Jacob Mwaruanda. |
Wananchi wamemuua mtuhumiwa wa mauaji wakati akijaribu kutoroka kutoka mjini Namanyere wilayani Nkasi, mkoani Rukwa.
Mtuhumiwa huyo Denisi Gagala (31 ) mkazi wa Kitongoji cha Chanji, Manispaa ya Sumbawanga amekuwa akitafutwa na Polisi kwa zaidi ya miezi miwili iliyopita akituhumiwa kumchinja dereva wa pikipiki 'bodaboda' , Sylvester Mandala.
Inadaiwa kuwa Denis na wenzake walimuua dereva huyo kwa kumchinja kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kuondoka na kichwa hicho kwenda mahali kusikojulikana huku wakiutelekeza mwili wa marehemu katika makaburi ya kitongoji cha Sumbawanga Asilia, Manispaa ya Sumbawanga.
Mkasa huo uliotokea Novemba 6, mwaka huu mjini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema mtuhumiwa huyo jana alikamatwa na wakazi wa mji wa Namanyere ambako alikimbilia kujificha mara baada ya kutenda unyama huo.
"Mtuhumiwa huyo ambaye Polisi ilikuwa ikimtamfuta kwa muda mrefu juzi alikamatwa na wananchi mjini Namanyere akijaribu kutoroka kutoka katika nyumba alikokuwa amejificha.
"Polisi walifika eneo la tukio ili kumuokoa ambapo wananchi hao walitawanyika hata hivyo mtuhumiwa alikufa akiwa amelazwa hospitalini kwa matibabu," alisema Kamanda.
Aidha Kamanda Mwaruanda amesema kwamba hadi sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na kuuawa kwa mtuhumiwa huyo.
Alisema pia kuwa wanaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushirikiana na marehemu kumchinja dereva huyo wa bodaboda ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

No comments:
Post a Comment