CHEKA KIMYA-KIMYA...

Jamaa mmoja mlevi kafika nyumbani kwake akiwa kalewa chakari. Akabisha hodi na mambo yalikuwa hivi. Jamaa: "Mke wangu nifungulie mlango." Mke: "Nasema sifungui maana nimechoshwa na tabia yako ya ulevi!"
Jamaa: "Kama hufungui mlango basi mie najitupa kwenye hili shimo hapa nje nife kabisa!" Mke: "Kufa maana huna faida yoyote katika hii dunia." Jamaa akatupa jiwe kubwa kwenye lile shimo. Mke akajifunga khanga haraka na kutoka nje kwa kasi. Jamaa bila kufanya ajizi akaingia ndani spidi na kufunga mlango. Mke: "Nifungulie mlango la sivyo nitapige kelele majirani waje." Jamaa: "We piga kelele na wakishakuja uwaeleze unatoka wapi na khanga moja usiku huu!" Duh...

No comments: