Marehemu Mzee Dude enzi za uhai wake. |
Vyanzo vya habari vinasema kuwa Mzee Dude alikimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa juzi Jumapili. Haikuweza kufahamika mara moja maradhi aliyokuwa akisumbuliwa nayo marehemu.
Mzee Dude atakumbukwa sana na mashabiki wa vichekesho kwa jinsi alivyokuwa akiimudu fani hiyo licha ya umri wake mkubwa.
Pamoja na mpasuko uliotokea kwenye kundi la Futuhi miaka kadhaa iliyopita na baadhi ya wasanii kujiengua na kuunda kundi la Babatan, Dude aliendelea kuwa nguzo muhimu kwa Futuhi hadi mauti yalipomkuta.
Blogu ya ziro99 inaungana na familia ya marehemu pamoja na wasanii wenzake wa Futuhi katika maombolezo ya kifo cha msanii nguli, Mzee Dude.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi, Amina.
No comments:
Post a Comment