Baadhi ya watoto walionusurika wakipatiwa hewa ya oksijeni hospitalini. |
Mvulana wa miaka 13 ameelezea jinsi 'pumzi zake zilivyokatika' wakati harufu yenye sumu ilivyokuwa ikitapakaa kwenye nyumba yao mjini Damascus wakati wa shambulio la gesi linalodaiwa kufanywa na vikosi vya serikali ya Syria.
Mvulana huyo amepewa nafasi ya kwanza kama shuhuda katika shambulio hilo la Jumatano asubuhi ambalo linadaiwa kuua watu takribani 1,700 wakiwa wamelala vitandani mwao.
Ushahidi wake wa kushitua umekuja huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia Watoto (UNICEF) likibainisha kwamba idadi ya watoto wa Syria waliolazimishwa kuihama nchi yao kama wakimbizi sasa imefikia milioni moja.
Na jana vikosi hivyo vya Rais Bashar al-Assad vimekuja kwenye shinikizo jipya kufuatia washirika wake wa karibu Urusi wakimuasa kuruhusu wakaguzi wa Umoja wa Mataifa kwenda kwenye eneo linalodaiwa kutokea mauaji hayo ya kinyama.
Serikali ya Syria imekanusha kufanya shambulio hilo, ambapo madai ya shuhuda wa kwanza yamefichuka jana asubuhi.
Mvulana huyo ambaye ametambulishwa tu kama Abdullah, alielezea jinsi alivyokuwa amelala kitandani wakati shambulio hilo lilipoanza kabla ya kupoteza fahamu Jumatano.
"Nilikuwa nimelala," alilieleza gazeti la Daily Telegraph. "Kisha pumzi zangu zikakatika. Nilijaribu kupandisha ngazi lakini nikashindwa kabisa kupiga hatua. Nilishindwa kabisa kuhimili mwili wangu."
Baba yake na kaka waliuawa, alisema. Mama yake angali hai.
Shuhuda wa pili, aliyetajwa kama Mohammed Ibrahim, umri wa miaka 24, alilieleza gazeti hilo jinsi alivyosikia mlipuko wa kwanza na kukimbilia nje kwenda kusaidia.
Alisema: "Niliwaona wanawake na watoto wakiwa wamelala mitaani wakikata roho au kuanguka ama tayari wakiwa wamekufa, hata watoto wadogo. Nami nikavuta hewa hiyo na kuzirai na sikukumbuka chochote baada ya hapo."
Kama ushahidi wa futuri, Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi jana imegeuka kwa namna ya ajabu
Inakadiriwa nusu ya wakimbizi wote milioni 2 walioorodheshwa kutoka Syria ni watoto, na takribani 740,000 ya wote wako chini ya umri wa miaka 11, kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa ya wakimbizi na watoto.
"Huyu mtoto mkimbizi wa milioni moja si namba nyingine tu," alisema Anthony Lake, mkuu wa UNICEF.
"Huyu ni mtoto halisia aliyekimbizwa kutoka nyumbani, pengine kutoka kwenye familia, akakabiliana na matukio ya kutisha ambayo tunaweza tu kuanza kuyatambua."
No comments:
Post a Comment