Hii ndio penalti ya 'kizembe' zaidi katika mechi kubwa iliyopigwa na Romelu Lukaku ambayo iliigharimu timu ya Chelsea ya England na kujikuta ikishuhudia Bayern Munich ya Ujerumani ikibeba Super Cup jana mjini Prague. Katika mechi hiyo ambayo Chelsea ilionekana kama ingeibuka na ushindi, timu zote zimaliza dakika 120 kwa sare ya 2-2 wakati Wajerumani hao wakisawazisha mara mbili huku bao la pili likifungwa na Martinez zikiwa zimesalia sekunde mbili za muda wa ziada. Jambo la kufurahisha ni kwamba mabao yote ya Chelsea yalifungwa kwenye lango moja na yale ya Bayern yakifungwa kwenye lango jingine.
Saturday, August 31, 2013
MKE ADUNDWA NA KUTIMULIWA KWA KUASI KANISA ANALOSALI MUMEWE...
![]() |
Biblia Takatifu. |
Bila yeye mwenyewe kutarajia, mke wa ndoa amejikuta akicharazwa bakora na kutimuliwa nyumbani na mumewe baada ya mama huyo kuacha kuabudu katika madhehebu ya Katoliki alikofunga ndoa na mumewe aitwaye Martin Kikondo (50) na kuamua kubatizwa na kuanza kusali katika Kanisa la Assemblies (EAGT).
KIONGOZI WA DHEHEBU LA WANAOKULA NYAMA ZA BINADAMU AUAWA NA WANAKIJIJI...
![]() |
Kiongozi huyo, Stephen Tari akiwa hoi kwa kipigo kutoka kwa wanakijiji. |
Kiongozi mmoja wa madhehebu ya wanaokula nyama za watu akijiita Yesu Mweusi, ambaye aliwachinja wafuasi wake wa kike wanaojulikana kama 'Flower Girl' na kunywa damu yao, amejiua mwenyewe kwenye misitu minene ya Papua New Guinea.
PACHA ALIYETENGANISHWA MUHIMBILI ASUBIRI KUTENGENEZEWA NJIA YA HAJA KUBWA...
![]() |
Madaktari wakifanya upasuaji katika Hospitali ya Muhimbili. |
Saa 24 mara baada ya upasuaji wa kuwatenganisha watoto mapacha waliokuwa wameungana uliofanywa na jopo la madaktari bingwa saba, kutoka Hospitali ya Muhimbili (MNH) na Taasisi ya Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu na Mifupa (MOI), Dar es Salaam, mtoto mlengwa wa upasuaji huo ameonesha maendeleo mazuri na sasa ameanza kunyonya bila ya usumbufu.
Friday, August 30, 2013
Thursday, August 29, 2013
TAARIFA YA MSIBA...
*********************************
*********************************
MAMA NJILIMA AMETUTOKA!!
MAMA NJILIMA AMETUTOKA!!
Familia ya Mzee Duncan Njilima wa Ubungo N.H inasikitika kutangaza kifo cha mama yao kipenzi, (mama wa Wendy, Janet, Masunga, Bruce na Mandago) kilichotokea leo asubuhi baada ya kuugua kwa muda mfupi. Msiba na mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwao kota za Ubungo N.H jirani na Hoteli za Sharon na Whitemark. Bwana ametoa, Bwana ametwaa, Jina lake libarikiwe. Amina.
*********************************
*********************************
Wednesday, August 28, 2013
Tuesday, August 27, 2013
Monday, August 26, 2013
Sunday, August 25, 2013
Saturday, August 24, 2013
UFISADI!! BILIONI 9/- ZATEKETEA BANDARI KWA VIKAO VIWILI TU VYA WAFANYAKAZI...
![]() |
Bandarini Dar es Salaam. |
Kamati ya Bunge Hesabu za Serikali (PAC) imemwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, kukagua maeneo matatu ya matumizi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) ili kubaini mianya ya ubadhirifu, ikiwa ni pamoja na matumizi ya Sh bilioni 9 kwa ajili ya vikao viwili tu kwa mwaka.
MAREHEMU DAUDI MWANGOSI SASA AGEUZWA MTAJI WA KISIASA...
![]() |
KUSHOTO: Marehemu Daudi Mwangosi. KULIA: Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwangosi. |
Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari nchini (UTPC), umekionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) dhidi ya kutumia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Wanahabari mkoani Iringa (IPC), Daudi Mwangosi kama mtaji wa kisiasa.
Friday, August 23, 2013
Thursday, August 22, 2013
Wednesday, August 21, 2013
MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE WAPATA AJALI DODOMA...
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Kiongozi wa Mbio hizo Kitaifa, Juma Ali Simai (kushoto) hivi karibuni. Simai na wenzake 9 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo. |
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa, Juma Ali Simai (32) amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa kwenye ajali, iliyotokea kwenye msafara wa mbio za mwenge mjini hapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)