WAISLAMU WANASWA WAKIVUNJA NA KUCHOMA MOTO MAKANISA...

Mmoja wa Waislamu hao akivunja msalaba uliokuwa juu kabisa ya kanisa.
Video bayana imefichuliwa kutoka Misri ikionesha kuvunjwa kwa kanisa moja la Misri, na sasa kuthibitisha madai kwamba wafuasi wa Rais wa zamani Mohammed Morsi wamekuwa wakitapakaza uchafu kwenye makanisa ya Kikristo.

Picha hizo cha kushitusha zinaonesha kundi la Kiislamu likivunja kanisa hilo mji wa kaskazini mwa Misri wa Sohag, wakivunja samani na kuta na kuchoma moto magari huku wakiondoka.
Mwishoni mwanaume mmoja alikwea mpaka juu ya mnara na kuvunja kisha kuuangusha msalaba chini kwenye eneo la kanisa hilo.
Wafuasi zaidi wa kundi hilo kisha wanauzingira msalaba huo ulioanguka na kuuchapa kwa bakora.
Video hiyo ya dakika sita, iliyochukuliwa na tovuti ya MidEast Christian, ilirekodiwa Agosti 14, mwaka huu.
Siku hiyohiyo mjini Cairo, kambi za mitaani zinazomuunga mkono Morsi zilifanya maandamano na vikosi vya usalama vilifyatua risasi na kuua watu zaidi ya 600, na kuzusha ghasia zaidi na umwagaji wa damu katika nchi yote ya Misri.
Tovuti hiyo ya habari inadai kwamba kundi hilo - ambalo lilijumuisha wanaume na baadhi ya watoto - liligadhibika kufuatia kuondolewa kwa wafuasi wa Morsi kutoka kwenye kambi za mjini Cairo.
Video hiyo inaanzia kutoka mahali fulani panapofaa kutazamia jambo nje ya kuta za kanisa hilo.
Maelezo ya picha hizo yanaeleza kwamba washambuliaji hao waliingia kanisani humo na kuimba "Tunajitolea nafsi zetu na damu kuokoa Uislamu".
Mtazamo huo kisha unaelekea ndani ya kanisa hilo, ambako, kwa mujibu wa maelezo, "Mmoja wa washambuliaji hao alimwamuru mwenzake kuvunja msalaba."
Katikati ya moshi mweusi uliokuwa ukifuka, mwanaume mmoja anamsaidia mwenzake kukwea kwenda kwenda msalaba ulioko juu kabisa ya mnara.
"Waliimba 'Mungu ni mkubwa' huku msalaba ukivunjwa," yalisomeka maelezo hayo, huku wanaume hao wakiangusha msalaba na kuutupa kwenye umati uliokusanyika chini.
Wakristo wa Misri wanasema mamia ya makanisa yao yameshambuliwa na wanachama na wafuasi wa Muslim Brotherhood kufuatia Morsi kung'olewa madarakani Julai 3, mwaka huu.
Wapinzani wanasema rais huyo wa zamani alikuwa akidhamiria kuigeuza Misri kuwa taifa la Kiislamu.
Wakristo wanafanya asilimia 10 ya idadi ya watu wa Misri wanaofikia milioni 80, lakini wafuasi wa Morsi wamekuwa wakiwashutumu kwa kuangushwa kwake, kwa mujibu wa viongozi wa Kanisa la Misri.
Askofu Makarios, kiongozi wa Kanisa la Misri kutoka Minya, aliwashutumu viongozi wa Muslim Brotherhood kwa kupanga mashambulio hayo kwenye makanisa ya Kikristo, nyumba na biashara katika juhudi za kuzidi kuligawa taifa hilo.
"Tulitarajia wiki hizi za matukio kabla ya makanisa kubomolewa, ikiwa ni uthibitisho wa mipango iliyofanywa na viongozi wa Brotherhood dhidi ya Makanisa ya Misri," alisema Makarios.
"Kisha tukashangazwa na mashambulio ya kufanana kwenye makanisa na mali za Kanisa la Misri, mengi kati yao yakitokea katika muda sawa kwenye maeneo tofauti, katika mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa chini ya mpango waliouita 'Plan B', ambao ulilenga makanisa yote kuchomwa moto na kuangamizwa."
Serikali hiyo ya kijeshi imeahidi kujenga upya makanisa ya Kikristo yaliyoharibiwa na makundi hayo.

No comments: