Tuesday, December 31, 2013

SERIKALI TATU YAENDELEA KUTAWALA RASIMU YA KATIBA MPYA...

Jaji Joseph Warioba akihutubia wakati alipowasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba, Dar es Salaam, jana.
Muundo wa serikali tatu umeendelea kuwa ndani ya Rasimu ya Katiba iliyokabidhiwa jana kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na ambacho Tume ya Mabadiliko ya Katiba imesema ndiyo itakuwa suluhu ya malalamiko juu ya kero za Muungano.

UTAFITI: VINYWAJI VYA KUONGEZA NGUVU MWILINI NI HATARI KWA AFYA...

Vinywaji baridi vyenye lengo la kuongeza nguvu vinadaiwa kuwa hatari kwa afya ya watumiaji baada ya kubaini baadhi ya kemikali husababisha madhara mwilini.

JICHO LA TATU...


KAMANDA ERNEST MANGU ATEULIWA KUWA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI

IGP Ernest Mangu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana amemteua Kamishna wa Polisi Ernest Mangu kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini.

Monday, December 30, 2013

MKUU WA DINI YA KIYAHUDI ASHITAKIWA KWA KUFYEKA UUME WA KITOTO KICHANGA...

KUSHOTO: Rabbi Mordechai Rosenberg. JUU: Oparesheni hiyo ilidumu kwa saa 8. CHINI: Sherehe hizo zilifanyika mahali hapa.
Mkuu wa dini ya Kiyahudi kutoka Pittsburgh, Pennsylvania anashitakiwa kwa kufyeka uume wa kitoto kichanga wakati wa sherehe haramu za Bris.

MICHAEL SCHUMACHER MAHUTUTI BAADA YA KUBAMIZA KICHWA KWENYE JABALI...

KUSHOTO: Schumacher alipokuwa akitamba kwenye Formula One. KULIA: Akiserereka kwenye barafu.
Bingwa wa zamani wa mbio za magari za Formula One, Michael Schumacher yuko hoi mahututi hospitalini baada ya kuanguka na kujibamiza kwenye mwamba wakati akicheza mchezo wa kuserereka kwenye barafu akiwa na mtoto wake wa kiume.

MAJANGILI SASA WAFANYA KUFURU, WAUA TEMBO WAWILI KILA SIKU...

Tembo 60 wameuawa na majangili kwenye hifadhi mbalimbali nchini  katika mwezi mmoja tangu operesheni tokomeza isitishwe.

JICHO LA TATU...


KIFO CHA MAMA MJAMZITO CHAZUA TAFRANI SUMBAWANGA...

Kifo cha mjamzito aliyekuwa akijifungua katika kituo cha afya Mtowisa, wilayani Sumbawanga,  kimezua tafrani baada ya wananchi kushambulia gari la kubeba wagonjwa  wakitaka kulichoma kwa madai kwamba limechangia.

Sunday, December 29, 2013

BALOZI WA PAPA ATAKASA KANISA LILILOPIGWA BOMU ARUSHA...

KUSHOTO: Askofu Fransisco Padilla. KULIA: Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti siku lilipopigwa bomu.
Hatimaye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi la Olasiti jijini hapa lililopigwa bomu Mei 5 mwaka huu na kuahirishwa uzinduzi wake, limezinduliwa jana na Balozi wa Papa na Mwakilishi wa Vatican nchini Tanzania, Askofu Fransisco Padilla.

JICHO LA TATU...


AUA MKEWE KWA KUMCHARANGA MAPANGA BAADA YA KUDAIWA UNYUMBA...

Kamishna Dhahiri Kidavashari.
Mwanamke  mkazi  kitongoji  cha Tulieni  kijijini Tumaini  wilayani  Mlele, Rehema  Lubinza (47) ameuawa  kikatili  kwa  kucharangwa  na mapanga na mumewe  kisha  mwili  wake  kufungiwa  ndani  ya nyumba  yake  kwa  siku  tatu.

Saturday, December 28, 2013

ASILIMIA 96 YA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA KUJIUNGA SEKONDARI...

Asilimia 96.15 ya wanafunzi wa darasa la saba waliofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu na kufaulu, ndio waliochaguliwa kujiunga na sekondari za serikali.

APIGWA HADI KUFA KATIKA FUMANIZI LA MAPENZI KIGOMA...

Mtu mmoja mkulima na mkazi wa eneo la Kumsenga wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, aliyefahamika kwa jina la Yusuph Pascal, ameuawa kwa kupigwa na vitu mbalimbali katika tukio linalodaiwa kuwa ni fumanizi la mapenzi.

BOMBA LA GESI LAAJIRI VIJANA 400, WATAALAMU 200 WAZAWA PIA KUAJIRIWA...

Mradi wa ujenzi wa bomba la gesi umetengeneza ajira mpya 400 kwa vijana tangu ulipoanza Agosti. 

JICHO LA TATU...


POLISI YAPIGA MARUFUKU ULIPUAJI FATAKI MWAKA MPYA...

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limepiga marufuku ulipuaji wa fataki wakati wa sherehe za mkesha wa Mwaka Mpya, kutokana na sababu za kiusalama.

BEI YA VITALU UTAFITI WA GESI ASILIA HAIKAMATIKI...

Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limetangaza kuyaalika rasmi makampuni ya wazawa yenye uwezo wa kifedha na kitaalamu kushiriki katika zabuni  ya kutafuta wawekezaji wa vitalu vya utafiti wa gesi asilia sambamba na makampuni ya nje, huku gharama zake zikionekana kuwa `mlima mrefu’.

Friday, December 27, 2013

AUAWA KWA KUKUTWA UCHI KWENYE SHIMO LA DHAHABU...

Mkazi wa Kijiji cha Kapanda  Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi, Yunge  Maboja  (70)  amekufa  baada ya kushambuliwa  na wananchi  kwa kupigwa na  silaha za jadi, ngumi na mateke  baada ya kukutwa mtupu  usiku wa manane kwenye shimo la kuchimba dhahabu.

JICHO LA TATU...


MBARONI KWA KUSAFIRISHA MAITI YENYE DAWA ZA KULEVYA...

Polisi mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti akiwa na kete 17 tumboni kati ya 24  zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya wakitokea mjini Tunduma, mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam.

MAWAZIRI WANNE WALIOTIMULIWA WAZUNGUMZIA KILICHOWASIBU...

Mawaziri waliotimuliwa, kutoka kushoto ni David Mathayo, Shamsi Vuai Nahodha, Emmanuel Nchimbi na Khamis Kagasheki.
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri watatu na mmoja kujiuzulu, kutokana na kashfa zilizotokana na Operesheni Tokomeza Ujangili, viongozi hao wamezungumza yaliyowasibu kila mmoja kwa staili yake.

Thursday, December 26, 2013

WALAJI NYAMA YA NGURUWE HATARINI KUPATA UGONJWA WA KIFAFA...

Nyama ya nguruwe.
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimehadharisha walaji wa nyama ya nguruwe nchini, kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa.

MWANAMKE AMUUA MPENZI WAKE KWA KUMVUTA KORODANI ZAKE...

Jeshi la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mwanamke na mkazi wa Kijiji cha Usiulize wilayani Meatu kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumvuta korodani, kutokana na wivu wa kimapenzi.

JICHO LA TATU...


GESI, MAFUTA, DHAHABU NA PEMBE ZA NDOVU KUIANGAMIZA TANZANIA...

Mtambo wa Gesi ya Msimbati.
Watanzania wametakiwa kuwa makini na mali na rasilimali za nchi, ikiwemo gesi, mafuta, pembe za ndovu na dhahabu kwani zimeanza kuonesha dalili za kugawa Taifa.

WATOTO 124 WAZALIWA MKESHA WA SIKUKUU YA KRISMASI DAR...

Baadhi wa wazazi katika Hospitali ya Mwananyamala.
Watoto 124 wakiwemo wa kiume 80 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za Dar es Salaam  huku wengi wakiwa wa kiume.

Wednesday, December 25, 2013

ALIYEMUUA KIKATILI DEREVA WA BODABODA NAYE AUAWA KIKATILI...

Jacob Mwaruanda.
Wananchi  wamemuua mtuhumiwa wa  mauaji  wakati akijaribu kutoroka kutoka  mjini  Namanyere  wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.

RASIMU YA MAHAKAMA YA KADHI ZANZIBAR YAIVA...

Msikiti mkongwe wa Chake Chake, Pemba.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema Rasimu ya Mahakama ya Kadhi imekamilika na inatazamiwa kuwasilishwa katika ngazi za makatibu wakuu kabla ya kufikishwa  kwenye Baraza la Mapinduzi.

JICHO LA TATU...


MAENEO YA PWANI KUKUBWA NA DHORUBA...

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imehadharisha juu ya kutokea upepo mkali utakaoambatana na mawimbi makubwa katika maeneo ya pwani mwa bahari ya Hindi leo.

LIPUMBA AIONYA CHADEMA KUHUSU MGOGORO...

Profesa Ibrahim Lipumba.
Chama cha Wananchi (CUF) kimekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kumaliza mgogoro wake ili kuweka nguvu kwenye Bunge la Katiba linalotarajiwa kuanza mwakani.

Tuesday, December 24, 2013

MJANE MWEUPE SAMANTHA ANASWA AKIONDOKA KAMBI YA MAFUNZO YA KIGAIDI KWA NGAMIA...

Samantha Lewthwaite.
Mjane mweupe wa Uingereza anaaminika kuwa anasuka mipango mipya ya mashambulio ya ugaidi kutoka kwenye kambi ya mafunzo inayohusishwa na Al Qaeda baada ya kuonekana akiondoka kwa kutumia ngamia katika msitu wa nyoka wa kufugwa nchini Somalia.

JICHO LA TATU...


KANISA LAAMRIWA KUZIMA KENGELE ZAKE, KISA? ZINA MADHARA KWA AFYA...

Kanisa la St. Mary's.
Kanisa moja limefungiwa kupiga kengele zake usiku sababu kelele hizo 'zina madhara kwa afya'.

Monday, December 23, 2013

MUME NA MKE WAMCHANGIA MTALAKA NA KUMNYOFOA MDOMO RUVUMA...

Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linafanya uchunguzi kuhusu tukio la mume na mke kumshambulia mtalaka wake Faustina Komba (35) mkazi wa jiji la Mbeya kwa kumpiga ngumi, makofi na kumng'ata mdomo wake wa chini na kuuondoa wote.

POLISI WAKIRI KUFANYA MAKOSA OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI...

Haya ni moja ya mateso yanayodaiwa kufanywa dhidi ya raia wakati wa utekelezaji operesheni hiyo.
Jeshi la Polisi, limekuwa la kwanza kati ya taasisi saba zinazohusika moja kwa moja, kukiri udhaifu katika utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyowaondoa mawaziri wanne katika nafasi zao.

WAZEE WACHACHAMAA WINNIE KUTEUA KIONGOZI WA FAMILIA YA MANDELA...

Winnie Mandela.
Wazee wa ukoo wa kichifu wa Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, AbaThembu, wameelezea kukasirishwa na kauli ya mke wa zamani wa kiongozi huyo, Winnie, kumteua mwanawe wa kike, Makaziwe kuwa Mkuu wa familia.

JICHO LA TATU...


SERIKALI KUAJIRI WALIMU 26,000 KUANZIA MWEZI UJAO...

Kassim Majaliwa.
Serikali imetangaza kutoa ajira mpya 26,000 za walimu kuanzia Januari mwakani, ikiwa ni mpango endelevu wa kupunguza uhaba wa walimu  katika shule za msingi na sekondari nchini.

Sunday, December 22, 2013

HOTUBA YA MIZENGO PINDA AKIHITIMISHA MOJA YA MIKUTANO YA KUVUTIA YA BUNGE...

HOTUBA YA MHESHIMIWA MIZENGO P.  PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WAKATI WA KUHITIMISHA SHUGHULI ZA MKUTANO WA 14 WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TAREHE 21 DESEMBA, 2013

I:    UTANGULIZI 
    Masuala ya Jumla

Mheshimiwa Spika,

Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo. Tumekuwepo hapa Dodoma kwa takriban siku 15 za kazi ambapo tumeweza kutekeleza majukumu na kazi za Mkutano wa 14 wa Bunge lako Tukufu ambapo tunahitimisha shughuli zilizopangwa hivi leo.

Mheshimiwa Spika,
Nitumie nafasi hii ya mwanzo kabisa kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Asha Rose Migiro, (Mb.) kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge katika Bunge lako Tukufu.  Wengi wetu tunafahamu uwezo mkubwa wa Dkt. Asha Rose Migiro na bila shaka ndiyo sababu Mheshimiwa Rais alifanya uamuzi wa kumteua kuwa Mbunge kwa kuzingatia sifa nzuri alizonazo. Pamoja na kumpongeza napenda kumtakia kazi njema ndani na nje ya Bunge lako Tukufu.

Mheshimiwa Spika,
Tangu Mkutano wa 13 wa Bunge baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wamepotelewa na Ndugu, Jamaa na Marafiki.  Napenda kutumia fursa hii kuwapa pole wote waliofikwa na misiba hiyo. Lakini katika Mkutano huu, Waheshimiwa Wabunge walipata fursa ya kujadili Azimio la Bunge kuhusu kuungana na Nchi ya Afrika Kusini, katika kuombeleza kifo cha Muasisi, Mpinga ubaguzi wa rangi, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, Hayati Nelson Madiba Mandela kilichotokea tarehe 5 Desemba 2013.  Wote tunakubaliana kwamba huu ni msiba Mkubwa kwa Dunia nzima na hasa kwa wale wanaomfahamu Mzee Mandela na historia yake. 

Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutuwakilisha vyema Watanzania wote katika msiba huu mkubwa wa Afrika na Dunia nzima.  Hotuba ya Mheshimiwa Rais aliyoitoa wakati wa mazishi ya Hayati Nelson Mandela tarehe 15 Desemba, 2013 pale Qunu ilitosha kabisa kuitangaza Tanzania Dunia nzima katika ushiriki wake kwenye harakati za ukombozi Barani Afrika katika Karne ya 20.  Ninaamini kwamba hiyo ni Historia ambayo haitafutika vizazi vingi vijavyo. Tutaendelea kumuenzi Mzee Mandela kwa kuiga na kufuata nyayo zake.

MAZIKO YA MANDELA UTATA MTUPU, BAADHI WAHOJI KAMA ALIVIRINGWA NGOZI YA NG'OMBE...

Jeneza lenye mwili wa Mzee Nelson Mandela wakati wa heshima za mwisho kijijini Qunu.
Siku ya maziko rasmi ya kiongozi wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Mzee Nelson Mandela katika kijiji alichokulia cha Qunu, jimboni Eastern Cape, Desemba 15, hakuna mtu aliyeshuhudia mila zikifanyika nje ya wanafamilia.

PINDA ATANGAZA VITA NA WALAFI SERIKALINI, 866 WASHUGHULIKIWA...

Mizengo Pinda.
Watumishi 866 wa serikali wamechukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa ubadhirifu wa fedha katika halmashauri mbalimbali nchini.

JICHO LA TATU...


ZITTO AAPA KUENDELEA KUPIGANIA DEMOKRASIA CHADEMA...

Kabwe Zitto katika moja ya mikutano yake Kigoma.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mkoani Kigoma, Kabwe Zitto amesema kuwa ataendelea kupigania haki yake ya kidemokrasia na uwajibikaji ndani ya chama chake hadi dakika za mwisho.

Saturday, December 21, 2013

PADRI KATOLIKI KIZIMBANI KWA KUSHINDWA KUTUNZA MTOTO SINGIDA...

Kanisa Katoliki limeingia kwenye kashfa baada ya mmoja wa mapadri wake katika Jimbo Katoliki Singida, Deogratius Makuri kufikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini hapa, akituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

WAZIRI MUHONGO AMSHUKIA REGINALD MENGI KUHUSU UMILIKI WA VITALU...

Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Reginald Mengi.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema baadhi ya wazalendo nchini wanamiliki vitalu kwa asilimia 70 lakini baadhi yao wanashindwa kuendeleza maeneo na kusisitiza kwamba si kweli kuwa vingi vinamilikiwa na wageni nchini.

JICHO LA TATU...


Friday, December 20, 2013

OPERESHENI TOKOMEZA UJANGILI YAENDA NA MAWAZIRI WANNE...

KUTOKA KUSHOTO: Balozi Khamis Kagasheki, Dk Emmanuel Nchimbi, Shamsi Vuai Nahodha na Dk David Mathayo.
Rais Jakaya Kikwete ametangaza kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne kufuatia wabunge kuungana bila kujali itikadi za vyama vyao na kumshinikiza kwa pamoja Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mawaziri watatu wanaowajibika na Operesheni Tokomeza Ujangili, kuwajibika, kutokana na operesheni hiyo kudaiwa kusababisha vitendo vya kikatili na mauaji kwa wananchi.