Polisi mkoani Morogoro inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti akiwa na kete 17 tumboni kati ya 24 zinazodhaniwa kuwa ni dawa za kulevya wakitokea mjini Tunduma, mkoani Mbeya kwenda jijini Dar es Salaam.
Maiti huyo ametambuliwa ni Mfanyabiashara wa Kariakoo ambaye jina ni Khalid Abdul Kitala (47).
Habari zaidi zinasema kwamba maiti huyo aliyekamatwa alikuwa akisafirishwa na gari lenye namba ya usajili T 887 BSW.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, amethibitisha kukamatwa kwa maiti na gari hilo.
Alisema kwamba askari Polisi wa Kituo cha Mikumi kulichopo Barabara kuu ya Morogoro- Iringa walifanikiwa kuwanasa wahusika baada ya kupewa taarifa na raia wema na kuweka mtego.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa , ilipofika usiku wa saa saba kuamkia juzi walilinasa gari hilo likiwa na watu watatu wakitokea mkoani Iringa kwenda jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo alisema , kutokana na kutiliwa shaka huko, polisi waliamuru mwili huo ufanyiwe uchunguzi na madaktari na baada ya kupasuliwa ulikutwa na kete 17 tumboni zinazodhaniwa ni dawa za kulevya na nyingine saba kwa watuhumiwa hao na kufanya jumla ya kete 24.
“ Kwa sasa tunawashikilia watuhumiwa hawa watatu, tutapeleka kete hizo kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kuthibitisha iwapo ni dawa za kulevya na zina thamani ya kiasi gani ...hatuwezi kueleza zaidi tunasuburi uthibitisho huo,” alisema Kamanda wa Polisi wa Mkoa.
Bila kujata majina yao kwa kuhofia kuvuruga upelelezi, Kamanda huyo alisema , wanamshikilia dereva wa gari hilo na abiria wengine wawili kwa ajili ya uchunguzi zaidi na wapo chini ya ulinzi.

No comments:
Post a Comment