KLABU YA YANGA YATOA TAMKO KUHUSU SUALA LA EMMANUEL OKWI...

Uongozi wa Yanga umeamua kuweka hadharani ukweli kuhusiana na usajili wa mshambuliaji wake wa kimataifa kutoka nchini Uganda, Emmanuel Okwi ambaye kamati ya maadili na hadhi za wachezaji imemzuia kuichezea Yanga mpaka watakapopata uthibitisho kutoka FIFA.

Yanga ilikamlisha usajili wa Okwi tangu Desemba 15, 2013, na kupata Hati ya Uhamisho wake wa Kimataifa (ITC) ambayo iliwasilishwa TFF na fomu mama za usajili wa Ligi Kuu ya Vodacom....
Baada ya kukamilisha zoezi hilo TFF ilipitisha jina lake kwa kutupatia leseni no: 921225001 ambayo inamruhusu mchezaji kuichezea Yanga na kisha kulituma CAF, Desemba 31, 2013 kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo CAF nao walimuidhinisha kuwa mchezaji halali wa Yanga kwa mashindano hayo.
Cha kustaajabisha siku mbili kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom Kamati ya Maadili na hadhi za wachezaji wakamzuia mchezaji huyo kuichezea Young Africans ilihali akiwa ameshaidhinishwa na TFF na CAF kuwa mchezaji halali wa Young Africans.
Swali? Walikuwa wapi Kamati ya Maadili na Hadhi za Wachezaji kujiridhisha juu ya usajili ambao ulishakamilika tangu Disemba 15 2013? Wanakuja kutoa maamuzi hayo mwezi mmoja na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa, ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom?

No comments: