Friday, February 28, 2014

BUNGE LA KATIBA LAWEKWA NJIAPANDA KUHUSU KURA YA SIRI...

Kifungo cha kura ya siri katika Rasimu ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, kimeliweka Bunge njia panda baada ya wajumbe bila kujali vyama na makundi, kugawanyika.

CHEKA KIMYA-KIMYA...

Jamaa mmoja mlevi kafika nyumbani kwake akiwa kalewa chakari. Akabisha hodi na mambo yalikuwa hivi. Jamaa: "Mke wangu nifungulie mlango." Mke: "Nasema sifungui maana nimechoshwa na tabia yako ya ulevi!"

MJI WA BAGAMOYO KUWA JIJI LA VIWANDA NA BIASHARA...

Moja ya mitaa ya mji wa Bagamoyo.
Uendelezaji wa maeneo maalumu ya uwekezaji katika mji wa Bagamoyo ukikamilika, utasaidia mji huo kuwa Jiji kubwa la viwanda na biashara na kuchangia katika shughuli za maendeleo ya nchi.

MTAMBO WA KUCHUNGUZA GHARAMA WAJA KUZIBANA KAMPUNI ZA SIMU...

Simu za mkononi.
Kampuni za simu nchini zitaanza kufuatiliwa na mtambo maalumu ili kubaini kila senti zinazoingiza na kuwezesha Serikali kupata kodi yake kikamilifu.

JICHO LA TATU...


KANISA LA MKUNAZINI LALALAMIKIA KUHUJUMIWA ZANZIBAR...

Kanisa la Anglikana Mkunazini, Zanzibar.
Wakati Jeshi la Polisi likisema milipuko ya mabomu karibu na Kanisa la Mkunazini si hujuma, uongozi wa Kanisa hilo umepinga na kusema ni sehemu ya mikakati ya kuzusha taharuki na hofu kwa waumini wake ili washindwe kuendelea na ibada.

Thursday, February 27, 2014

MWENYEKITI BUNGE MAALUMU APIGWA 'STOP' KUHUDHURIA VIKAO VYA CHAMA...

Kikao cha Bunge Maalumu mjini Dodoma.
Wakati kampeni za chini chini za kumpata Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, zikiripotiwa kuonesha mchuano mkali kati ya wajumbe Samuel Sitta na Andrew Chenge, nafasi hiyo imewekewa vizingiti vya kumdhibiti yeyote atakayechaguliwa kushika nafasi hiyo.

MSHITAKIWA WA KWANZA KESI YA UTOROSHAJI TWIGA AUGUA GHAFLA...

Twiga.
Kesi utoroshwaji wa twiga kwenda Uarabuni, imekwama baada ya mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kamran Ahmed, kuugua ghafla muda mfupi kabla ya kufika mahakamani hapo.

JICHO LA TATU...


VIBANDA VYA MAMA LISHE BUNGENI DODOMA VYABOMOLEWA...

Bomoabomoa Dodoma.
Siku moja baada ya mama na baba lishe kusogeza chakula cha bei nafuu  karibu na Bunge, vibanda vya huduma hiyo vilivyokuwa vimejengwa pembezoni mwa barabara, vimebomolewa.

Wednesday, February 26, 2014

SHAHIDI AKIRI MAHAKAMANI KUSHIRIKI KUPAKIA TWIGA KWENYE NDEGE...

Shahidi wa 20 katika kesi ya utoroshaji wa wanyama hai aina ya twiga kwenda Arabuni, amedai kushuhudia wanyama hao wakipakiwa katika ndege saa nane usiku.

CHEKA KIMYA-KIMYA...

Babu mmoja baada ya kuibiwa nauli yake ndani ya daladala, akatangaza: "Jamani aliyeniibia nauli yangu arudishe haraka kabla sijafanya kama mwaka juzi!"

MAMALISHE 'WAWAOKOA' WAJUMBE BUNGE LA KATIBA DODOMA...

Mamalishe akiwa kazini mjini Dodoma.
Wakati wabunge wakisubiri nyongeza ya posho kwa madai maisha Dodoma ni ghali, huduma ya chakula cha bei nafuu, imesogezwa karibu nao.

MADIWANI WA CHADEMA WAJIUZULU MANISPAA YA SHINYANGA...

Kikao cha madiwani Shinyanga.
Mtaji wa viongozi wa Chadema mikoani umeendelea kuporomoka kutokana na mgogoro wa uongozi unaoendelea katika chama hicho, kuanza kukumba viongozi wa kuchaguliwa.

JICHO LA TATU...


MSHITAKIWA KESI YA PAPAA MSOFFE ATISHIA KUJIUA ASIPOACHIWA...

Makongoro Nyerere.
Mshitakiwa Makongoro Nyerere  anayekabiliwa na kesi ya mauaji ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imuachie huru akaishi na watoto wake au ajiue.

NECTA YAFAFANUA ALAMA ZA UFAULU MATOKEO YA KIDATO CHA NNE...

Dk Charles Msonde.
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) limetoa ufafanuzi kuhusu viwango vya ufaulu, alama ya chini ya ufaulu na ufaulu wa jumla, ambavyo vimetumika kwa mara ya kwanza mwaka huu.

Tuesday, February 25, 2014

DINI INAYOZUIA WAUMINI KWENDA SEKONDARI YAIBUKA KIGOMA...

Dini mpya iitwayo Matengenezo inayozuia waumini wake kwenda sekondari na  hospitali, imeingia wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

MASHOGA SASA WAWEKWA KITANZINI, OBAMA AWATETEA...

Baadhi ya mashoga wakisherehekea siku yao.
Hatimaye Rais Yoweri Museveni amesaini Muswada wa Sheria inayoharamisha na kutoa adhabu kali kwa wanaojihusisha na vitendo vya ushoga nchini na wanaowaficha.

JICHO LA TATU...


Sunday, February 23, 2014

MAMA ATAKA KUJITAJIRISHA KWA KUISHI CHOONI WILAYANI HAI...

Mama huyo akiwa na mwanae chooni humo wanamoishi.
Baada ya mvua kubwa na upepo mkali iliyosababisha maafa katika maeneo mengi ya wilaya ya Hai, hali hiyo imeanza kutumiwa ndivyo sivyo na baadhi ya wananchi wakitegemea kunufaika na misaada mbalimbali.

MAKINDA AWACHARUKIA WAJUMBE WANAOTAKA KUTAJIRIKIA BUNGE LA KATIBA...

Anne Makinda.
Spika wa Bunge, Anne Makinda ametaka wanaotarajia kugombea katika uchaguzi  mkuu wa 2015 kujiweka sawa kiuchumi badala ya kutegemea kutajirika wakiwa bungeni.

MASHINE ZA EFDs SASA ZAHAMIA KWENYE MABASI YA ABIRIA...

Mabasi ya mikoani ambayo sasa yataanza kutumia mashine za EFDs.
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo katika mchakato wa kuanzisha mfumo wa mashine za kieletroniki (EFD) katika utoaji wa risiti kwenye mabasi ya abiria, kasino na magari ya mizigo.

PINDA AHOJI WAJUMBE BUNGE LA KATIBA WANATAKA TANGANYIKA IPI?...

Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekiri kuwa Bunge Maalumu la Katiba, limeanza na changamoto, huku akihoji wanaotaka Serikali ya Tanganyika, wanakusudia ipi ya mkoloni au ya baada ya uhuru ya miaka mitatu.

MWENYEKITI, MADIWANI WANUSURIKA SHAMBULIO LA UJAMBAZI KATIKA BAA...

Makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Wilayani Simanjiro, Jackos Sipitek pamoja na madiwani wawili wa viti maalumu wamenusurika  katika shambulio la majambazi kutaka kuwadhuru polisi kwenye baa ya Pama iliyopo makao mapya jijini Arusha.

JICHO LA TATU...


WAZINDUA KUMBUKUMBU YA MIAKA 20 YA MAUAJI YA KIMBARI...

Wapiganaji wa Intarahamwe.
Ubalozi wa Rwanda nchini umezindua kumbukumbu ya miaka 20 ya mauaji ya Kimbari na kuitambulisha kwa jina la Kinyarwanda kuwa ni Kwibuka20, ikiwa na maana ya kukumbuka.

Saturday, February 22, 2014

UFAULU WAPANDA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE, WANAWAKE HAWAKAMATIKI...

Dk Charles  Msonde.
Ufaulu wa watahiniwa wa kidato cha nne mwaka jana umeongezeka kwa mujibu wa taarifa ya matokeo ya mitihani hiyo kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

LORI LAHAMA NJIA NA KUPARAMIA BASI DOGO LA ABIRIA MKURANGA...

Watu watano wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace kugongwa na lori eneo la Mwandege, Mkuranga. Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Usalama Barabarani wa mkoa huo, Edward Mutairuka, chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori ambaye alihama njia na kulifuata basi hilo lililokuwa likitokea Mbagala kwenda Mkuranga.

MKURUGENZI WA ZAMANI MANISPAA YA ILALA KORTINI KWA MAUAJI...

Gabriel Fuime.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Gabriel Fuime (61) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya mauaji.

JICHO LA TATU...


WABUNGE WA KATIBA WAPATIWA KINGA, WAKO HURU KUTOA MAONI...

Jaji Frederick Werema.
Kila mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, ana uhuru wa maoni ambayo hayatahojiwa mahakamani au sehemu yoyote nje ya Bunge hilo.

AFUNGWA JELA MAISHA KWA KUMNAJISI MTOTO MDOMONI...

Mkazi wa  mtaa wa Nsemulwa, Athuman  Mussa (54) amehukumiwa  kifungo cha maisha jela na Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, baada ya kutiwa  hatiani kwa kosa la kumnajisi mtoto  wa kike  mwenye umri wa miaka minne mdomoni.

Friday, February 21, 2014

POSHO YAGAWA WAJUMBE BUNGE LA KATIBA, BAADHI WAKATAA NYONGEZA...

Wajumbe Bunge la Katiba.
Wakati Bunge Maalumu la Katiba likiunda kamati maalumu ya kufuatilia suala la nyongeza ya posho za wajumbe, umetokea mgawanyiko miongoni mwa wabunge hao.

KIKWETE, KAGAME WAPANGA KUKUTANA KUMALIZA TOFAUTI ZAO...

Rais Jakaya Kikwete (kushoto) na Rais Paul Kagame.
Marais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda, wamepanga kukutana mara kwa mara kujadili matatizo yanayoibuka na kuhatarisha amani baina ya nchi hizo.

JICHO LA TATU...


MEMBE APONGEZA KUADHIBIWA WANAOSAKA URAIS KUPITIA CCM...

Bernard Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amepongeza hatua ya CCM kumpa onyo kali na kumweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, kutokana na kubainika kuanza kampeni za urais kabla ya muda.

Thursday, February 20, 2014

WALIOUA MSICHANA NA KUMWAGIA TINDIKALI BAADA YA KUMBAKA SIKU TATU WAHUKUMIWA KIFO...

Eneo ambapo msichana huyo alibakwa kwa siku tatu kabla ya kuuawa.
Wanaume watatu wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini India baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka 'mande' msichana mwenye umri wa miaka 19.

WABUNGE WAKATAA POSHO YA 300,000/-, WASEMA HAILINGANI NA HADHI YAO...

Wajumbe wakiwa kwenye kikao cha Bunge la Katiba.
Wakati mjadala wa kihistoria wa kuunda Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ukiwa katika hatua ya kupata kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, baadhi ya wajumbe wameamua kuelekeza nguvu kudai posho nono.

JICHO LA TATU...


MEMBE KUZUNGUMZIA LEO ADHABU YAKE ALIYOPEWA CCM...

Bernard Membe.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema leo atazungumzia hatua ya CCM kumpa onyo kali na kumweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja.

WATAKAOFANYA VURUGU BUNGE LA KATIBA KUFUNGIWA SIKU KUMI...

Spika wa muda, Pandu Ameir Kificho.
Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba atakayevunja, kujaribu kuvunja utaratibu, amani na utulivu au kuonesha tabia za vurugu kwa kutumia nguvu na mabavu ndani ya ukumbi wa mikutano, atakabiliwa na adhabu ya kuzuiwa vikao kwa siku 10.

Tuesday, February 18, 2014

CHEKA KIMYA-KIMYA...

Jamaa mmoja kaamua kwenda kumtupa paka wake baada ya kuchoshwa na tabia za paka huyo kudokoa mboga jikoni kila mara. Siku moja alfajiri jamaa akambeba paka huyo na kwenda kumtupa mbali.

JICHO LA TATU...


NAFASI YA Z'BAR KATIKA MUUNGANO YAWA GUMZO KWENYE KATIBA MPYA...

Ikulu ya Zanzibar.
Wakati wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakifikiria nani atakuwa Mwenyekiti wao, wasomi karibu 100 waliokutana jana Dar es Salaam, wamejikuta wakiingia katika mjadala wa namna gani Zanzibar itambulike katika Katiba mpya.

KIWANJA CHA MWALIMU NYERERE CHAPIGWA DANADANA KINONDONI...

Hayati Mwalimu Nyerere.
Familia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imeendelea kupigwa chenga na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, walikokwenda mara kadhaa kufuatilia haki ya kiwanja walichoachiwa na baba yao.

WATAKAOTEGA VIKAO VYA BUNGE LA KATIBA KUKATWA POSHO...

Spika Anne Makinda alipokagua ukarabati wa ukumbi wa Bunge kwa ajili ya vikao vya Bunge la Katiba.
Mbunge ambaye hatashiriki shughuli za Bunge Maalumu, hatapewa posho maalumu, isipokuwa ataambulia Sh 80,000 za posho ya kawaida.

EWURA YAPATA MKURUGENZI MKUU MPYA...

Felix Ngamlagosi.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imepata Mkurugenzi Mkuu mpya, Felix Ngamlagosi.

RUBANI MSAIDIZI ETHIOPIAN AIRLINES ATEKA NYARA NDEGE YA SHIRIKA LAKE...

Ndege hiyo mara baada ya kutua.
Rubani msaidizi wa Shirika la Ndege la Ethiopia ameteka nyara ndege ya shirika hilo inayofanya safari zake kwenda Roma mapema leo na kuirusha kwenda Geneva, ambako alikuwa akitaka hifadhi ya mkimbizi wa kisiasa, maofisa walisema.

JICHO LA TATU...