Samantha Lewthwaite. |
Samantha Lewthwaite, mwenye umri wa miaka 29, anashukiwa kusaidia kuratibu shambulio katika jengo la biashara la Nairobi mnamo Septemba ambalo lilisababisha vifo vya watu 67.
Inaaminika mtuhumiwa huyo wa ugaidi alisafirishwa katika gari la 4x4 kuvuka mpaka wa Kenya kwenda nchini Somalia ambako tangu wakati huo alionekana mara nne.
Kuonekana kwake kwa hivi karibuni kabisa kulikuwa wiki mbili zilizopita, pale mashushushu walipomwona mama huyo wa watoto wanne akiendesha ngamia kati ya kambi za mafunzo mjini Baidoa.
Samantha, mjane wa mmoja wa walipuaji wa 7/7 mjini London, sasa anaaminika kuwa katika kambi ya mafunzo iliyojificha katika msitu huo ambayo inaendeshwa na makundi ya kigaidi yanayohusishwa na Al Qaeda.
Kanali Yasin Hiro wa Jeshi la Serikali ya Somalia alieleza: "Amekuwa akisafiri kwa kutumia ngamia. Tunadhani yuko kwenye kambi hizo. Tunatumaini nyoka hao na nge wanampenda."
Kiongozi huyo wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab, kutoka Aylesbury, Buckinghamshire, kwanza alisafiri kwenda Somalia baada ya mauaji ya kimbari kwenye jengo la biashara mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, kisha alisafirishwa kwa boti kuelekea ufukwe mmoja usiofikika kwa urahisi kabla ya kuendelea kwenda katika maficho ya Raas Kaambooni.
Samantha kisha akaonekana akielekea Kismayu - ngome kuu ya zamani ya magaidi - kabla ya kuelekea tena Barawe kwa kutumia boti iendayo kasi.
Ofisa wa Umoja wa Mataifa, Guled Mohamed alieleza: "Watu katika mji huu mzuri mno wa zamani wa Wareno wana ngozi nyeupe na macho ya kibluu hivyo anaweza pia kujichanganya nao."
Kuonekana kwa mwisho Mwingereza huyo kulikuwa wakati akisafiriki kwa kutumia ngamia kwenda Baidoa ambako Jeshi la Serikali ya Somalia linapigana na magaidi takribani 8,000.
Inahofiwa wajahidina hao wanatumia kambi hiyo kuandaa mashambulio zaidi ya kigaidi.
Interpol imetoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Samantha baada ya kutajwa kama mmoja wa watuhumiwa muhimu walioshiriki katika mauaji ya kimbari katika jengo la biashara la Westgate mjini Nairobi mwezi Septemba.
Samantha pia anasakwa nchini Kenya kwa tuhuma za kuamuru mauaji ya viongozi wawili wakuu wa Kiislamu, mahubiri wawili wa Kilokole, na wengine watatu waliohusishwa na Al-Shabaab.
Kamanda wa polisi wa East Kenya, Aggrey Adoli alisema: "Tunaamini Samantha Lewthwaite anahusika na mauaji haya na pia genge la watu wengine.
"Tunaamini alihusika katika kuajiri wanajihadi na kuwasuka wanaharakati wa Al-Shabaab na Al Qaeda katika nchi hii kwa kushirikiana na wengine binafsi wenye mtazamo kama huo. Pale tutakapomtia nguvuni Samantha atakuwa na maswali mengi ya kujibu.
"Bila shaka yoyote ni tishio kubwa kwa taifa na usalama wa kimataifa. Tunafanya kazi saa zote kuweka kumdhibiti asiweze kuleta madhara makubwa zaidi."
Ofisa huyo alisema Samantha anatafutwa kwa mashitaka ya 'mauaji na kuwachochea vijana wa Kiislamu kujiingiza kwenye vurugu'.
No comments:
Post a Comment