Saturday, April 28, 2012

MATEKA AZIKWA HAI NA MAJESHI YA SERIKALI SYRIA...

  
Ikionesha mwanaume akililia uhai wake huku akizikwa hai na mtutu wa bunduki mbele yake, hii inaweza kuwa video ya kushitusha zaidi kutoka Syria.
Japo ni vigumu kubainisha picha hizi zilizopigwa kama ni halisia au la, lakini ukweli bado unabaki kwamba zote zina nguvu na zinaumiza mno.
Mwanaume anaonekana akiwa amezikwa hadi shingoni huku akiwa amezingirwa na askari wanaotii majeshi yanayoongozwa na Rais Bashar al-Assad.
Wakati Kamanda wa Kikosi akikaribia, vichwa vya habari kwenye video hiyo vimesema: "Ndio mheshimiwa, tumemuweka pale kama ulivyoagiza."
Ofisa akauliza: "Ana kitu gani? Mmemkuta na chochote huyu mnyama asiye na thamani?"
Mwanaume huyo, anayesadikiwa kutokea Al-Qussair, mji wa waasi magharibi mwa Syria jirani na Homs, anadaiwa kubeba kamera na kurekodi matukio yote yanayofanywa na vikosi vya Rais Assad na kusambaza picha hizo kwenye vituo mbalimbali vya televisheni.
Aliitwa 'mnyama' mara kadhaa na 'mbwa' kabla ya kutekelezwa amri ya kumzika. Maaskari waliomzingira walimtupia mchanga kichwani wakati mwanaume huyo akilia "Natoa ushuhuda kwamba hakuna mungu ila Allah."
Wakati kichwa chake kikipotelea ardhini, askari walimkashifu wakisema: "Sema hakuna Mungu ila Bashar we mnyama."
Hakuna askari yeyote aliteonekana sura katika video hiyo na haikujulikana ilipatikanaye ama ilitumwa vipi kwenye mtandao wa YouTube.
Ni kipande cha video kinachochanganya kikijaribu kuonesha unyama unaoendelea kwenye mapigano nchini Syria tangu kuanza kwa uasi zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
Mapema mwezi huu, kipande cha video kilipatikana hadhari kikionesha vikosi vya Syria vikimuadhibu mmoja wa waasi wanaoipinga serikali katika vitongoji vya mji mkuu wa nchi hiyo, Damascus.
Ilionesha mwanaume akiwa amelala kifudifudi kwenye sakafu ya vumbi, mikono nyuma huku askari watatu waliovaa kivita wakiwa wamesimama shingoni na mgongoni wakimpiga.
Wakati huohuo, habari zimedai kuwa mlipuko mkubwa umeua watu 70 kwenye mji wa Hama. Nyumba kadhaa mjini Masha, katika wilaya ya Tayyar kusini mwa Hama zimeharibiwa na mlipuko huo mkubwa.
Hatahivyo, Shirika la Habari la Syria limesema mlipuko huo umesababishwa na vikosi vya waasi kushindwa kudhibiti makombora yao na kusababisha mlipuko ulioua watu wapatao 16.

No comments: