Showing posts with label LiveJukwaani. Show all posts
Showing posts with label LiveJukwaani. Show all posts

Sunday, May 4, 2014

TOTOO ZE BINGWA AAMUA KUJIWEKA KANDO KILI MUSIC AWARDS

Tuzo za muziki Tanzania 'Kili Music Awards' zimepata pigo jingine baada ya mwanamuziki mashuhuri wa dansi na rapa, Totoo Ze Bingwa kutangaza kujiondoa kwenye tuzo hizo.
Katika taarifa yake aliyoisambaza kwenye ukurasa wake wa Facebook, Totoo amesema haoni haja tena ya kushirikishwa kwenye tuzo hizo baada ya kutoambulia chochote kwa kipindi cha miaka mitano aliyoshirikishwa.
Totoo ambaye ni kiongozi wa bendi ya Malaika amewaomba radhi mashabiki wake kwa uamuzi wake huo na kuwataka wamuelewe kwanini kafikia uamuzi huo.
Ujumbe wake ulisomeka hivi: "Najaribu kujiuliza ni kwa nini nashirikishwa kili music awards cpati jibu haki ya mungu kwa heshima ya mashabiki wangu naomba kama kutakua na uwezekano nisishirikishwe tena mara 5 ni miaka mitano nimechoka kuzalilishwa."
Kwa kipindi kirefu sasa kumekuwa na mlolongo wa wasanii wa muziki wa aina mbalimbali ambao wamekuwa wakilalamikia Tuzo hizo na baadhi yao kutangaza kuomba wasishirikishwe katika kinyang'anyiro hicho kwa madai ya kutotendewa haki ama kuandaliwa washindi kabla ya onesho hilo.
Mbali na hilo, madai yao yameonekana kuwa na uzito hasa kwa kuzingatia jinsi shindano lenyewe linavyoendeshwa na hata wakati mwingine mshiriki mmoja kushinda tuzo zaidi ya tano.
Katika shindano la mwaka huu, msanii wa bongofleva, Naseeb Diamond alijizolea tuzo saba katika 'category' zote saba alizoshirikishwa.

Friday, April 11, 2014

Wanamuziki wa bendi ya Shengen Academy wakishambulia jukwaa kwenye Ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni. Hawavumi lakini wamo. Ni jina geni kidogo lakini limesheheni wanamuziki wenye majina makubwa katika medani ya muziki. Bendi hii iko chini ya uongozi wa Rais Liva Hassan Sultan. (Video ya ziro99blog).

Saturday, April 5, 2014

JICHO LA TATU...


SITTA AVUNJA KAMATI YA UONGOZI BUNGENI...

Samuel Sitta akiongoza Bunge la Katiba.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta ametengua uteuzi wake wa awali wa nafasi tano za Kamati ya Uongozi ili kuifanya kamati hiyo kuwa na uwakilishi mpana.

Friday, April 4, 2014

HAPANA KUKOSA ONESHO HILI...


MKUU WA MKOA AMTOLEA NJE MNYIKA KUHUSU BODABODA...

Said Meck Sadik.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amesema hawezi kusitisha agizo lake la pikipiki na bajaj kuingia  katikati ya jiji, kwani hana mamlaka hayo, kwani anasimamia sheria.

NYONGEZA YA MSHAHARA WA WABUNGE YAZUSHA BALAA...

Wabunge wa Bunge la Uganda juzi wamezua tafrani baada ya kuibua hoja ya kutaka waongezewe mishahara, ambapo tayari mshahara yao ni mara 60 ya mshahara wa mfanyakazi wa umma.

KURA THELUTHI MBILI ZAKWAMISHA UAMUZI KAMATI ZA BUNGE...

Wajumbe wa Bunge la Katiba ambao baadhi yao wanaunda kamati mbalimbali.
Hatua ya kufanya uamuzi wa kupitisha vifungu vya rasimu ya Katiba mpya katika ngazi ya kamati za Bunge, ilifikiwa jana huku changamoto ya kutopatikana kwa theluthi mbili ya kura kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ikijitokeza katika kamati nyingi.

JICHO LA TATU...


Thursday, April 3, 2014

IKULU YAANIKA POSHO ALIZOLIPWA JAJI WARIOBA NA WENZAKE...

Jaji Joseph Warioba (wa pili kutoka kulia).
Tume ya Mabadiliko ya Katiba haikufukuzwa kazi, isipokuwa siku ya ukomo iliwekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

BODABODA, BAJAJI MARUFUKU KUBEBA MTOTO WA MIAKA TISA...

Mtindo huu sasa ni marufuku kabisa.
Kanuni mpya za uendeshaji usafiri wa pikipiki na bajaj maarufu bodaboda, zimeainishwa zikisisitiza waendeshaji wa vyombo hivyo, kutekeleza masharti, ikiwemo linalokataza kupakia mtoto mwenye umri wa miaka tisa na  chini yake.

KESI DHIDI YA SHEKHE PONDA YAKWAMA...

Shekhe Ponda Issa Ponda akisindikizwa na askari mahakamani.
Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Mkoa wa Morogoro jana imeshindwa kuanza kusikiliza kesi  ya Katibu wa Jumuiya ya Waislamu  Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda.

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMUUA TRAFIKI...

Mkazi wa Kijitonyama, Cresence Nguzo (25) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kujaribu kumuua askari wa kikosi cha usalama barabarani.

Wednesday, April 2, 2014

NHC YAWEKA SOKONI NYUMBA ZAKE 118 ZA MAKAZI...

David Shambwe.
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa mara nyingine jana limezindua mradi mpya wa mauzo ya nyumba za makazi ya familia 118 katika Mtaa wa Wakulima, Hananasif, wilayani Kinondoni.

MKUU WA MKOA CHUPUCHUPU MTEGO WA SIKU YA WAJINGA...

Dk Rajab Rutengwe.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi , Dk Rajab Rutengwe  ametoa ushuhuda wake  jinsi  alivyoponea chupuchupu,  kuhadaiwa  na mkazi mmoja  mjini Mpanda jana asubuhi,  ambayo ilikuwa Siku ya Wajinga Duniani.

Sunday, March 30, 2014

BAKWATA YAUNGANA NA KIKWETE, NAO WAKATAA SERIKALI TATU...

Mufti Issa Shaaban Simba (kulia) akiteta jambo na Rais Jakaya Kikwete.
Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) limesema Waislamu wanataka Katiba itakayojali maslahi kwa wananchi wa pande zote mbili Bara na Visiwani na kuhakikisha Muungano unadumu.

YASEMAVYO MAGAZETI YA LEO....




Saturday, March 29, 2014

WAJUMBE WAKUBALIANA SUALA LA KURA KUPISHA MCHAKATO UENDELEE...

Wajumbe Bunge Maalum la Katiba wakipiga kura.
Hatimaye Bunge Maalumu la Katiba limemaliza mvutano wa Kanuni, hasa kuhusu kura ya wazi au ya siri katika kufanya uamuzi wa kupitisha ibara na sura za rasimu ya Katiba, kwa kuamua kura zote zitumike kwa kadri mjumbe mmoja mmoja atakavyoona inafaa.