MAHAKAMA YAAMURU BINTI WA MIAKA 20 ABAKWE NA KUNDI LA WANAUME...

KUSHOTO: Polisi wakiwa wamewakamata baadhi ya watuhumiwa. KULIA: Binti huyo akiwasili hospitalini.
Mwanamke mwenye miaka 20 ametelekezwa akiwa mahututi hospitalini jana baada ya mahakama moja ya kangaroo nchini India kumwamuru abakwe na kundi la wanaume kwa kuwa na mahusiano na kijana kutoka kijiji kingine.

Adhabu hiyo ya kutisha ilidaiwa kutolewa na 'mahakama' inayofanana na hiyo ambayo ilimpata na hatia kwenye kijiji kimoja karibu na Suri katika jimbo la magharibi la Bengal, maili 150 kutoka Kolkata, polisi ilisema.
Polisi ilisema kwamba wanaume wote 13 wanaotuhumiwa - kumi kati yao wanaounda mahakama hiyo ya kangaroo - wameshakamatwa kwa ubakaji. Miongoni mwao ni kiongozi wa kijiji.
Polisi walikamata takribani watu 12 kwa kuhusiana na ubakaji huo wa kundi dhidi ya mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 kutoka Wilaya ya Birbhum huko West Bengal, nchini India.
Licha ya hali yake mbaya na kupigania maisha yake, mwathirika huyo wa kike alimudu kusimulia mkasa wake kwa gazeti la The Times of India.
"Nilikuwa na mahusiano na mwanaume mmoja," alilieleza gazeti hilo.
"Tulikokotwa hadi kwenye mkusanyiko wa watu ambako mkuu wetu alikuwapo. Walinitaka kulipa rupia 50,000 (Sawa na Pauniza Uingereza 490). Pale niliposema sina uwezo huo, waliniadhibu vikali."
Daktari mmoja alilieleza gazeti hilo kwamba mwanamke huyo mwenye umri mdogo alikuwa hai 'sababu tu ni msichana jasiri wa kabila hilo.'
Mama wa mwanamke huyo alisema kwamba "uhalifu huo ulifanywa na watu wetu wenyewe."
Aliongeza: "Walimtesa binti yangu na kumtupa nyumbani usiku wa manane. Tulitishwa tusiende polisi.
"Tulijaribu kwenda hospitali ya Bolpur, lakini walituzuia."
Gazeti hilo lilisema mwanamke huyo alibakwa katika kijiji kimoja huko kwenye eneo la kituo cha polisi cha Labhpur.
Ilikuwa Jumatatu mchana ndipo kundi la wanaume wa kabila letu walipomkuta mwanamke huyo akiwa ameketi na mpenzi wake, ambaye anatokea kijiji cha Chowhatta na wa dini tofauti.
Waliwakokota wote wawili hadi kwenye sehemu moja ya kidini inayofahamika kama 'kuliko' ambako mahakama ya kupokezana ilikuwa ikikutana pamoja kwa amri za machifu wa kabila hilo.
Polisi walisema kwamba kijana huyo alitakiwa kulipa faini ya Pauni za Uingereza 245 na kuonywa kwamba kama asingelipa, wanaume kutoka kijiji hicho 'wangemchezea msichana huyo watakavyo.'
Kufuatia kukosekana kwa pesa hizo, mwanamke huyo alidaiwa kufungwa kwenye mti kabla ya kulazimishwa kufunikwa macho na kubakwa mfululizo hadi Jumanne asubuhi.
Familia ya mwanamke huyo ililazimishwa kubaki imejifungia ndani siku yote ya Jumanne, wakifanya kila wawezalo kunusuru maisha ya binti yao ambaye alikuwa akitokwa na damu kwenye majeraha yake makubwa.
Kwa mujibu wa the Times of India, familia hiyo ilimudu kutoroka nje siku ya Jumatano mchana na kumpeleka mwanamke huyo kwenye kituo cha afya, ambako madaktari walisema alitakiwa kukimbizwa haraka kwenye hospitali ya karibu.
Lakini kutoka kwenye hospitali hiyo alihamishwa tena kwenda hospitali ya Suri akiwa katika hali mbaya wakati wa usiku.
"Hapa ndipo uhalifu huo ulipofahamika hadharani," alisema ofisa wa polisi Prashanta Chowdhury. "Alibakwa na kundi la wanaume na taarifa zaidi bado zinafanyiwa uchunguzi."
Tukio hilo la kushitusha si mara ya kwanza kwa mwanamke kuhukumiwa kwa kuwa na mahusiano katika eneo hilo.
Miaka minne iliyopita msichana mwenye umri chini ya miaka 20 alivuliwa nguo na kulazimishwa kutembea uchi kupita vijiji vinne, huku mamia ya watu wakimdhalilisha na kumtomasa.
Walifikia hata kumrekodi video kwa kutumia simu zao za mikononi, ambazo ziliwafanya polisi kwenda katika eneo hilo na kukamata watuhumiwa.
Msichana huyo alipokea tuzo ya ujasiri kutoka kwa Waziri Mkuu Manmohan Singh na jana alihamia kwenye makazi yanayoendeshwa na serikali.

No comments: