Ezekiah Wenje. |
Mbunge wa Nyamagana, Ezekiah Wenje (Chadema) anashikiliwa na Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuchochea maandamano yasiyo na kibali.
Wenje anadaiwa kuchochea maandamano hayo juzi kutoka katika viwanja vya Furahisha, ambapo wafuasi wa Chadema walikusanyika wakitoka Buzuruga wakiwa na ujumbe wa kumtaka mkuu wa mkoa wa Mwanza, awaondolee Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Henry Matata.
Wakiwa uwanjani hapo, Wenje anadaiwa kuwachochea wafuasi hao kuwa mbunge wao waliyemwagiza kwenda ofisi ya mkuu wa mkoa hapatikani kwenye simu, hivyo nao waandamane kwenda huko.
Akizungumza na mwandishi, Mangu alikiri kumshikilia kwa mahojiano kwa saa tatu kwa tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi na yeye mwenyewe kuandamana pamoja na wafuasi wake.
“Hata yeye mwenyewe aliandamana na wafuasi wake kuja kwa mkuu wa mkoa baada ya kuwahamasisha kufanya hivyo katika uwanja wa Furahisha, alirudishwa nyuma na mabomu ya machozi yalipoanza,” alisema Mangu.
Kamanda aliwataka viongozi wa kisiasa, kujenga mazingira ya kuaminika. Mwandishi alimtafuta Wenje kupitia simu yake ya mkononi, hakupatikana.
Juzi jeshi la Polisi mkoani hapa, lililazimika kutumia mabomu ya machozi, kutawanya wafuasi wa Chadema, waliokuwa wakiandamana.
No comments:
Post a Comment