Tuesday, February 18, 2014

CHEKA KIMYA-KIMYA...

Jamaa mmoja kaamua kwenda kumtupa paka wake baada ya kuchoshwa na tabia za paka huyo kudokoa mboga jikoni kila mara. Siku moja alfajiri jamaa akambeba paka huyo na kwenda kumtupa mbali.
Aliporejea nyumbani akashangaa kumkuta paka yule amejilaza mlangoni. Jamaa hakukata tamaa, siku iliyofuata akamchukua paka wake na kwenda naye umbali wa kilometa takribani 50 huku akipita njia za vichochoroni zenye kona nyingi mno. Baada ya kumtelekeza kwenye kichaka, jamaa akaanza safari ya kurejea nyumbani. Baada ya kama hatua 20 hivi, jamaa akampigia simu mkewe nyumbani na mambo yalikuwa hivi. Jamaa: Mama nanihii, vipi huyo paka yupo hapo nyumbani? Mke: Ndio, huyu hapa kajilaza mlangoni! Kwani vipi? Jamaa: Duh, hebu mpe simu niongee naye alielekeze maana nimepotea njia huku!! Kasheshe...

No comments: