KANISA LAAMRIWA KUZIMA KENGELE ZAKE, KISA? ZINA MADHARA KWA AFYA...

Kanisa la St. Mary's.
Kanisa moja limefungiwa kupiga kengele zake usiku sababu kelele hizo 'zina madhara kwa afya'.

Kengele hizo katika Kanisa la St. Mary's huko Ashwell, Hertfordshire, zimekuwa zikirindima kila baada ya dakika 15 kwa miaka 117.
Lakini baada ya kupokea malalamiko 12, Halmashauri ya Wilaya ya North Herts (NHDC) 'ilidaiwa kushurutishwa' kuchunguza kelele hizo.
Kufuatia ukaguzi, tume ikaamua kwamba kengele hizo ni kero na zinatakiwa kuzimwa kati ya Saa 5 usiku na Saa 12 alfajiri.
Uamuzi huo umeibua kelele huku kundi la kampeni ya Okoa Kengele likidai kanisa hilo limekuwa 'likishinizwa' na halmashauri hiyo.
Chris Pack, anayeongoza kampeni hiyo, alisem: "Wanasema wamefurahishwa kuna makubaliano lakini hilo sio suluhisho.
"Sasa tutafanya kampeni kubwa zaidi kubadili uamuzi wa halmashauri ya parokia hiyo sababu wamechukua mtazamo huo kutokana na shinikizo la NHDC."
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Parokia ya Ashwell, Peter Long alidai jana 'sehemu kubwa ya wanakijiji hawajisumbui'.
Lakini alisema kanisa hilo lililazimika kukubali kuzima kengele hizo wakati wa usiku sababu 'halmashauri hiyo inaweza kutoa waraka wa kuzuia kabisa kelele kama tusingefanya hivyo'.
Alisema: "Kisha tungeweza kabisa kukata rufaa na tulitaka kukwepa kupoteza fedha za jamii katika taratibu za kisheria."
Halmashauri ya Parokia ya Ashwell imezitaka vigango vya St Albans kama zitaweza kurekebisha mida kuhakikisha kengele hizo kutolia kati ya saa hizo zilizotajwa.
Pia imekata rufaa kuweza kulipwa gharama za Pauni za Uingereza 1,900.
Kengele hizo zilizimwa kwa miezi 18 wakati zikifanyiwa ukarabati, lakini zikarejeshwa tena Juni, 2012.

No comments: