Sunday, April 29, 2012

NDEGE YANUSURIKA KUSOMBWA NA UPEPO MKALI WAKATI IKITUA...


Picha za kushangaza zimenasa tukio la kutisha na kusisimua pale marubani na abiria wa ndege wakikaribia kifo kufuatia ndege yao kushambuliwa na upepo mkali wakati ikijaribu kutua kaskazini mwa Hispania wiki hii.
Picha hizo za ndege iliyokuwa ikijaribu kutua kwenye Uwanja wa Ndege wa Loiu mjini Bilbao zimeonesha ndege hiyo ikisukumwa kando na kutikiswa kiasi cha kupoteza mwelekeo huku marubani wakipambana kuishusha chini salama kwenye barabara za kuruka na kutua ndege uwanjani hapo.
Wakati rubani mmoja akifanikiwa kuilengesha ndege kwenye mstari wa kutua, mwingine analazimishwa na upepo mkali kupaa na kuondoa uwezekanao wa ndege kutua kwenye njia yake.
Mamlaka ya Taifa ya Hali ya Hewa iliripoti kuwa upepo huo ulifikia kiwango cha maili 40 kwa saa uwanjani hapo, wakati upepo mkali ulifikia kiwango cha maili 80 kwa saa maeneo mengine katika Mkoa wa Basque.
Usafiri wa anga umeathiriwa, wakati ndege nne zimelazimika kubadili safari na kutua viwanja tofauti, kwa mujibu wa AENA, mamlaka ya uwanja wa ndege.

No comments: