Thursday, April 26, 2012

MSTAAFU AUA PANYA MWENYE UREFU WA FUTI NNE...



Panya mkubwa anayefikia futi 4 kuanzia puani hadi mkiani amenaswa na kuuawa na mstaafu kwa kutumia mbao shambani kwake.
Brian Watson mwenye miaka 67 kutoka Waskerley, Consett mjini County Durham, alitambua uwezo wa mnyama huyo mkubwa pale rafiki wa kiume wa mjukuu wake alipopiga kelele wakati akikata majani.
Watson alisema: "Nimlisikia akipiga mayowe akisema kuna panya mkubwa. Nilitoka nikikimbilia kwenye kichochoro ambako nilifanikiwa kupata ubao na kwenda nao."
"Hakuwa na kasi sana. Nilimudu kumuua palepale."
"Sijawahi kuona panya mkubwa kiasi kile hapo kabla."
Sababu moja ya kuwa taratibu kiasi ni kwamba lazima alikuwa na mimba.
"Nadhani alikuwa akikaribia kuzaa," aliongeza Watson.
Baadhi ya wachunguzi wa mambo wanaamini panya huyo ni aina ya panya wanaopatikana Amerika Kusini ambapo pia wanatambulika kama panya wa kwenye mito.
Baada ya kumuua, babu huyo alijaribu kumchota na koleo lakini alikuwa mzito mno na koleo hilo kuvunjika.
Tukio hilo lilifahamika hadharani baada ya rafiki wa Watson, Bri Mitchell kuituma katika mtandao wa Twitter picha ya panya huyo baada ya kukamatwa.
Watson alisema: "Tulimtelekeza pale kwa siku kadhaa hatimaye tukakubaliana tummalizie kwa kumchoma moto na kumaliza tatizo hilo."
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, msemaji wa Polisi wa Dulham alisema kwa sasa hawachunguzi wanyama.

No comments: