![]() |
| Freeman Mbowe. |
Baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumsimamisha wadhifa aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba naye kujitokeza kutoa tuhuma, chama hicho sasa kimeamua kumjibu mfululizo.
Taarifa iliyotolewa jana na chama hicho kupitia Ofisa Habari wake, Tumaini Makene, ilisema kimeanza kutoa na kuandaa taarifa rasmi kujibu kinachoita uongo, upotoshaji, uchonganishi ulioandikwa na mwenyekiti huyo.
“Kutokana na hatua ya Mwigamba, aliyesimamishwa uenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, kukiri mbele ya waandishi wa habari kuwa amevunja Katiba, kanuni, maadili, miongozo, taratibu na itifaki za chama kwamba yeye ndiye aliyeandika (kwa kutumia jina bandia) kwenye mitandao ya kijamii, waraka uliojaa uongo, upotoshaji na uchonganishi kwa wanachama na viongozi.
“ Idara ya Habari ya Chadema imechukua hatua ya kuanza kutoa na kuandaa utolewaji wa taarifa rasmi zinazojibu uongo, upotoshaji na uchonganishi ulioandikwa na Mwigamba, ili kuweka kumbukumbu sawa, wanachama na Watanzania wote waelewe,” ilisema taarifa hiyo.
Ilisema itashughulikia zaidi ufafanuzi juu ya suala la kikatiba la ukomo wa uongozi ndani ya chama na kuendelea kumshutumu Mwigamba, kwamba kupitia vyombo vya habari ameendelea kutunga mambo yasiyokuwapo badala ya kuwasilisha hoja kama anazo, kupitia vikao halali vya chama ambavyo yeye ana uwezo wa kuviitisha au kuhudhuria.
Taarifa hiyo ilisema katika kikao cha Baraza la Uongozi wa Kanda ya Kaskazini (Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Arusha), muda mfupi kabla Mwigamba hajatuhumiwa kwa usaliti na hujuma, alikuwa amewasilisha taarifa ya hali ya chama katika mkoa wa Arusha akisifia viongozi wa chama Taifa kwa kusimamia maslahi na matakwa ya Watanzania katika hoja au ajenda mbalimbali na kuendesha chama vizuri.
“Akamsifia Mbunge wa Arusha Mjini (Godbless Lema), kwa juhudi zake za uenezi na uimarishaji wa chama…baada ya kubainika kwa tuhuma hizo, pamoja na uthibitisho uliokuwa chini ya waraka huo, uliotumika na wataalamu wa kompyuta kubainisha pasi na shaka kuwa waraka ule umetoka na umehifadhiwa kwenye kompyuta yake, Mwigamba alikana kabisa mbele ya kikao, akisema hahusiki wala haijui ilitokea wapi. Lakini jana (juzi) mbele ya waandishi wa habari aligeuka ghafla na kusema ni yake,” ilibainisha taarifa ya Makene.
Kuhusu madai ya uongozi wa juu wa chama kuchakachua Katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa kushika madaraka ya uongozi ndani ya Chadema inajitetea kwamba hayana ukweli kwa kadiri ya ufahamu wa Katibu Uenezi wa chama hicho, John Mnyika.
Mnyika taarifa yake inayohusishwa na taarifa ya Makene jana, anaeleza kuwa mwaka 2006 hakukufanyika marekebisho ya Katiba bali Katiba iliandikwa upya kutoka ile ya mwaka 2004. “Waraka uliandikwa nchi nzima kwa wanachama kutoa maoni na kuwasilisha makao makuu kuanzia kwenye ngazi zao za chini za kikatiba”.
Baada ya kukusanya maoni, alisema Mnyika, kulikuwa na timu tatu; moja ikihusu kuandika falsafa na itikadi ya chama ambayo Mwenyekiti wake alikuwa Profesa Mwesiga Baregu na Katibu wake akiwa yeye.
Alisema sehemu zingine katika Katiba kwa sehemu kubwa kazi ya kuunganisha maoni mapya na kufanya pia rejea kwenye Katiba ya zamani ilifanywa na timu ya watu watatu ikiongozwa na muasisi wa chama, Victor Kimesera, wengine wakiwa ni Mkurugenzi Benson Kigaila na yeye.
Kulikuwa na timu nyingine ya kuandaa miongozo ya mabaraza ya chama: Baraza la Wazee, BAVICHA na BAWACHA ambao nao walifanya kazi kwa upande wao na alishiriki kupendekeza mwelekeo na mapitio ya kulinganisha rasimu ya miongozo yao na rasimu ya Katiba ya chama.
“Kwa ninavyokumbuka, hicho kinachoitwa kipengele kinachozuia kiongozi kuongoza kwenye nafasi moja kwa zaidi ya vipindi viwili vya miaka mitano mitano, hakijawahi kuingizwa kwenye Katiba mpya ya Chadema,” ilisema taarifa ikimnukuu Mnyika.
Ilisema mwaka 2009 Chadema ilifanya uchaguzi mkuu nchi nzima ambapo vifungu vya masuala ya uchaguzi wa ndani ya chama vilifanyiwa rejea mara kwa mara. Kuanzia mwaka 2010 mpaka 2013 ilisema taarifa, madai hayo hayakupata kutolewa kwenye kikao chochote cha kikatiba katika ngazi ya Taifa.
“Madai kama hayo yangetolewa na asiye mwanachama au walau mwanachama wa kawaida, tungesema ni maoni ya kawaida yaheshimiwe na aelimishwe. Lakini madai kama hayo yakitolewa na kiongozi wa chama mwenye nafasi ya kuujua ukweli wote huo yanaacha maswali kuhusu dhamira yake. Naamini mamlaka zinazohusika za chama zitatumia Katiba, kanuni, maadili na itifaki kuchunguza na kuchukua hatua kuanzia kwenye ngazi huko tukio lilikotokea,” ilisema taarifa.
Katika taarifa yake kwa wanahabari juzi, Mwigamba alisema: “ Ni muhimu wana Chadema mkafahamu kwamba kitendo cha kuondolewa kwa kipengele hicho ndicho kinacholeta mpasuko leo kwenye chama unaotokana na Mbowe (Freeman) na Zitto (Kabwe) kupigania uenyekiti.
“Kama kingekuwepo leo Mbowe alikuwa anakatazwa na Katiba kugombea kipindi cha tatu na hivyo vita iliyopo kati yake na Zitto isingekuwepo na chama kingekuwa imara zaidi. Ni dhahiri Mbowe aliondoa kipengele hicho kwa makusudi ili aweze kuendelea kugombea bila mwisho na huu ni udikteta kama ule tu wa akina Lyatonga Mrema, John Cheyo na wengineo, na wana Chadema hatupaswi kuuruhusu si kwa Mbowe tu, bali kwa yeyote atakayepata nafasi ya kuwa mwenyekiti wa chama chetu.”

No comments:
Post a Comment