MBUNGE WA CCM JIMBO LA CHALINZE AFARIKI DUNIA...

Said Ramadhani Bwanamdogo.
Mbunge wa Chalinze, Said Ramadhani Bwanamdogo (CCM), aliyekuwa amelazwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa (MOI), amefariki dunia.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ndugu wa karibu, Mheshimiwa Bwanamdogo alikuwa akisumbuliwa na maradhi kwa takribani miaka miwili na kwamba amefariki mapema leo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari, marehemu anatarajiwa kuzikwa kijijini kwake huko Chalinze kesho.

No comments: