![]() |
| Moja ya vichwa vya treni vya TRL. |
Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa kwa huduma ya treni ya jiji leo ili kutoa nafasi ya kukarabati vichwa cha treni.
Kazi ya ukarabati wa vichwa hivyo kwa mujibu wa Msemaji wa TRL, Midladjy Maez ilikuwa imeshaanza Morogoro, lakini haikukamilika kwa wakati kama walivyotarajia.
“Taarifa za kiufundi zimebainisha kuwa ukarabati wa vichwa hivyo utakamilika mapema kesho (leo) asubuhi na hivyo kuwasili Dar es Salaam jioni tayari kuanza huduma kesho kutwa (kesho),” alisema.
Kuhusu kichwa cha treni kilichopata hitilafu ya kuungua moto juzi jioni kikiwa safarini kutoka stesheni ya Kamata kuja kituo kikuu cha Dar es Salaam, Maez alisema ni miongoni mwa vichwa vitatu vinavyofanyiwa ukarabati huko Morogoro.
Aliwaomba radhi wakazi wa jiji ambao ni watumiaji wakubwa wa huduma hiyo inayoanzia Stesheni ya Ubungo Maziwa hadi Stesheni ya Dar es Salaam.
“Uongozi umewahakikishia kuwa mafundi wa TRL katika karakana za Morogoro na Dar es Salaam wanafanya kila jitihada kurejesha huduma hiyo kwa wakati ili kupunguza usumbufu kwa wateja wake ambao wamezoea huduma na kunufaika nayo,” alisema.

No comments:
Post a Comment