MKUU WA DINI YA KIYAHUDI ASHITAKIWA KWA KUFYEKA UUME WA KITOTO KICHANGA...

KUSHOTO: Rabbi Mordechai Rosenberg. JUU: Oparesheni hiyo ilidumu kwa saa 8. CHINI: Sherehe hizo zilifanyika mahali hapa.
Mkuu wa dini ya Kiyahudi kutoka Pittsburgh, Pennsylvania anashitakiwa kwa kufyeka uume wa kitoto kichanga wakati wa sherehe haramu za Bris.

Rabbi Mordechai Rosenberg, ambaye pia ni mganga wa jadi, alifanya sherehe hizo kwenye Sinagogi la The Tree Of Life huko Squirrel Hill mapema mwaka huu mnamo Aprili 28.
Gazeti la The Huffington Post liliripoti kwamba wazazi hao wameendelea kuhifadhiwa majina yao kuepusha kufichua utambulisho wa mtoto wao huyo.
Mtoto huyo aliyetoka tu kuzaliwa alilazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Watoto ambako madaktari walifanya oparesheni ndogo ya dharura kuunganisha uume huo uliokuwa umeng'olewa.
CBS iliripotiwa kwamba mtoto huyo alihitajika kuongezewa damu mara sita na alilazwa kwa miezi miwili.
Oparesheni hiyo inayohitaji umakini wa hali ya juu ilichukua masaa manane kukamilika.
CBS iliongeza na daktari wa upasuaji aliyejitambulisha kwa jina la Dokta Joe Losee kuhusu utaratibu huo wa oparesheni ndogo.
"Kama kidole chako, kidole gumba chako kikatwa kabisa na kurejeshwa mahali pake, hilo ni jambo la kushangaza kidogo," alisema Losee.
"Wakati fulani, haiwezi kufanikiwa," anasema. "Pale unaporejesha sehemu ambapo inahusisha mishipa ya fahamu, wakati mwingine mishipa ya fahamu haiwezi kupona vema pale ulipounganishia. Hivyo kunakuwa na ukomo wa uhakika."
Oparesheni hiyo ndogo ya mtoto huyo iliripotiwa 'kufanikiwa', lakini endapo au la mtoto huyo atakuwa na matatizo baadaye kwenye maisha bado haijafahamika.
Licha ya tukio hilo la kutisha, mkuu huyo wa dini ya Kiyahudi bado anaendelea na shughuli zake za uganga wa jadi.
CBS ilizungumza na mwanasheria David Llewellyn ambaye anashughulikia kesi zinazohusiana na tohara haramu zinazofanya na waganga wa jadi au daktari.
"Hilo ni jambo zito sana na hutokea mara chache," alisema mwanasheria David Llewellyn.

No comments: