PADRI KATOLIKI KIZIMBANI KWA KUSHINDWA KUTUNZA MTOTO SINGIDA...

Kanisa Katoliki limeingia kwenye kashfa baada ya mmoja wa mapadri wake katika Jimbo Katoliki Singida, Deogratius Makuri kufikishwa kwenye Mahakama ya Mwanzo Utemini mjini hapa, akituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake mwenye umri wa mwaka mmoja.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Ferdinand Njau, ilidaiwa, kuwa Padri Makuri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu na Maria Boniphace (26) ambaye  alikuwa mhudumu katika jimbo hilo.
Ilielezwa kuwa  katika kipindi cha uhusiano wao, Padri Makuri alimpa  mimba mtumishi wa jimbo hilo, Maria.
Maria aliiambia Mahakama hiyo  kuwa mara alipopata ujauzito, aliwaarifu wazazi wake ambao walimwendea  Padri na alikubali kuhusika na ujauzito wa binti huyo.
Ilidaiwa kuwa Padri aliahidi kwa maandishi kuwa atatunza mtoto  atakayezaliwa  hadi  atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Maria aliendelea kudai kuwa Padri Makuri alitekeleza ahadi yake hiyo kwa miezi michache tu  kisha  akasitisha huduma hiyo ya kumpa mwanawe matunzo.
Alisema baada ya hapo,  alimfikisha Padri huyo  Idara ya Ustawi wa Jamii ambapo  katika hati ya mkataba, aliahidi kuwa atakuwa anatoa  Sh 80,000 kila mwezi  na iwapo atashindwa kufanya hivyo, afikishwe  mahakamani mara moja.
Hata hivyo, pamoja na ahadi hiyo, Padri Makuri alianza kudai  mtoto huyo si wake,  hivyo akaamua  kuacha kutoa matunzo.

No comments: