Showing posts with label slide. Show all posts
Showing posts with label slide. Show all posts

Monday, August 18, 2014

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Exim Tanzania na baadhi ya wateja wakuonesha fataki kusherehekea maadhimisho ya miaka 17 ya benki hiyo ambayo husherehekewa kila Agosti 15. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Tawi la kwanza kufunguliwa na benki hiyo mwaka 1997 lililoko Samora, Dar es Salaam.

Afisa Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji (katikati) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bruce Macfarlane (kulia, mara baada ya kutiwa saini mkopo wa Shilingi bilioni 300.

Banda la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Vijana Duniani.

Baadhi ya wacheza ngoma wa kikundi cha Bujora wakishangilia baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa katika fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mabatini, jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kwa ushindi huo, Bujora walijinyakulia kikombe pamoja na pesa taslimu Shilingi 1,100,000.

Monday, August 4, 2014

Mratibu Maafa Ofisi ya waziri Mkuu, Edga Senga akipokea maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Florence Turuka kuhusu masuala ya maafa alipotembelea banda hilo katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea mkoani Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na michezo, Said Ali Mbarouk akizungumza na wamiliki wa mahoteli pamoja na wenye kusambaza bidhaa katika mahoteli ili kutatua matatizo yao huko kwenye Ukumbi wa Wizara ya Habari Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Samwel Sitta akiongoza kikao cha Kamati ya uongozi cha Bunge hilo kilichokaa leo kupanga ratiba ya bunge hilo linaloanza kesho Agosti 5, 2014 baada ya kuahirishwa Aprili 25, 2014 kupisha Bunge la Bajeti.

Washiriki wa Shindano la Redd's Miss Kinondoni 2014 wakiwa katika picha ya pamoja kwenye mazoezi yanayofanyika kwenye Hoteli ya Piccolo jijini Dar es Salaam. Jumla ya warembo 20 wapo kwenye mazoezi kujiwinda kwa shindano hilo litakalofanyika Ijumaa ya Agosti 15, 2014 kwenye fukwe za Escape One kwa kiingilio cha Shilingi 10,000 na 30,000 kwa VIP.

Wednesday, July 30, 2014

Miili ya abiria waliokufa kwenye ajali ya basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa ikiwa imelazwa kando ya basi hilo baada ya kugongana uso kwa uso na lori katika eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo asubuhi na kusababisha vifo vya watu 17 wakiwamo madereva wa magari yote mawili pamoja na kondakta na utingo wa lori hilo.

Wasamaria wakihangaika kunasua majeruhi na miili ya marehemu kutoka kwenye basi la Morobest lenye namba za usajili T 258 AHV lililogongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi. Watu 17 wamethibitishwa kufariki na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya.

Basi la Morobest lenye namba za usajili T 258 AHV likiwa eneo la tukio baada ya kugongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.

Majeruhi wa ajali ya basi la Morobest lililokuwa likitokea Mpwapwa kuelekea Dar es Salaam, wakiwa wamelazwa chini kusubiria huduma ya matibabu hospitalini. Watu 17 wamethibitishwa kufariki dunia mpaka sasa katika ajali hiyo ambayo basi hilo lenye namba za usajili T 258 AHV liligongana uso kwa uso na lori lenye namba T 820 CKU kwenye eneo la Pandambili, mkoani Dodoma mapema leo majira ya Saa 2 asubuhi.

Friday, July 25, 2014

Kiongozi wa Dini ya Kiislam Shehe Ali Mkoyogore (kulia) akisoma dua ya kuliombea Taifa mambo mema.  

Kiongozi wa Dini kutoka CCT,Steve Mang’ana (kulia) akisoma Sala ya kuliombea Taifa.

Kiongozi wa dini kutoka TEC, Liberatus Kadio (kulia) akisoma sala ya kuliombea Taifa wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa.

Wanajeshi wa JWTZ wakiwa katika gwaride la Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam mapema leo.

Monday, July 21, 2014

Gari lenye namba T166 CAF lililobeba mifuko hiyo ya plastiki inayoaminika kuwa na mabaki ya miili ya binadamu likiwa nje ya kituo cha polisi baada ya kukamatwa jana.

Mifuko ya plastiki inayoaminika kuwa na mabaki ya viungo na mabaki ya miili ya binadamu ikiwa imetelekezwa kwenye eneo la machimbo Mbweni Mpiji Magohe, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana.

Mifuko ambayo imesheheni mabaki ya kile kilichoelezwa kuwa ni mabaki ya miili ya binadamu ambayo ilitupwa na kugundulika mapema leo kwenye eneo la machimbo ya kokoto sehemu ya Mbweni Mpiji Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni limesema linaanza uchunguzi wa kina kuhusiana na suala hilo.

Friday, July 18, 2014

Crumpled: Wreckage of the Malaysia Airlines jet carrying 298 people from Amsterdam to Kuala Lumpur a day after it crashed, near the town of Shaktarsk, in east Ukraine