HII NDIO PENALTI YA 'KIZEMBE' ZAIDI ILIYOIGHARIMU CHELSEA KWENYE SUPER CUP...


    
Hii ndio penalti ya 'kizembe' zaidi katika mechi kubwa iliyopigwa na Romelu Lukaku ambayo iliigharimu timu ya Chelsea ya England na kujikuta ikishuhudia Bayern Munich ya Ujerumani ikibeba Super Cup jana mjini Prague. Katika mechi hiyo ambayo Chelsea ilionekana kama ingeibuka na ushindi, timu zote zimaliza dakika 120 kwa sare ya 2-2 wakati Wajerumani hao wakisawazisha mara mbili huku bao la pili likifungwa na Martinez zikiwa zimesalia sekunde mbili za muda wa ziada. Jambo la kufurahisha ni kwamba mabao yote ya Chelsea yalifungwa kwenye lango moja na yale ya Bayern yakifungwa kwenye lango jingine.

No comments: