuni ya Kuhudumia Kontena Bandarini (TICTS), imepiga marufuku wateja wake kulipa kwa Shilingi kuanzia Jumatatu na kutaka walipe kwa dola ya Marekani.

JICHO LA TATU...


Thursday, January 23, 2014

WAJUMBE 201 WATAKAOUNDA BUNGE LA KATIBA KUTANGAZWA WIKI IJAYO...

Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua marekebisho ya ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba.
Maandalizi ya Bunge Maalumu la Katiba, yamefikia hatua nzuri zaidi na wiki ijayo majina  201 ya wajumbe wa nyongeza wa Bunge hilo, yatatangazwa katika Gazeti la Serikali ili kukamilisha wajumbe 604.

MBUNGE WA CHALINZE KUZIKWA KESHO KIJIJINI KWAKE BAGAMOYO...

Said Bwanamdogo.
Mbunge wa Chalinze, Said Bwanamdogo (46),  aliyefariki dunia jana katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (Moi), Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kwa matibabu anatarajiwa kuzikwa kesho kijijini kwao Miono, wilayani Bagamoyo Pwani.

AJALI YA BARABARANI YAUA WANAFUNZI WATANO MTWARA...

Zelothe Steven.
Siku tatu baada ya kutokea ajali mkoani Lindi na Singida zilizogharimu maisha ya Watanzania 27, wakazi wa Mtwara nao wameingia katika majonzi baada ya gari dogo kupamia wanafunzi wa Sekondari ya Mustafa Sabodo, waliokuwa kwenye mchakamchaka na kuua watano.

JICHO LA TATU...


MAFURIKO YASOMBA BARABARA MOROGORO-DODOMA...

Daraja la Mkundi likiwa limebomolewa kabisa na mafuriko hayo.
Mafuriko yaliyotokana na mvua zilizonyesha katika milima ya Kiteto mkoani Manyara, yamesababisha maafa katika Wilaya ya Kilosa na kukata mawasiliano ya barabara kati ya Morogoro na Dodoma.

KITUO CHA DALADALA UBUNGO KUHAMISHWA WIKI IJAYO...

Kituo cha daladala kilichopo Ubungo.
Kituo cha  daladala Ubungo kinatarajiwa wiki ijayo, kuhamishiwa eneo jipya lililo jirani na Mawasiliano Tower.

Wednesday, January 22, 2014

MBUNGE WA CCM JIMBO LA CHALINZE AFARIKI DUNIA...

Said Ramadhani Bwanamdogo.
Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM), aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa (MOI), amefariki dunia.

IDADI YA WALIOPOTEZA MAISHA AJALI YA NOAH SINGIDA SASA YAFIKIA WATU 14...

Askari wakichukua moja ya miili ya waliofariki katika ajali hiyo eneo la tukio.
Mtoto wa miezi sita aliyejeruhiwa kwenye ajali ya gari dogo la abiria la Toyota Noah na lori la Scania mkoani hapa juzi, amefariki dunia na kufanya idadi ya waliokufa kufikia 14.

VIONGOZI WA DINI WAINGIA MAKUBALIANO NA SERIKALI KWENYE GESI...

Rais Jakaya Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa dini walioshiriki katika kongamano hilo.
Serikali imeanzisha utaratibu wa kusimamia rasilimali za nchi kwa kushirikiana na viongozi wa dini, ili kuondoa upotoshaji na kuimarisha umoja na amani ya nchi.

JICHO LA TATU...


MZAHA WA LEO...

Tarehe huwa zinavutia sana hasa kwa wale wanaokuwa ofisini. Utasikia: "Mi nina hamu kweli ya matembele."