Zifuatazo eti ndio tafsiri za majina ya miji mbalimbali mkoani Kilimanjaro kulingana na inayodaiwa kuwa hulka ya wenyeji wa mkoa huo wa kabila la Wachagga wanavyoaminika kupenda sana pesa ama 'ankara' au 'umate-mate'!
Sala Kuu: MOSHI: Mungu Onesha Sehemu Hela Iko
Viitikio:
1. Hata Ikipungua Mungu Ongeza! (HIMO)
2. Mungu Angalia RAia NGawira Utuhakikishie! (MARANGU)
3. Mungu Ahidi Mapesa Bila Ajira! (MAMBA)
4. Mungu Wekeza Ishara Kwenye Akaunti! (MWIKA)
5. Kristu Imarisha Leo Elimu na Mapesa Akauntini! (KILEMA)
6. Kristu Imarisha Riziki Ujaze Akaunti! (KIRUA)
7. Usitunyime Riziki Uchumi! (URU)
8. Kila Ikipungua Baba Ondoa Siasa Hela Ongeza! (KIBOSHO) (By the way, Wakibosho si wanasiasa!!)
9. Mungu Atupe Chanzo Halisi na Ambacho Mapesa ni Endelevu!( MACHAME)
NA
10. Kwetu Ikikosekana SHIlingi MUngu Nakuapia Dunia Utaichukia! (KISHIMUNDU)

No comments:
Post a Comment