KITUO CHA DALADALA UBUNGO KUHAMISHWA WIKI IJAYO...

Kituo cha daladala kilichopo Ubungo.
Kituo cha  daladala Ubungo kinatarajiwa wiki ijayo, kuhamishiwa eneo jipya lililo jirani na Mawasiliano Tower.

Meya  wa Manispaa ya Kinondoni,  Yusuph Mwenda alimwambia mwandishi kwamba ujenzi wa kituo kipya, umekamilika kwa kiwango kikubwa.
"Kituo kiko kwenye hatua za mwisho na kitaanza kutumika mwisho wa mwezi huu na magari yote yatahamia huko," alisema Mwenda.
Akizungumza na mwandishi jana, alisema kituo hicho kilichopo Mawasiliano Tower, ujenzi wake ulianza mwaka jana.
Alisema wameamua kuhamisha kituo hicho, kutokana na ufinyu wa eneo Ubungo, uliochangiwa  na ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi.
Aidha, Mwenda alisema katika kituo  kipya,  wafanyabiashara ndogo hawataruhusiwa kuwepo kituoni, kama ilivyo sasa kwa Ubungo.
" Katika kituo hicho kipya hatutaruhusu wafanyabiashara wadogo na tutakuwa na ulinzi mkali," alisema.
Alisema, "hii ni kwa sababu maeneo hayo si salama kwao na sio sehemu husika kwa wafanyabiashara hao kwani kuna eneo maalumu lililotengwa na serikali kwa ajili yao. "

No comments: