![]() |
| Marehemu Julius Nyaisanga. |
Mtangazaji mwandamizi na mwandishi wa habari mkongwe nchini, Julius Nyaisanga (53) maarufu kama Anko J, amefariki dunia mkoani Morogoro, baada ya kusumbuliwa kwa muda mrefu na ugonjwa kisukari na shinikizo la damu.
Meneja wa matangazo kituo cha Abood Media ambako Nyaisanga alikuwa Meneja wa kituo hicho, Abed Dogoli, alisema kuwa Nyaisanga alifariki dunia jana saa 1 asubuhi katika Hospitali ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro.
Dogoli alisema utaratibu za mazishi unafanyika nyumbani kwa marehemu Kihonda na wanatarajia kumsafirisha kwenda nyumbani kwao mkoani Mara, kwa maziko.
Nyaisanga aliwahi kufanya kazi katika kituo cha utangazaji cha Radio Tanzania (RTD), kabla ya Media ambako alikuwa Mkurugenzi wa Radio One. Pia aliwahi kufanya kazi katika kituo cha radio cha Deutsche Welle (DW) cha Ujerumani.
Akizungumza na mwandishi mke wa marehemu, Leah Nyaisanga, alisema kuwa mumewe juzi jioni hali yake ilibadilika ghafla na kuzidiwa ambapo alipelekwa hospitali ya Mazimbu kwa matibabu mpaka mauti yalipomfika jana asubuhi.
Mbunge wa Morogoro Mjini, Aziz Abood ambaye familia yake ndio wamiliki wa kituo cha Abood Media, alielezea kupokea msiba wa meneja huyo aliyekuwa mchapakazi kwa masikitiko.
Alisema alimfahamu Nyaisanga miaka mingi tangu akiwa katika vituo mbalimbali vya utangazaji na alikuwa mahiri na maarufu.

No comments:
Post a Comment