ADHABU YA DOKTA WA PAKISTANI ALIYESAIDIA WAMAREKANI KUMNASA OSAMA YATENGULIWA...

Daktari Shakil Afridi (kulia) aliendesha programu ya chanjo mbele ya makazi ya Osama (pichani kushoto).
Daktari wa Pakistani ambaye alisifiwa kama shujaa baada ya kuwasaidia CIA kumsaka Osama bin Laden amefutiwa hukumu yake ya kifungo cha miaka 33 jela kwa uhaini.

Shakil Afridi alitiwa hatiani Mei 2012 kwa mashitaka yasiyohusiana na tukio hilo la bin Laden la 'njama dhidi ya taifa hilo' kwa kutoa pesa na kutoa huduma za matibabu kwa wanamgambo wa Kiislamu katika eneo la kabila la Khyber nchini Pakistani.
Familia ya daktari huyo na wanamgambo hao wamekanusha madai hayo.
Juzi ofisa wa juu wa mahakama nchini Pakistani alitengua hukumu hiyo na kuamuru kuanza upya kusikilizwa kwa kesi hiyo, kwa misingi kwamba mtu aliyetoa hukumu hiyo hakuwa amethibitishwa kusikiliza kesi hiyo.
Dk Afridi aliendesha programu ya chanjo kwa ajili ya CIA kuweza kukusanya vinasaba katika jaribio la kuthibitisha uwepo wa kiongozi huyo wa al-Qaeda kwenye makazi hayo yaliyoko katika mji wa Abbottabad. Makomandoo wa Marekani baadaye walimuua bin Laden katika makazi hayo mnamo Mei 2011 katika mapambano ya upande mmoja.
Maofisa wa Pakistani walifanyiwa ukatili na oparesheni hiyo ya bin Laden, ambayo ilipelekea mashaka ya kimataifa kwamba walikuwa wakimficha muasisi huyo wa al-Qaeda. Machoni mwao, Afridi alikuwa msaliti ambaye alishirikiana na mashirika ya mashushu wa kigeni katika oparesheni batili ndani ya ardhi ya Pakistani.
Kesi hiyo ilisababisha msuguano kati ya Pakistani na Marekani, kuharibu uhusiano ambao Marekani inautazaman kama muhimu katika kupambana na Taliban na al-Qaeda, pia huku majadiliano kumaliza vita katika nchi ya jirani ya Afghanistani.
Katika Marekani na mataifa mengine ya Magharibi, Afridi alikuwa akitazamwa kama shujaa ambaye alisaidia kumwangamiza mtu anayewindwa zaidi duniani.
Maofisa katika Marekani wametaka Afridi aachiwe huru. Juzi, Msemaji wa Serikali Marie Harf aliwaeleza waandishi kwamba kuendelea kushikiliwa kwa Afridi 'hakika kunapeleka ujumbe usio sahihi.'
"Tunatumaini maendeleo haya ya hivi karibuni yanapelekea matokeo ambayo yanaakisi ukweli ambao unamtia Osama kwenye hukumu ulikuwa dhahiri kwa manufaa ya Pakistani - pia kama wetu," alisema Harf.
Daktari huyo alijaribu chini ya Kanuni za Makosa za Frontier, au FCR, fungu la sheria ambazo zinaongoza uhuru wa kujitawala wa mikoa ya kikabila nchini Pakistani. Mashirika ya haki za binadamu yameshutumu FCR kwa kutowapa watuhumiwa haki ya uwakilishi wa kisheria, kuwasilisha ushahidi, au kuwachunguza mashahidi. Hukumu zinatolewa na ofisa wa serikali kwa kushauriana na wazee wa baraza.
Anis, kamishna anayesimamia utekelezaji wa FCR, aliamuru kwamba Afridi atashitakiwa chini ya kanuni na ofisa wa juu wa kisiasa huko Khyber, alisema Shah. Afridi hapo awali alishitakiwa na msaidizi wa ofisa huyo.
Mwanasheria wa daktari huyo, Samiullah Khan, aliupokea uamuzi huo wa kurejewa kwa mashitaka, akisema: "Nadhani hii ni hatua nzuri kwetu." Aliuita uamuzi wa awali uliomhukumu Afridi kifungo cha miaka 33 jela 'kinyume kabisa cha sheria.'
Haijafahamika kama kurejewa huko kwa mashitaka kutamfanya Afridi aachiwe huru au kupunguziwa adhabu ya awali.

No comments: