Monday, April 30, 2012

KIJEMBE CHA LEO...

Hapa ilikuwa kwenye Barabara ya Mandela maeneo ya Tabata Matumbi leo asubuhi. (Picha na ziro99blog).

MCHEZO HUU HATARI BADO UNAENDELEA...

Vijana hawa pichani wakijimiminia mabaki ya mafuta kutoka kwenye moja ya malori yaliyokuwa kwenye foleni katika Barabara ya Mandela maeneo ya Buguruni leo asubuhi. Vitendo hivi licha ya kupigwa marufuku kwa sababu za kiusalama, vimeibuka tena kwa kasi baada ya vijana hawa kuona hakuna hatua zozote za kuwazuia zikichukuliwa. (Picha zote na ziro99blog).

BORA PUNDA AFE MZIGO UFIKE...

Mwendesha baiskeli aina ya guta akiwa amepakia magunia ya mihogo kuelekea Buguruni kwenye Barabara ya Mandela maeneo ya Bakhressa leo asubuhi. (Picha na ziro99blog).

JICHO LA TATU...

KUTANA NA WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

...Haya sasa, mzazi huyu kaamua kumvalisha ngoma mwanae na kuanza kuipiga. Sijui ana nia gani na mtoto huyu?
Kakosa vya kupika mpaka amfanye mtoto kitoweo? Je, ungepata nafasi ya kumweleza mzazi huyu juu ya kitendo alichofanya ungekuwa na yapi ya kumwambia? Bofya comments hapa chini kisha uandike ujumbe wako!

CHEKA TARATIBU...

Nikiwa kwenye msiba nyumbani kwa binti mmoja jirani yetu maeneo ya Magomeni ambaye amefiwa na mwanae, mara ikasikika sauti ya mwanamke mmoja akilia kwa sauti na kutamka maneno mbalimbali. Nikashawishika kusogea kwa dirishani nione ni nani aliyekuwa akitamka maneno mazito hivyo. Aah, kumbe ni huyo binti mfiwa ambaye mtoto aliyefariki alisemekana kuzaa na Mchina. Katika kusema hili na lile ndipo binti huyo akatamka kwa uchungu, "Mie nilijua tu, siku zote nasema vitu vya Kichina havidumu...mmeona sasa?" Watu wote msibani midomo mwaaaa...

ZIRO PLUS...

ZIRO PLUS...

ASIMAMISHA SHUGHULI ZOTE MTAANI BAADA YA KUTISHIA KULIPUA JENGO...


Jamaa huyo mara baada ya kutiwa nguvuni huku akiwa tumbo wazi.
Huyu ndiye mtu anayedaiwa kusimamisha shughuli zote katikati ya Jiji la London jana baada ya kutishia kulipua jengo na tuhuma za kuwashikilia mateka wanaume wanne huku akidai kubeba mabomu.
Mtu huyo alikamatwa majira ya saa 9 alasiri na kukokotwa bila shati hadi kwenye gari la polisi kabla ya polisi kuanza kuchunguza kwa umakini jengo hilo lililoko Barabara ya Tottenham Court.
Maelfu ya watu waliondolewa maeneo yanalolizunguka jengo hilo majira ya mchana baada ya ripoti kuzagaa kuwa mwanaume mmoja amebeba mitungi ya gesi na kiberiti cha kuwashia, akitishia kulipua ofisi za kampuni inayotoa mafunzo ya udereva na kisha kutishia kujilipua mwenyewe.
Inaaminika alikuwa na chuki na kampuni hiyo baada ya kufeli mara mbili mtihani wa udereva.
Kamanda wa Jeshi la Polisi, Mak Chishty alisema mtuhumiwa ni mwananchi wa kawaida tu.
Alithibitisha kuwa hakuna mateka aliyebaki kwenye jengo baada ya mtuhumiwa kuondolewa kwenye jengo kufuatia wapatanishi kupelekwa eneo la tukio.
Ofisa huyo alisema mwanzoni polisi waliamini mtuhumiwa alikuwa na mabomu ama vifaa vya milipuko lakini uchunguzi eneo la tukio umebaini hakuwa na chochote kati ya hivyo.
Mtuhumiwa bado anashikiliwa na polisi.
Mwanaume huyo alikuwa akiwashikilia mateka wanne baada ya kuingia kwenye ofisi za kampuni hiyo ya mafunzo.
Alidai amefeli mara mbili mitihani ya udereva na kwamba anataka kurejeshewa fedha zake, huku akipiga kelele: "Sina sababu za kuendelea kuishi."
Maofisa, wakiwamo walinzi, wataalamu wa mabomu na wapatanishi wa polisi walikimbilia eneo la tukio muda mfupi baada ya mchana.
Waliamuru kuondolewa zaidi ya wafanyakazi 1,000 wa jengo hilo na watu waliokuwa wakifanya manunuzi madukani pamoja na watalii katika eneo hilo.
Abby Baafi mwenye miaka 27, Mkuu wa Mafunzo na Uendeshaji wa Advantage, kampuni inayotoa kozi za udereva, alisema mwanaume huyo alizilenga ofisi zake na alikuwa akiwashikilia mateka wanaume wanne. Alisema mwanaume huyo alifeli mara mbili kozi ya udereva.
Mateka hao inaaminika kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa kampuni hiyo pamoja na maofisa mauzo watatu.
Abby aliliambia gazeti la Huffington Post: "Tulikuwa ofisini na mtu mmoja akaingia ndani. Nilimtambua kwa kuwa aliwahi kuwa mmoja wa wateja wetu.
"Alikuja namtungi mkubwa wa gesi akiwa ameubana kwapani na kutishia kulipua ofisi.
"Alisema hahofii maisha yake, hahofii chochote, anachotaka yeye ni kulipua ofisi.
"Ni dhahiri alikuwa akinitafuta mimi lakini sikuthubutu kujitambulisha jina langu na akaniruhusu kuondoka sababu nilikuwa na mimba ya miezi mitatu."
Aliongeza, mwanaume huyo akachukua simu zote za mikononi za mateka wake hao.
Mfanyakazi wa mgahawa wa KFC, Arti Pal mwenye miaka 23 alisema: "Sakata zima lilianza majira ya saa 6:30. Polisi walifika na kuwaagiza wateja wasiendelee kuagiza chakula na kwamba wanatakiwa kutoka nje.
"Dakika 15 baadaye walikuja na kutuamuru kutoka nje mapema iwezekanavyo. Vitu vyetu vyote bado viko ndani."
Haikufahamika mara moja mtuhumiwa alifikaje eneo la tukio, ikiwa ni kwa gari ama kwa miguu.
Polisi hawakueleza kiundani zaidi kama kuna mashuhuda wowote waliomwona mtuhumiwa akiingia ama kuona gari lolote linalohusiana na mtuhumiwa.
Edwards, Meneja wa Shirika la Outside alisema: "Kuna mtu alikuwa akitupa vitu dirishani - zilionekana kompyuta na samani mbalimbali kisha makaratasi.
Polisi walifika ofisi ya mapokezi na kutuambia tunatakiwa kutoka kwenye jengo mara moja.
Richard Webb mwenye miaka 26 anayefanya kazi kwenye eneo hilo anasema: "Niliona polisi wakiingia kwenye jengo hilo na mara kutoka nje na watu wanne huku mikono yao ikiwa kichwani.
"Watu walikuwa wakikimbia huku na huko mtaani na polisi walikuwa wakiwashusha watu kutoka kwenye magari yao ambayo hadi sasa yametelekezwa kwenye mtaa."

Sunday, April 29, 2012

JICHO LA TATU...

KUTANA NA WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

Hii tena kali! Mzazi huyu akikokota baiskeli ya mtoto kwenye supamaketi huku akiwa amerundika bidhaa alizonunua juu ya mwanae kwa raha zake...
Mhh...No Comments! Labda msomaji wangu unaweza kusema chochote kuhusu picha hii. Bofya comments hapo chini uniambie mawazo yako kuhusu mzazi huyu na mwanaye pichani.

CHEKA TARATIBU...

Farida akiwa amejilaza kwenye kochi huku wakiwa mezongwa na mawazo tele kichwani kuhusu mambo mbalimbali yaliyokuwa yakimzonga kichwani hatimaye kaamua kuwashirikisha ndugu zake.
Akawaita mama yake na kaka yake na kusema, "Hakuna anayenipenda…dunia nzima watu wananichukia!"
Baada ya sekunde kadhaa, kaka yake aliyekuwa bize na intaneti muda wote akageuka na kujibu, "Sio kweli dada yangu Farida. Kuna baadhi ya watu hata hawakufahamu!"

MWANAMIELEKA WA WCW AMKWEPA 'ISRAELI'...

Hatimaye mwanamieleka Buff Bagwell sasa anapumua na kula mwenyewe baada ya kukaribia kifo kufuatia ajali mbaya ya gari Jumatatu iliyopita, kwa mujibu wa mke wa mwanamieleka huyo.
Judy Bagwell amesema nyota huyo wa zamani wa WCW amekuwa akipumua kwa msaada wa mashine huku madkatari katika chumba cha wagonjwa mahututi wakihaha kumtibu majeraha yake makubwa usoni na katika uti wa mgongo.
Lakini sasa, Judy anasema, "Mashine ya kupumulia imeondolewa Jumatano, anaongea...ameanza kula vyakula vigumu."
"Madaktari wameshtushwa sana kwa jinsi alivyoweza kuwasiliana mapema hivi...ni mpambanaji."
Kama ilivyoripotiwa awali, Buff alipinduka na gari lake aina ya Jeep baada ya moja ya magurudumu yake kupata hitilafu.
Judy amesema Buff tayari amewasiliana na rafiki zake wa zamani wa WCW akiwamo Sting, Scott na Rick Steiner na 'Diamond' Dallas Page.
"Imemfariji mno kuwasiliana na marafiki zake...hakika imemfanya ahisi upendo wa dhati."

ZIRO PLUS...

ZIRO PLUS...

NDEGE YANUSURIKA KUSOMBWA NA UPEPO MKALI WAKATI IKITUA...


Picha za kushangaza zimenasa tukio la kutisha na kusisimua pale marubani na abiria wa ndege wakikaribia kifo kufuatia ndege yao kushambuliwa na upepo mkali wakati ikijaribu kutua kaskazini mwa Hispania wiki hii.
Picha hizo za ndege iliyokuwa ikijaribu kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Loiu mjini Bilbao zimeonesha ndege hiyo ikisukumwa kando na kutikiswa kiasi cha kupoteza mwelekeo huku marubani wakipambana kuishusha chini salama kwenye barabara za kuruka na kutua ndege uwanjani hapo.
Wakati rubani mmoja akifanikiwa kuilengesha ndege kwenye mstari wa kutua, mwingine analazimishwa na upepo mkali kupaa na kuondoa uwezekanao wa ndege kutua kwenye njia yake.
Mamlaka ya Taifa ya Hali ya Hewa iliripoti kuwa upepo huo ulifikia kiwango cha maili 40 kwa saa uwanjani hapo, wakati upepo mkali ulifikia kiwango cha maili 80 kwa saa maeneo mengine katika Mkoa wa Basque.
Usafiri wa anga umeathiriwa, wakati ndege nne zimelazimika kubadili safari na kutua viwanja tofauti, kwa mujibu wa AENA, mamlaka ya uwanja wa ndege.

KUTOA NI MOYO, SI UTAJIRI...

  MCHANGIE KIJANA MWENZAKO 
          SAJUKI, ANAUMWA!!            
Kufuatia hali ilivyo (alivyoonekana zamani na alivyo sasa hapo juu), ziro99blog tunatoa wito kwa wasomaji wetu na wadau mbalimbali tumchangie fedha msanii maarufu wa filamu nchini, Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki kwa ajili ya matibabu yake kupitia simu ya mkononi kwa kutuma kwenye Tigopesa namba 0713 666 113 au kwenye akaunti namba 050000003047 katika Benki ya Akiba Commercial yenye jina la Wastara Juma Issa.
 UJUMBE: Si kwamba tunacho kikubwa mno lakini kidogo tulichojaliwa tunagawana!   MUNGU AWABARIKI!!

Saturday, April 28, 2012

SOUTHAMPTON WAREJEA LIGI KUU ENGLAND...

Ushindi wa mabao 4-0 ilioupata nyumbani kwa Coventry City umeirejesha moja kwa moja timu ya Southampton kwenye Ligi Kuu ya England.
Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Nigel Adkins kilifahamu fika ushindi dhidi ya timu hiyo iliyoshuka daraja utaihakikishia Southampton nafasi ya pili nyuma ya vinara, Reading na kurejea Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu iliposhuka daraja mwaka 2005, na dalili hizo zilianza kuonekana ndani ya dakika 20.
Mabao yaliyoibeba Southampton yaliwekwa kimiani na Billy Sharp dakika ya 16, Jose Fonte dakika ya 19, Jos Hooveid dakika ya 53 na Lallana katika dakika ya 63 na hivyo kuamsha shamrashamra za kuwashangilia 'Wakatatifu' hao kurejea Ligi Kuu.

KIJEMBE CHA LEO...



JICHO LA TATU...

KUTANA NA WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

Huyu mzee vipi? Ndio ubebaji gani huu wa mtoto jamani?
Kama haitoshi, huyu mama naye kama haoni mchezo wa hatari anaofanya mwanae!

CHEKA TARATIBU...

Ama kweli, ushamba mzigo! Mmasai mmoja kaamka asubuhi na kwenda moja kwa moja zahanati ya jirani kupima akitaka kujua anasumbuliwa na nini. Alipofika kwa daktari, akawekewa chombo cha kupimia joto la mwili mdomoni kujua kama ana homa au la. Baada ya dakika kama ishirini hivi, daktari akamfuata kutaka kuchukua kile chombo ili aangalie joto limefikia kiasi gani. Kwa mshangao Mmasai akafungua mdomo lakini hakukua na kitu zaidi ya meno na ulimi wake tu. Ndipo daktari akauliza, "Kiko wapi kile chombo nilichokuwekea mdomoni?" Mmasai kwa kujiamini akajibu, "Imemesa yote! Mimi nasani ile kidonge mupya." Dah...

MATEKA AZIKWA HAI NA MAJESHI YA SERIKALI SYRIA...

  
Ikionesha mwanaume akililia uhai wake huku akizikwa hai na mtutu wa bunduki mbele yake, hii inaweza kuwa video ya kushitusha zaidi kutoka Syria.
Japo ni vigumu kubainisha picha hizi zilizopigwa kama ni halisia au la, lakini ukweli bado unabaki kwamba zote zina nguvu na zinaumiza mno.
Mwanaume anaonekana akiwa amezikwa hadi shingoni huku akiwa amezingirwa na askari wanaotii majeshi yanayoongozwa na Rais Bashar al-Assad.
Wakati Kamanda wa Kikosi akikaribia, vichwa vya habari kwenye video hiyo vimesema: "Ndio mheshimiwa, tumemuweka pale kama ulivyoagiza."
Ofisa akauliza: "Ana kitu gani? Mmemkuta na chochote huyu mnyama asiye na thamani?"
Mwanaume huyo, anayesadikiwa kutokea Al-Qussair, mji wa waasi magharibi mwa Syria jirani na Homs, anadaiwa kubeba kamera na kurekodi matukio yote yanayofanywa na vikosi vya Rais Assad na kusambaza picha hizo kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.
Aliitwa 'mnyama' mara kadhaa na 'mbwa' kabla ya kutekelezwa amri ya kumzika. Maaskari waliomzingira walimtupia mchanga kichwani wakati mwanaume huyo akilia "Natoa ushuhuda kwamba hakuna mungu ila Allah."
Wakati kichwa chake kikipotelea ardhini, askari walimkashifu wakisema: "Sema hakuna Mungu ila Bashar we mnyama."
Hakuna askari yeyote aliteonekana sura katika video hiyo na haikujulikana ilipatikanaye ama ilitumwa vipi kwenye mtandao wa YouTube.
Ni kipande cha video kinachochanganya kikijaribu kuonesha unyama unaoendelea kwenye mapigano nchini Syria tangu kuanza kwa uasi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mapema mwezi huu, kipande cha video kilipatikana hadhari kikionesha vikosi vya Syria vikimuadhibu mmoja wa waasi wanaoipinga serikali katika vitongoji vya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
Ilionesha mwanaume akiwa amelala kifudifudi kwenye sakafu ya vumbi, mikono nyuma huku askari watatu waliovaa kivita wakiwa wamesimama shingoni na mgongoni wakimpiga.
Wakati huohuo, habari zimedai kuwa mlipuko mkubwa umeua watu 70 kwenye mji wa Hama. Nyumba kadhaa mjini Masha, katika wilaya ya Tayyar kusini mwa Hama zimeharibiwa na mlipuko huo mkubwa.
Hatahivyo, Shirika la Habari la Syria limesema mlipuko huo umesababishwa na vikosi vya waasi kushindwa kudhibiti makombora yao na kusababisha mlipuko ulioua watu wapatao 16.

ZIRO PLUS...

ZIRO PLUS...

Friday, April 27, 2012

MUONEKANO WA BARABARA YA BAGAMOYO WAKATI UJENZI UKIENDELEA...

Maeneo ya Tegeta Darajani hali ilikuwa  hivi jioni ya leo. (Picha zote na ziro99blog)

KIJEMBE CHA LEO...

Hii ilikuwa kwenye Barabara ya Mandela maeneo ya Ubungo Tanesco mkabala na kituo cha Songas.

HALI YA FOLENI JIJINI DAR ES SALAAM LEO...

Hapa ilikuwa kwenye Barabara ya Bagamoyo maeneo ya njiapanda ya kwenda Africana jioni ya leo.

KINYAGO ANACHOVAA MICHAEL JACKSON CHAINGIZWA MNADANI...


Kinyago cheusi kinachofunika uso ambacho Michael Jackson anadaiwa kuvaa siku moja kabla ya kufikwa na mauti mwaka 2009, kimevunja rekodi ya mauzo katika mnada ambapo bei imevuka Dola za Marekani 20,000.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa madalali wa kampuni ya udalali ya Nate D. Sanders, Michael Jackson alivaa kinyago hicho wakati wa mazoezi kujiandaa kwa ziara yake ya tamasha la 'This Is It' Juni 24, mwaka 2009, yakiwa ni mazoezi ya mwisho kabisa ya mwimbaji huyo.
Madalali hao walidai kinyago hicho kimetengenezwa kwa nyuzi ya hariri ikiwa ni ubunifu wa Mfalme huyo wa Pop duniani, likiwa na matundu kwa ajili ya kuonesha vipodozi anavyopaka Michael anapokuwa jukwaani katika maonesho mbalimbali pamoja na nywele zake nyeusi.
Mmoja wa mabaunsa wa zamani wa Michael Jackson ndiye alikuwa akilimiliki kinyago hicho. Mfalme huyo wa Pop alikuwa akivaa kinyago hicho wakati wa matembezi yake kama moja ya njia za kuepuka usumbufu njiani.
Mnada huo unafungwa rasmi Aprili 30 na zabuni zimeshafikia bei ya Dola za Marekani 21,190. Madalali wanakadiria kinyago hicho kitauzwa kati ya Dola za Marekani 50,000 na 150,000.

JE, WAJUA?

Zifuatazo eti ndio tafsiri za majina ya miji mbalimbali mkoani Kilimanjaro kulingana na inayodaiwa kuwa hulka ya wenyeji wa mkoa huo wa kabila la Wachagga wanavyoaminika kupenda sana pesa ama 'ankara' au 'umate-mate'!
Sala Kuu: MOSHI: Mungu Onesha Sehemu Hela Iko

Viitikio:
1.                   Hata Ikipungua Mungu Ongeza! (HIMO)
2.                   Mungu Angalia RAia NGawira Utuhakikishie!   (MARANGU)
3.                   Mungu Ahidi Mapesa Bila Ajira! (MAMBA)
4.                   Mungu Wekeza Ishara Kwenye Akaunti! (MWIKA)
5.                   Kristu Imarisha Leo Elimu na Mapesa Akauntini! (KILEMA)
6.                   Kristu Imarisha Riziki Ujaze Akaunti! (KIRUA)
7.                   Usitunyime Riziki Uchumi! (URU)
8.                   Kila Ikipungua Baba Ondoa Siasa Hela Ongeza! (KIBOSHO) (By the way, Wakibosho si wanasiasa!!)
9.                   Mungu Atupe Chanzo Halisi na Ambacho Mapesa ni Endelevu!( MACHAME)
NA
10.            Kwetu Ikikosekana SHIlingi MUngu Nakuapia Dunia Utaichukia! (KISHIMUNDU)

KUTANA A WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

Kha! Hii kali tena...Mtoto anapiga fegi kwa raha zake tena bila kuwahofia wazazi wake.
Na huyu naye sigara imemnogea hadi kapandisha mguu juu. Si bure inaonesha anaifahamu vizuri...

JICHO LA TATU...

CHEKA TARATIBU...

Panya watatu wameketi chini ya uvungu wa kabati wakitambiana kuhusu jinsi walivyo jasiri kushinda wengine.
Panya wa kwanza akaanza, "Mimi ni jasiri sana, siku moja nimekula keki yote iliyokuwa na sumu ya panya!"
Panya wa pili akasema, "Mimi ni jasiri zaidi, siku moja nilinaswa na mtego wa panya lakini nikafanikiwa kuuvunja vipande vipande!"
Panya wa tatu akamalizia, "Baadaye washikaji wangu, ngoja nikamshikishe adabu paka sebuleni!" Duh...

ZIRO PLUS...

ZIRO PLUS...

MAMIA YA MBWA WALIOKUWA WAKIPELEKWA MAHOTELINI KWA KITOWEO WAOKOLEWA...

Mbwa waliokuwa wakipelekwa kuchinjwa na kusambazwa kwenye migahawa mbalimbali ya China wameokolewa baada ya lori walimobebwa kuzuiwa njiani na wanaharakati wa haki za wanyama.
Lori hilo lililokuwa limebeba mbwa wapatao 505 waliofungiwa kwenye vizimba 156, lilisimamishwa kwenye barabara kuu katika Jimbo la Yunnan likitokea Fumin kwenda Kunming kufuatia madereva wengine kushtukia mzigo huo haramu.
Idadi ya picha na maoni mbalimbali yalitumwa kwenye mtandao wa kijamii wa China unaofanana na Twitter, Weibo, wakishawishi polisi kulikamata lori hilo katika kizuizi kinachofuata.
Baada ya kukamatwa, lori hilo lilipelekwa kituo cha polisi kinachofuata ambapo wapenda wanyama waliovujisha taarifa hizo walianza kuwasili kituo hapo.
Kwa majonzi, kufuatia hali mbaya wengi wa mbwa hao walikuwa tayari wamekufa wakati walipogundulika.
Mmoja wa wanaharakati hao alisema: "Walirundikwa pamoja. Kizimba kimoja waliwekwa mbwa kati ya saba na nane. Tuliumia sana mioyo kuona tukio hili."
Wafanyakazi wa kujitolea walivunja vizimba hivyo ndani ya lori na walitumia usiku mzima kuwalisha, kuwanywesha na kuwatibu wanyama hao.
Wakielezea tukio hilo la kutisha, maofisa kutoka Idara ya Ukaguzi wa Wanyama ya eneo hilo inayochunguza tukio walifafanua kuwa usafirishaji mbwa ni ruksa.
Mtu anayewamiliki anayo leseni ya kufanya hivyo na polisi wameshindwa kufanyia kazi madai kuwa walikuwa wakipelekwa kwenye migahawa mbalimbali kwa ajili ya kuuzwa nyama.
Mwanaharakati mwingine ameongeza: "Hatuwezi kuwazuia kula mbwa, hasa kwa kuzingatia kuwa hatuna sheria za kulinda wanyama. Tunaimani Serikali itawadhibiti wanaojihusisha na mbwa kufanya biashara hiyo."
Hatahivyo, kituo binafsi cha kuokoa mbwa kimechukua hatua ya kuwakusanya mbwa wote kutoka kwa wamiliki wake kwa ghara ya Pauni za Uingereza 5,900. Wanyama hao watakaa chini ya uangalizi maalumu hadi watakapopata wamiliki wapya.
Mpaka sasa, nchi 11 duniani bado zinakula mbwa. Nchi hizo ni China, Indonesia, Korea, Mexico, Philippines, Polynesia, Taiwan, Vietnam, Arctic na Antatctic na miji miwili nchini Uswisi.

Thursday, April 26, 2012

BAYERN MUNICH YAIKATA MAINI YA WAHISPANIA MWAKA HUU...

        FAINALI MABINGWA ULAYA:        
     NI CHELSEA vs BAYERN MUNICH         
Bayern Munich ya Ujerumani usiku wa kuamkia leo imefanikiwa kufanya kile kilichotarajiwa na wengi pale ilipoweza kuibana Real Madrid ya Hispania na kuing'oa mashindanoni kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 3-1 ndani ya dimba la Santiago Bernabeum mjini Madrid. Haikuwa kazi rahisi kwani hadi dakika 120, Real Madrid walikuwa wakiongoza 2-1 na hivyo kufanya matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2 kufuatia ushindi wa Bayern wa 2-1 mjini Munich wiki iliyopita. Licha ya kufunga mabao yote mawili, Cristiano Ronaldo na mwenzake Ricardo Kaka penalti zao kwa upande wa Madrid zilipznguliwa na kipa wa Bayern Manuel Neur. Sasa Bayern itavaana na Chelsea ya England ambayo juzi iliwavua ubingwa Wahispania wengine, Barcelona kwa kulazimisha sare ya 2-2 kwenye Uwanja wa Camp Nou, mjini Barcelona na kufanya matokeo ya jumla kuwa mabao 3-2, baada ya kuwa wameshinda 1-0 kwenye mechi yao ya kwanza Uwanja wao wa Stamford Bridge, mjini London wiki iliyopita. Mechi ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya timu hizo itapigwa kwenye dimba la Allianz-Arena, mjini Munich Mei 19 mwaka huu.

KUTANA NA WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

Hakika mwana wa nyoka ni nyoka! Fikiria mtoto huyu akifikisha miaka kumi kwa spidi hii atakuwaje...Hapaa anaramba pombe iliyoachwa na mzazi wake!
Tangazo mlangoni linasomeka "Ili kuingia ndani lazima uwe na umri kuanzia miaka 21!" Sasa imekuwaje mzazi wa mtoto huyu kumruhusu aingie humo?

KIJEMBE CHA LEO...

JICHO LA TATU...

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja akiwa hoi bin taabani kitandani akisubiria 'Israeli' achukue roho yake akasema, "Mke wangu, siwezi kufa kabla sijakwambia ukweli wangu. Siku zote nilizokuwa nikikwambia nimechelewa kazini, nilikuwa nakudanganya badala yake nilikuwa nikila raha na wanawake wengine. Na si mmoja bali utitiri wa wanawake." Mkewe akamtazama kwa huruma na kisha kujibu, "Kwani unadhani sababu nimekulisha sumu?" Duh…

MSTAAFU AUA PANYA MWENYE UREFU WA FUTI NNE...



Panya mkubwa anayefikia futi 4 kuanzia puani hadi mkiani amenaswa na kuuawa na mstaafu kwa kutumia mbao shambani kwake.
Brian Watson mwenye miaka 67 kutoka Waskerley, Consett mjini County Durham, alitambua uwezo wa mnyama huyo mkubwa pale rafiki wa kiume wa mjukuu wake alipopiga kelele wakati akikata majani.
Watson alisema: "Nimlisikia akipiga mayowe akisema kuna panya mkubwa. Nilitoka nikikimbilia kwenye kichochoro ambako nilifanikiwa kupata ubao na kwenda nao."
"Hakuwa na kasi sana. Nilimudu kumuua palepale."
"Sijawahi kuona panya mkubwa kiasi kile hapo kabla."
Sababu moja ya kuwa taratibu kiasi ni kwamba lazima alikuwa na mimba.
"Nadhani alikuwa akikaribia kuzaa," aliongeza Watson.
Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanaamini panya huyo ni aina ya panya wanaopatikana Amerika Kusini ambapo pia wanatambulika kama panya wa kwenye mito.
Baada ya kumuua, babu huyo alijaribu kumchota na koleo lakini alikuwa mzito mno na koleo hilo kuvunjika.
Tukio hilo lilifahamika hadharani baada ya rafiki wa Watson, Bri Mitchell kuituma katika mtandao wa Twitter picha ya panya huyo baada ya kukamatwa.
Watson alisema: "Tulimtelekeza pale kwa siku kadhaa hatimaye tukakubaliana tummalizie kwa kumchoma moto na kumaliza tatizo hilo."
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, msemaji wa Polisi wa Dulham alisema kwa sasa hawachunguzi wanyama.

Wednesday, April 25, 2012

NYOTA WA MIELEKA WCW APATA AJALI MBAYA, YU MAHUTUTI HOSPITALINI...


Nyota wa zamani wa mieleka ya WCW, Buff Bagwell yuko kwenye chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya Atlanta baada ya gari lake aina ya Jeep kupinduka, ikisemekana kuvunjika mishipa kadhaa shingoni mwake.
Kwa mujibu wa hospitali hiyo, ajali hiyo ilitokea Jumatatu usiku ikimwacha nyota huyo mwenye miaka 42 akiwa amevunjika mifupa shingoni, usoni pamoja na kuvunjika taya lake.
Bagwell alisafirishwa hadi hospitali ya jirani ambako alilazwa chumba cha wagonjwa mahututi.
Taarifa zaidi zitafuatia...

KIJEMBE CHA LEO...

Hapa lilinaswa kwenye maeneo ya Ilala Boma, Dar es Salaam jana. Kama unacho kijembe na unataka kuwashirikisha wengine tuma picha yenye kijembe kwa baruapepe ziro99blog@gmail.com

JICHO LA TATU...

Kujibu swali alilouliza mheshimiwa hapo juu, bofya sehemu ya comments hapa chini kisha acha ujumbe wako.

KUTANA NA WAZAZI WABAYA ZAIDI DUNIANI...

Usalama kwanza! Katoto haka kakiwa kamefungwa mkanda kwa sababu za usalama. Kamefungwa sahihi au la, hilo anajua mzazi wake.
Haachwi mtu nyumbani! Anaonekana mzazi huyu akikafungia katoto kake kwenye buti la gari tayari kuanza safari...