Sunday, April 29, 2012

MWANAMIELEKA WA WCW AMKWEPA 'ISRAELI'...

Hatimaye mwanamieleka Buff Bagwell sasa anapumua na kula mwenyewe baada ya kukaribia kifo kufuatia ajali mbaya ya gari Jumatatu iliyopita, kwa mujibu wa mke wa mwanamieleka huyo.
Judy Bagwell amesema nyota huyo wa zamani wa WCW amekuwa akipumua kwa msaada wa mashine huku madkatari katika chumba cha wagonjwa mahututi wakihaha kumtibu majeraha yake makubwa usoni na katika uti wa mgongo.
Lakini sasa, Judy anasema, "Mashine ya kupumulia imeondolewa Jumatano, anaongea...ameanza kula vyakula vigumu."
"Madaktari wameshtushwa sana kwa jinsi alivyoweza kuwasiliana mapema hivi...ni mpambanaji."
Kama ilivyoripotiwa awali, Buff alipinduka na gari lake aina ya Jeep baada ya moja ya magurudumu yake kupata hitilafu.
Judy amesema Buff tayari amewasiliana na rafiki zake wa zamani wa WCW akiwamo Sting, Scott na Rick Steiner na 'Diamond' Dallas Page.
"Imemfariji mno kuwasiliana na marafiki zake...hakika imemfanya ahisi upendo wa dhati."

No comments: