MZAHA WA LEO...

Tarehe huwa zinavutia sana hasa kwa wale wanaokuwa ofisini. Utasikia: "Mi nina hamu kweli ya matembele."
Mwingine atadakia: "We acha tu, halafu upate na dagaa wako uchanganye na nyanya chungu, mbona unaweza kumaliza ugali kilo nzima!" Halafu mwingine naye utasikia: "Halafu ugali wenye uwe wa dona, utakoma!" Swali linakuja: Hivi ni kweli wafanyakazi hasa waajiriwa tarehe hizi za mwanzoni mwa mwaka huwa hawana hamu ya vyakula vizuri, mfano Chips, ndizi za kuchoma, soseji au nyama choma? Kazi kwako....

No comments: