Thursday, October 31, 2013

POLISI WAMPIGA RISASI MWANAMKE ALIYEKAIDI AMRI ARUSHA...

Kamanda Liberatus Sabas.
Mwanamke mkazi wa PPF jijini hapa, Vailet Mathias, amepigwa risasi na polisi na kujeruhiwa eneo la Benki ya CRDB Mapato baada ya kukaidi amri halali ya Polisi na kumtishia silaha.

WABUNGE SASA WASHINIKIZA TANZANIA IJITOE JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI...

Samuel Sitta.
Serikali iko katika mazungumzo na nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Burundi ili kushirikiana kwa baadhi ya maeneo, hasa kutokana na ukweli kuwa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Rwanda, Kenya na Uganda, zimeonesha mwelekeo wa kujitenga.

CHADEMA YASISITIZA KWAO HAKUNA UKOMO WA MADARAKA...

Wafuasi na wanachama wa Chadema wakiandamana wakati wa moja ya mikutano ya chama hicho.
Chadema cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimekiri kubadili kifungu cha ukomo wa uongozi kwa kutumia ilichoita utaratibu sahihi na haikuwa katika kutoa fursa kwa baadhi ya watu.

JICHO LA TATU...


UJENZI WA DARAJA KUBWA LA MALAGARASI WAKAMILIKA...

Lori likipita juu ya Daraja la Malagarasi.
Ujenzi wa Daraja la Malagarasi lililopo mkoani Kigoma, maarufu kama Daraja la Kikwete, umekamilika rasmi na tayari magari yameanza kulitumia.

Wednesday, October 30, 2013

UVCCM WAKATAA SHILINGI 1,000 YA KODI YA SIMU ZA MIKONONI...

Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) limeitaka Serikali kurejesha bungeni kwa hati ya dharura Muswada wa Marekebisho ya Tozo ya Sh 1,000  kwa laini za simu kwa mwezi.

KIPENGELE CHA UKOMO WA MADARAKA CHAITAFUNA CHADEMA...

Freeman Mbowe.
Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumsimamisha wadhifa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba naye kujitokeza kutoa tuhuma, chama hicho sasa kimeamua kumjibu  mfululizo.

JICHO LA TATU...


HUKUMU YA BABU SEYA, PAPII KOCHA YAPITIWA LEO...

Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe Johnson Nguza 'Papii Kocha'.
Hukumu ya mwanamuziki maarufu nchini mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Nguza Viking ‘Babu Seya’ na mwanawe Johnson Nguza 'Papii Kocha', inatarajiwa kufanyiwa mapitio leo na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa nchini.

Tuesday, October 29, 2013

HATIMAYE MTU MREFU ZAIDI DUNIANI AFUNGA NDOA...

Sultan Kosen akiwa na mkewe, Mervi Dibo.
Raia wa Uturuki Sultan Kosen, mwenye urefu wa mita 2.51 (sawa na futi 8.3) ambaye ni mtu mrefu zaidi duniani, amefunga ndoa na mwanamke wa Syria anayemwita 'mpenzi wa maisha yangu', licha ya kumzidi mkewe huyo mita 1.75.

MWIGAMBA ALIA NA UBAGUZI NDANI YA CHADEMA, ASHAURI MBOWE AJIUZULU...

Samson Mwigamba.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Arusha, Samson Mwigamba, ambaye amesimamishwa kwa muda usiojulikana, ameelezea namna uongozi wa juu wa chama hicho, unavyobagua watu wa kuwaadhibu wakati wa kutoa maoni kuhusu chama.

VICHWA 13, MABEHEWA 274 RELI YA KATI KUTUA NCHINI MWAKANI...

Kero kama hizi kwa wasafiri wa Treni ya Reli ya Kati zinatarajiwa kuisha mwakani.
Kero zilizopo katika usafiri wa Reli ya Kati, ikiwemo uchafu na kuzeeka kwa miundombinu, inatarajiwa kuisha mwakani, pale vichwa vya treni vipya 13 na mabehewa mapya 274 yatakapowasili.

JICHO LA TATU...


ASKOFU KANISA KATOLIKI ASIFU MCHAKATO WA KATIBA MPYA...

Askofu Telesphory Mkude.
Askofu wa Jimbo la Kanisa Katoliki la Morogoro, Telesphory Mkude, amemsifia na kumpongeza Rais  Jakaya Kikwete, kwa kuanzisha, kusimamia na kuongoza vizuri mchakato wa kutungwa kwa Katiba mpya nchini.

Monday, October 28, 2013

MWENYEKITI CHADEMA ASIMULIA ALIVYOPOKEA MKONG'OTO ARUSHA...

Samson Mwigamba akihutubia moja ya mikutano.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, amesimulia namna alivyovamiwa na kupigwa na wanachama wenzake mithili ya mwizi.

WANAFUNZI 1,107 WALIOKOSA MIKOPO VYUO VIKUU WAPEWA SIKU 14...

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Wanafunzi 1,107 wa masomo ya kipaumbele waliokosa mkopo kutokana na fomu zao za maombi kuwa na dosari, wamepewa muda hadi Novemba 6 mwaka huu, wawe wameshasahihisha fomu hizo.

JICHO LA TATU...


UPANGAJI WA UFAULU ELIMU YA SEKONDARI KUBADILISHWA...

Profesa Eustella Bhalalusesa.
Wakati wanafunzi wanaotarajiwa kuhitimu kidato cha nne nchini, wakitarajiwa kuanza Mtihani wa Taifa Jumatano ijayo, Serikali inajiandaa kubadili mfumo wa upangaji alama za ufaulu wa mitihani ya sekondari.

Thursday, October 24, 2013

WABUNGE WASTAAFU WAGEUKA OMBAOMBA, WAMLILIA NJAA SPIKA OFISINI KWAKE...

Spika Anne Makinda akisisitiza jambo bungeni, Dodoma.
Ofisi ya Bunge inaangalia utaratibu wa kufundisha wabunge ujasiriamali baada ya kubainika baadhi ya wanaokoma kushika wadhifa huo, kukabiliwa na hali mbaya ya ukwasi na kulazimika kuomba msaada.

MWILI WA KAMANDA JAMES KOMBE KUAGWA KESHO...

Marehemu Kamanda James Kombe.
Mwili wa aliyekuwa Kamanda mstaafu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) James Kombe, utaagwa kesho katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),  Usharika wa Msasani jijini Dar es Salaam.

JICHO LA TATU...


MGAWANYO WA HALMASHAURI WAIBUA MGOGORO RUKWA...

Moshi Chang'a.
Mgawanyo wa halmashauri ya Sumbawanga wenye lengo la kufikisha huduma za Serikali karibu na wananchi, umeibua mgogoro baada ya halmashauri mpya ya wilaya ya Kalambo, kudai kuhujumiwa na halmashauri mama.

Wednesday, October 23, 2013

KAMANDA JAMES KOMBE AFARIKI DUNIA, MWILI WA UNCLE J WAAGWA...

Kamanda James Kombe enzi za uhai wake.
Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP) mstaafu, James Kombe, amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

AJITUNDIKA MWENYEWE BAADA YA KUUA MKE WAKE...

Kamanda Evaresti Mangala.
Mkazi wa Kijiji cha Idukilo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhela Galawa (35),  anadaiwa kumuua mkewe kwa kumnyonga shingo kisha kujiua kwa kujitundika kwenye kitanzi  nyumbani kwake kile kilichodaiwa ni wivu wa mapenzi.

JICHO LA TATU...


BUNGE LAAGIZA SERIKALI KUIMILIKI TTCL ASILIMIA 100...

Bunge la Jamhuri ya Muungano.
Wakati Serikali ikidaiwa mabilioni na Kampuni ya Simu ya TTCL, Kamati ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kununua asilimia 35 ya hisa za kampuni hiyo, zinazomilikiwa na Kampuni ya simu ya Airtel, ili kuwa na umiliki kamili.

VYAMA VYA SIASA VYAANZA KUHOJIWA RIPOTI YA UKAGUZI WA MAHESABU...

Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani katika moja ya mikutano ya pamoja. Kutoka kulia ni James Mbatia (NCCR), Prof. Ibrahim Lipumba (CUF) na Freeman Mbowe (Chadema).
Vyama vya siasa nchini, vimeanza kupokea barua ya mwito kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, ya kuwataka kuhudhuria kikao kilichoandaliwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), keshokutwa.

Tuesday, October 22, 2013

SERIKALI, BODI WAOKOA WANAFUNZI 1,107 WALIOKOSA MIKOPO VYUONIB...

Baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu Dodoma walipokuwa wakifuatilia mikopo yao.
Wanafunzi 1,107 wa masomo ya kipaumbele waliokosa mkopo kutokana na fomu zao za maombi kuwa na dosari, wamehurumiwa na Serikali na sasa watapata mikopo waanze chuo.

BINTI MAHUTUTI BAADA YA KULAZIMISHWA NA MPENZI WAKE KUNYWA TINDIKALI...

Jitendra Sakhpal akisindikizwa na polisi kuingia mahakamani.
Msichana mdogo ameungua vibaya baada ya rafiki yake wa kiume aliyevunja naye uchumba kudaiwa kumtega walipokutana, kumlazimisha kunya tindikali na kumsukumia kwenye bahari.

JICHO LA TATU...


MAHAKAMA YAWAACHIA HURU WAFUASI 52 WA SHEKHE PONDA...

Wafuasi wa Shekhe Ponda wakiwa katika Mahakama ya Kisutu.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imewaachia huru wafuasi 52 wa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda, ambao walikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja jela iliyotolewa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

TANZANIA YAHOJI KUTENGWA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI...

Bendera za nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Tanzania imeuandikia rasmi uongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kuhoji kuibuka kwa utaratibu wa baadhi nchi wanachama, kujadili masuala ya utangamano bila kushirikishwa.

Monday, October 21, 2013

WAMCHONGEA ZITTO KABWE ACHUKULIWE HATUA KWA KUTAJA MSHAHARA WA RAIS...

Kabwe Zitto.
Hatua ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu, imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali  Kuu na Afya (TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa  vile ni ukiukaji wa sheria.

HIKI NDICHO KILICHOMUUA MTANGAZAJI MKONGWE JULIUS NYAISANGA...

Marehemu Julius Nyaisanga.
Mtangazaji mwandamizi na mwandishi wa habari mkongwe nchini, Julius Nyaisanga (53) maarufu kama Anko J,  amefariki dunia mkoani Morogoro, baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa kisukari na shinikizo la damu. 

TRENI YA MWAKYEMBE YASITISHA HUDUMA...

Moja ya vichwa vya treni vya TRL.
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji leo ili kutoa nafasi ya kukarabati vichwa cha treni.

JICHO LA TATU...


MENEJA WA SHIRIKA LA TAIFA LA USAGAJI AIBUKA NA KUDAI HAJAKABIDHI MALI...

Dk James Wanyancha.
Aliyekuwa Meneja wa Shirika la Taifa la Usagishaji (NMC) mkoani Arusha, ameibuka na kuomba asihusishwe na upungufu wowote utakaoibuka ndani ya shirika hilo kwa kuwa hajakabidhi rasmi mali.

FASTJET YAZINDUA SAFARI KWENDA AFRIKA KUSINI...

Moja ya ndege za FastJet.
Shirika la Ndege la FastJet limezindua safari ya kwanza ya Kimataifa kutoka Dar es Salaam kwenda Johannesburg, Afrika Kusini.

Sunday, October 20, 2013

WAKAMATWA NA KUKIRI KUMWAGIA WATU TINDIKALI...

Kamanda Suleiman Kova.
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya kumwagia watu kemikali aina ya tindikali.

WATAKA TRAFIKI WA KUVUSHA WALEVI BARABARANI DODOMA...

Moja ya mitaa ya Dodoma.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi amekataa ombi la wakazi wa eneo la Chaduru katika Manispaa ya Dodoma kutaka kuwepo kwa Askari wa Usalama Barabarani  kwa ajili ya kuvusha walevi ambao wamekuwa wakigongwa kwa wingi katika eneo hilo.

JICHO LA TATU...


DAWA ZA KULEVYA ZAMCHEFUA MIZENGO PINDA CHINA...

Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema katika kipindi alichokaa ofisini na kushughulikia suala la dawa za kulevya amebaini kuwa tatizo la matumizi ya dawa hizo linakuzwa kwa kiasi kikubwa na hulka ya watu kutaka kupata utajiri wa haraka.

Saturday, October 19, 2013

WACHINA WAOMBA KWA MIZENGO PINDA KUIFUMUA RELI YA KATI...

Sehemu ya njia ya Reli ya Kati.
Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) ya hapa, imesema iko tayari kuja nchini kuijenga upya Reli ya Kati ili iwe ya kisasa zaidi.

MTEJA WA M-PESA AMTWANGA KICHWA JAMBAZI ALIYEKUWA AKIJIANDAA KUIBA...

Kamanda Liberatus Sabas.
Kama si mmoja wa wateja katika duka la huduma ya M-Pesa kumpiga kichwa mmoja wa watuhumiwa wa ujambazi na kumfanya achanganyikiwe na kisha kukimbia, watu hao wakiwemo walinzi wawili wa Kampuni ya Ulinzi ya KK Security, wangeweza kufanikisha uporaji wa kiasi kikubwa cha fedha jijini Arusha.

JICHO LA TATU...


MUME AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KATIKATI YA SHEREHE YA HARUSI...

KUSHOTO: Jacqueline na Dameion wakikata keki. KULIA: Jacqueline akikumbatiana na Dameion mara baada ya kufunga ndoa.
Bi harusi mpya alilazimika kushuhudia mume wake mpya akipigwa risasi na kufa na wanaume wenye silaha walioficha sura zao kwenye sherehe ya harusi yao nchini Jamaica.

ZITTO AJIWEKA KANDO KUONGOZA KIKAO ILI KUPISHA HAKI ITENDEKE...

Kabwe Zitto.
Wakati Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ikipitia faili moja baada ya jingine la vyama tisa vya siasa vyenye stahili ya ruzuku ili kujiridhisha kuhusu ripoti za hesabu kabla ya kusema lolote, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto amesema si Msajili wa Vyama vya Siasa ama CAG, atakayekwepa lawama kuhusu suala hilo.

Friday, October 18, 2013

UTATA WATANDA KUJIUA KWA MZAZI MWENZAKE UFOO SARO...

Ufoo Saro akiwa wodini baada ya kufanyiwa upasuaji.
Familia ya marehemu Anthery Mushi, anayedaiwa kujiua kwa kujipiga risasi, imeomba Polisi kutumia busara wakati wa uchunguzi wa kifo hicho, kwa sababu ndugu yao amekutwa na matundu mawili ya risasi, baada ya mwili wake kufanyiwa uchunguzi.

KABWE ZITTO AVISHIKA PABAYA VYAMA VYA SIASA...

Kabwe Zitto.
Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), Kabwe Zitto, ameendelea kusisitiza kuwa hadi sasa hakuna chama chochote cha siasa kilichowasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu zake kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na kuvitaka vyama hivyo kuacha propaganda na kulichukulia suala hilo kisiasa.

JICHO LA TATU...