BINTI ALIYEKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA PERU AONJA MACHUNGU YA JELA...

Mabinti hao, Melissa Reid na Michaella.
Melissa Reid ameandika barua kutoka gerezani kwenda kwa wazazi wake katika Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake akiwaeleza 'niombeeni'.

Melissa ambaye ametimiza umri wa miaka 20 akiwa ndani ya selo ya polisi, aliandika barua hiyo kwa mama yake Debra, kaka Liam, mwenye miaka 22, na dada zake mapacha Stephanie na Jennifer, wenye umri wa miaka 18, nchini Scotland.
Katika namna ya kuhuzunisha, aliandika: "Hii ni bethdei moja ambayo nitakuwa nikisahau ASAP! Najua kwamba mnafanya kila muwezalo lakini inakatisha tamaa na ngumu kwangu pale unaposhughulika na polisi kama hivi na baada ya siku 9 bado wanarandaranda tu wakituhoji!"
Barua hiyo iliyoandikwa kwenye pande zote mbili, iliyoandikwa kwenye karatasi ya A4, imefichua mahangaiko ya Melissa kuhusu maisha ndani ya gereza.
Aliandika: "Kila kitu hapa ni rushwa kama ulivyosema ni pesa tu, hasa katika jela!!! Nilisikia habari lakini ninahitaji kuwa imara sababu inaweza tu kuwa maneno ya mdomoni!"
Kuhusiana na mfungwa mwenzake, aliandika: "Nimepata dada wa maisha Michaella. Ninasema dada sababu dhamana yetu ndio kwanza inaanza na bila kujali tunayopitia haiwezi kuzuiliwa."
Lakini ukweli wa suala lake ilikuwa dhahiri ameshambulia nyumba.
"Nilikumbana na ugumu hapa mwanzoni. Nilikuwa nikilia mno humu ndani na sikuweza kuendana na vizuizi vya lugha, hakika ilikuwa inachanganya!
"Lakini hiyo ikanipa nguvu zaidi ndani yangu kama kuwaruhusu kunishusha chini kwenye selo, kuniambia nitulie au la sitoruhusiwa kurejeshwa juu," aliandika.
Alimalizia meseji yake yenye hisia kali: "Wote ninawapenda sana. Niombeeni tafadhali na bakieni imara."
Imekuja huku sakata la 'Peru Two' likielekea kufikisha wiki ya tatu.
Tangu wakati huo sura zao zenye mashaka zimekuwa maarufu kote duniani - na kesi yao imekuwa na maoni yaliyogawanyika.
Wakiwa wanatuhumiwa kusafirisha dawa za kulevya kutoka Peru, wanawake hao wawili, wote wenye umri wa miaka 20, wanakabiliwa na hukumu ya hadi miaka 15 jela.
Kwa wakati huu tayari wamepitia uhalisia wa machungu ya gereza la Peru, wakisubiria kesi.

No comments: