KIBAKA AJIFYEKA MIKONO YOTE BAADA YA KUCHOSHWA NA TABIA YA WIZI...

Ali Afifi.
Mwanaume mmoja raia wa Misri amefyeka mikono yake yote miwili kwa kuitega kwenye njia ya treni iendayo kasi ili kukomesha wizi wake uliokithiri.

Ali Afifi, mwenye umri wa miaka 28, dhahiri alikuwa akitishwa mno na mazoea ya uhalifu wake kiasi cha kujipa hukumu kwa kuifyeka mikono yake mwenyewe.
Mwanaume huyo, dhahidi alikuwa akiongozwa na hukumu za Sheria ya Sharia, ameifyeka bila huruma mikono yake yote katika adhabu yake ya kujihukumu mwenyewe.
Uamuzi wake unaonekana kabisa kwamba umetokana na mafundisho ya Kiislamu ya Sheria ya Sharia - kanuni, masharti na hukumu ambazo zinataarifu kila chembe ya uhai kwa wote walio katika Uislamu.
Afifi alisema 'maradhi' yake ya kuiba yalianza akiwa mdogo, kwanza kwa kuchukua vyakula vya wenzake kwenye Shule ya Msingi. Kisha ikaongezeka kwenda kwenye bishaa katika maduka na hadi hivi karibuni alikuwa akiwakwapulia watu simu za mikononi na vito vya dhahabu.
Alisema alikuwa akitoa fedha alizopata kutokana na wizi huo kwa watoto na familia za mafukara.
Lakini Afifi hakuwa na uwezo wa kuendana na hatia hiyo na kuamua kukata kabisa mikono yake na kuhitimisha kabisa mazoea yake hayo yasiyoweza kudhibitika.
Alisema anataka kusaidia mji wake anaoishi, kuboresha majengo na kujenga kituo cha vijana. Pia anataka kuoa lakini ana mashaka kama mwanamke wa Misri anaweza kumkubali kwa sababu ya historia yake ya wizi.
Mfumo wa sheria wa Kiislamu unahusika na mambo mengi yanayoelezewa katika sheria ya kidunia pia kutaarifu maamuzi ya kila siku binafsi na mambo ya kidunia, ikiwamo usafi, kufunga, kuswali, lishe, siasa, kujamiiana na sheria za ndoa.
Tafsiri ya  sheria hiyo kwa Waislamu inatofautiana kati ya tamaduni, lakini inakubalika katika nchi kadhaa kwamba kurudia kuiba adhabu yake ni kukata mkono huo.
Kawaida, mtu aliyekamatwa akiiba anaweza kushitakiwa kwenye mahakama ya Kadhi ambako wanasheria wa Kiislamu watatoa mwongozo kuhusiana na suala hilo.
Lakini kwa Afifi, anayetokea katikati ya mkoa wa delta ya Nile wa Tanta, Misri, aliamua akijua hukumu itayomkabili, kwa mujibu wa 'ubashiri wa sheria' hiyo.
Kwa mujibu wa Sharia, kuiba kunachukuliwa kama moja ya makosa makubwa kama ilivyoainishwa katika Kur'an Tukufu.
Mahakama ya Kadhi inaweza kutoa hukumu ya majeraha ya aina fulani kwenye mkono huo kwa aliyekamatwa akiiba kwa mara ya kwanza, kama kupitisha gari taratibu juu ya mkono huo.
Katika nchi kama Iran, Saudi Arabia na kaskazini mwa Nigeria, adhabu ya kukatwa kiungo kwa kurudia kuiba bado inatumika. Nchini Misri, hatahivyo, mahakama hazijaruhusiwa kutoa hukumu ya kukata viungo kwa miaka mingi sasa.
Mwaka jana, hatahivyo, chini ya serikali mpya ya Muslim Brotherhood, Mbunge Adel Azzazy, kutoka chama cha Nour, alipendekeza muswada wa kukata viungo kwa makosa fulani.

No comments: