Saturday, November 10, 2012

SHEREHE ALIYOANDAA NAOMI CAMPBELL KWA MPENZI WAKE YAINGIA DOA...

PICHA NDOGO KUSHOTO: Naomi akiwa na mpenzi wake, Doronin. PICHA KUBWA: Sehemu ilipofanyika sherehe hiyo. KULIA: Naomi akiingia kwenye eneo la sherehe.
Ilipangwa iwe sherehe ya aina yake kutokea katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, lakini mambo hayakwenda kabisa vile yalivyopangwa.
Naomi Campbell alisherehekea siku ya kuzaliwa mpenzi wake, Vladimir Doronin aliyekuwa akitimiza miaka 50 kwa ubadhirifu na pigo kubwa mjini Jodhpur mapema wiki hii, na licha ya kuwepo onesho la Diana Ross na orodha ya marafiki waliofika kutoka kote duniani, majirani hawakusisimka na makelele yote hayo.
Malalamiko ya kelele kutoka kwa wakazi wa eneo hilo la  ngome ya karne ya 15 yamesababisha kukamatwa kwa meneja wake aliyesimamia maandalizi ya sherehe hiyo.
Meneja huyo mwenye makazi yake mjini Mumbai, P.K. Pareek alikamatwa kwa madai ya 'usumbufu wa kelele' baada ya sherehe hiyo iliyoandaliwa na Naomi na kufanyika kwenye ngome ya karne ya 15.
"Alikamatwa Alhamisi na kuachiwa kwa dhamana leo (jana)," Kamishna wa Polisi Bhupendra Kumar Dak alisema mjini Jodhpur, jiji la pili kwa ukubwa India lililoko kaskazini mwa Jimbo la Rajastham.
Dak alisema mtu huyo alikamatwa baada ya wakazi wa eneo hilo kulalamikia kelele kubwa ya mafataki yaliyokuwa yakipigwa katika sherehe hizo kwenye Ngome ya Behrangarh, Jumatano iliyopita.
Kamishna huyo alisema waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wameruhusiwa kutumia mafataki na muziki mkubwa hadi Saa 4:00 usiku na kwamba polisis walipelekwa kwenye ngome hiyo majira ya usiku wa manane pale wakazi walipolalamika kuzidi kwa kelele.
"Hadi kufikia usiku mkubwa kulikuwa na sauti kubwa ya muziki kutoka kwenye ngome hiyo na milipuko mikubwa ya mafataki iliyotupa usumbufu wa kiakili," alisema Kamlash Prohit, ambaye anaishi jirani na jengo lililochukua sehemu kubwa ya Jodhpur.
Sherehe hiyo ailihudhuriwa na takribani wageni 200, wakiwamo marafiki wasanii nyota kama Duchess of York Sarah Ferguson na Kate Moss.
Diana Ross alitumbuiza shoo ya kipekee, baada ya kuwa amelipwa Dola za Marekani 500,000 kuchombeza umati uliokuwa ukimetameta.
Mwanamitindo huyo mwenye miaka 42, amekuwa na mahusiano na Doronin tangu mwaka 2008 na wawili hao wamekuwa kwa sasa wanaishi pamoja mjini Moscow.
Wamekuwa na kawaida ya kuandaliana sherehe kwa kila mmoja, ambapo Doronin aliwahi kufanya sherehe kubwa kwa ajili ya kusherehekea miaka 40 ya kuzaliwa Naomi huko Riviera nchini Ufaransa.

Friday, November 9, 2012

WAFIKA KUSHUHUDIA WAPENZI WALIONASIANA HOSPITALI YA TEMEKE...

Polisi wakidhibiti umati wa maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam waliofika kwenye Hospitali ya Temeke kushuhudia wapenzi wanaodaiwa kunasiana wakati wakifanya mapenzi maeneo ya Mbagala, jana.
Maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwa wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika Hospitali ya Temeke kushuhudia wapenzi wawili wanaodaiwa kunasiana wakati wakifanya mapenzi ambapo ilidaiwa kwamba waliletwa hospitalini hapo kwa ajili ya zoezi ya kutenganishwa. Hatua hiyo ya wakazi hao kukusanyika hapo ilisababisha huduma katika hospitali hiyo kusitishwa kwa zaidi ya masaa saba jana. Hatahivyo habari ambazo tumezipata jana jioni, Jeshi la Polisi limekanusha vikali uvumi huo na kusema hakuna tukio kama hilo lililotokea. Pia uongozi wa Hospitali ya Temeke nao umekanusha kupokelewa kwa wapenzi hao huku ukisisitiza kwamba taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

DK MWAKYEMBE AVUNJA BODI YA MAMLAKA YA BANDARI (TPA)...

Dk Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amevunja Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na kuteua wajumbe wapya wa Bodi hiyo katika jitihada zake za kurejesha ufanisi katika bandari hiyo.
Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa Dk Mwakyembe amevunja Bodi hiyo  tangu Novemba 6 kwa madaraka aliyopewa na Sheria ya Bandari  ya Mwaka 2004.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wajumbe sita walioondolewa wa Bodi hiyo ni Dustan Mrutu, George Ally, Mtutura Mtutura, Emmanuel Mallya, Mwantumu Malale na Maria Kejo.
Baada ya kuvunja Bodi hiyo, taarifa hiyo ya Wizara ya Uchukuzi, ilieleza kuwa Dk Mwakyembe ameunda Bodi mpya yenye wajumbe wanane ambao walitakiwa kuanza kazi mapema iwezekanavyo.
Walioteuliwa kuingia katika Bodi hiyo ni Dk Jabiri Bakari, John Ulanga, Caroline Temu, Jaffer Machano, Dk  Hildebrand Shayo, Saidi Sauko, Julius Mamiro na Asha Nassoro.
Baada ya kuteua Bodi mpya, Waziri Mwakyembe aliiagiza Menejimenti ya TPA, kuwapa nyaraka zote muhimu wajumbe wapya wa Bodi hiyo mpya, ili wajiandae kabla hawajakutana nao ndani ya siku kumi kuanzia Novemba 6.
Pia aliweka wazi kuwa katika mkutano huo kati ya Bodi mpya na Waziri, Serikali itaingia mkataba wa ufanisi na Bodi hiyo ili wafanikishe bandari ichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Safishasafisha hiyo ya bandari inayofanywa na Mwakyembe ilianzia katika Menejimenti ambapo aliwasimamisha watendaji wa bandari hiyo, akiwamo Mkurugenzi Mkuu, Ephraim Mgawe, naibu wakurugenzi wakuu wawili aliotajwa kwa jina moja moja la Mfuko na Koshuma na Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Cassian Ng’amilo, Meneja wa Kurasini Oil Jet na Mhandisi wa kitengo cha mafuta.
Baada ya kusimamisha kazi vigogo hao, Dk Mwakyembe aliunda kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na Bernard Mbakileki ambayo ilifanya kazi na kukabidhi ripoti ambayo Waziri aliahidi kuifanyia kazi.
Mwanzoni mwa wiki hii, Dk Mwakyembe alisema kama kuna watu wanaopanga kuhujumu bandari ya Dar es Salaam ili kukwamisha mabadiliko yaliyoanza, watambue wanajisafishia njia ya kwenda kutumikia kifungo gerezani.
Dk Mwakyembe alisema mabadiliko TPA, lazima yafanyike ili bandari itoe huduma bora kuliko hata ya Mombasa, Kenya,  ili kuleta tija katika pato la Taifa.
Alisema habari anazosoma katika vyombo vya habari zikielezea mipango inayofanyika kuhujumu bandari ya Dar es Salaam kama ni kweli, basi waliopo katika mtandao huo wafahamu watanyofolewa mmoja baada ya mwingine na kushughulikiwa kikamilifu, kwa sababu Serikali sasa imechoka kuchezewa.

NDEVU ZA SHEKHE FARID WA UAMSHO ZAZUA NONGWA MAHAKAMANI...

Shekhe Farid Hadi Ahmed.
Mawakili wa viongozi wa Jumuiya ya Uamsho wanaoshitakiwa kwa tuhuma tofauti, wamelalamikia kuvunjwa kwa haki za wateja wao wakiwa rumande ikiwamo kunyolewa ndevu kwa wateja hao akiwamo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Shekhe Faridi Hadi Ahmed.
Wengine wanaoshitakiwa katika kesi hiyo mbali na Shekhe Farid ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho, Shekhe Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Suleiman Juma Suleiman, Azan Khalid Hamdan, Khamis Ali Suleiman, Hassan Bakar Suleiman na  Ghalib Ahmada Omar.
Viongozi hao wako rumande wakishitakiwa kwa kutoa lugha za uchochezi na kusababisha ghasia na vitendo vya uvunjifu wa amani uliosababisha uharibifu wa miundombinu ya barabara.
Mbele ya Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, George Kazi jana, mawakili hao Salum Toufik na Abdallah Juma Kaka, wakiwasilisha hoja mbalimbali za uvunjifu wa haki za watuhumiwa walidai kuwa wateja wao wamenyolewa ndevu wakiwa rumande.
Mawakili hao walidai kuwa hatua hiyo ya Magereza ni kinyume na uhuru wa kuabudu, kwani ndevu kwa mashekhe ni sehemu ya ibada.
Akijibu hoja hizo, Mwanasheria wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Ramadhani Nasibu, akinukuu vifungu vya sheria kwenye Katiba ya Zanzibar, alidai kama kuna haki zinazovunjwa na chombo chochote au mtumishi wa Serikali, kuna mahala pengine pa kupeleka malalamiko hayo.
Baada ya mabishano hayo, Kazi aliamuru washitakiwa  wote warudishwe rumande hadi Novemba 20, itakapokuja katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kutajwa tena.
Viongozi hao kwa mara ya kwanza walifikishwa mahakamani hapo wakiwa wamenyolewa ndevu Oktoba 26 chini ya ulinzi mkali wa Polisi.
Kabla ya hapo, Oktoba 22 viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo wakiwa na ndevu nyingi kidevuni mwao, lakini Oktoba 26  walikuwa wamenyolewa na kuwafanya wawe na mwonekano tofauti, jambo ambalo lilizua gumzo kubwa miongoni mwa watu waliofika kusikiliza kesi hiyo.
Naye Flora Mwakasala anaripoti kuwa wakati Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Issa Ponda akiendelea kusota rumande kwa kesi ya uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Sh milioni 59, jana kiongozi mwingine wa taasisi hiyo amepandishwa kizimbani na kusomewa mashitaka hayo.
Mukadam Swalehe (45) alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka manne mbele ya Hakimu Victoria Nongwa.
Hata hivyo, Swalehe alirudishwa rumande, kwa kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) aliwasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa mshitakiwa kama ilivyo kwa Shekhe Ponda.
Awali wakili wa Serikali Tumaini Kweka alidai kuwa Oktoba 12 eneo la Chang’ombe Markasi mshitakiwa aliingia kwa nguvu  katika kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya AgriTanzania  Limited kwa nia ya kujimilikisha kiwanja hicho isivyo halali.
Alidai siku hiyo hiyo, bila uhalali mshitakiwa katika hali iliyokuwa ikisababisha uvunjifu wa amani, alijimilikisha  kwa nguvu ardhi  ya  kampuni hiyo na kuiba vifaa na malighafi, matofali 1,500, nondo, tani 36 za kokoto mali zote zina thamani ya Sh milioni 59.7.
Katika mashitaka ya uchochezi, inadaiwa katika eneo hilo la Chang’ombe Markasi kwa maelezo kuwa yeye ni kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T), alishawishi wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao kutenda makosa hayo.
Wakili Kweka alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na DPP amewasilisha hati ya kuzuia dhamana kwa mshitakiwa.
Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 15 mshitakiwa atakapounganishwa na washitakiwa 50 akiwamo Shekhe Ponda na kusomewa maelezo ya awali.

JERMAINE JACKSON AWASILISHA MAOMBI YA KUBADILI JINA LAKE...

Jermaine Jackson
Jermaine Jackson amefungua madai kisheria kuomba kubadili jina lake la mwisho ... akibadili "Jackson" kuwa "Jacksun" ... imefahamika.
Jermaine amefungua madai hayo ya kubadili jina kwenye Mahakama Kuu ya Los Angeles County juzi akitaka mabadiliko hayo katika mfumo wa majina.
Katika nyaraka, Jermaine amesema anataka kufanya mabadiliko kwa "sababu za kisanii" ... lakini hakutoa ufafanuzi wowote zaidi kuhusu hatua yake hiyo.
Ombi hilo bado halijathibitishwa na Jaji ... lakini shauri hilo limeshawekwa kwenye ratiba za mahakama.
Ili kufanikishwa uamuzi wake huo wa kiwendawazimu, Jermaine katika miezi kadhaa ijayo atatakiwa kutangaza hadharani mabadiliko ya jina lake mara kadhaa kabla ya kukubalika kisheria.
Matangazo kwa umma yanahusisha kuchapishwa kwa jina katika machapisho kashaa ya ndani ya eneo hilo ... kama ilivyofanyika kwa Ron Artest alivyolazimika kufanya pale alipobadili jina lake na kuwa Metta World Peace.

ADONDOKA KWENYE BEMBEA NA KUJIBAMIZA KATIKA UZIO WA CHUMA...

KUSHOTO: Yasmin baada ya ajali hiyo. KULIA: Yasmin kabla ya ajali.
Binti wa miaka 9 alivurumishwa futi 15 angani na kubamizwa kwenye uzio wa chuma baada ya kudondoka kutoka kwenye bembea la viwanja vya maonesho lililokuwa likiendeshwa kwa kasi ya mita 50 kwa saa.
Yasmin Vickery alikimbizwa hospitalini baada ya kufyatuliwa kutoka kwenye bembea hilo mbele ya mama yake alijawa na hofu, Kim, ambaye alihofia kwamba alikuwa amepooza.
Binti huyo alitibiwa shingo ambayo ilidhaniwa kwamba imevunjika kufuatia ajali hiyo iliyotokea Novemba 3 lakini katika hali ya kushangaza alinusurika kuvilia damu mwilini.
Jana Kim, mwanasheria wa kampuni alielezea tukio hilo la kutisha kwamba alihofia binti yake kwamba alikuwa amekufa.
Alisema: "YasMin alikuwa kwenye bembea pamoja na binamu yake mdogo Kya na chuma hilo likainuka juu, na alipojaribu kwenda kulirudisha alitupwa mbali.
"Alirushwa angani sababu lilikuwa likienda kasi mno, kisha unaweza kusikia mshindo huu. Alirushwa juu na kuvuka vizuizi.
"Wakati wote nilikuwa nikirekodi mwenendo wa bembea lile hadi pale liliposimama ghafla bila kujua kilichotokea, tulikuwa tukicheka na kutaniana wakati huo.
"Lakini ndipo nilipomwona binti yangu mdogo akiwa ametupwa upande mwingine. Mtoto wangu wa miaka sita alikuwa akitazama huku akibubujikwa machozi, alitishika mno - alidhani dada yake alikuwa amekufa.
"Nilipokimbilia kule na Yasmin alisema alikuwa amepoteza hisia sehemu za miguuni - nilifikiri kwamba amepooza, angeweza kufa kirahisi lakini alipata pigo kubwa kwa upande wake huo kuliko kichwani wakati huo.
"Athari zilikuwa upande kwa upande, lakini madaktari walisema kama angejibamiza kichwani kwanza basi ingekuwa hadithi nyingine, yaani angeweza kufa.
"Imekuwa ndoto mbaya kwa kila mama lakini najua ana bahati sana na ingeweza kuwa mbaya zaidi kuliko hivi ilivyo.
"Watu wengi huwa hawaponi kwenye ajali ya gari kwa spidi ile, kuchomoka peke yake na kutupwa angani mbali na bembea lile."
Mama huyo aliyeolewa mwenye watoto watatu, kim, mkazi wa Sevenoaks, huko Kent, sasa anapigania ukaguzi wa usalama kufanyika kwenye mabembea - ambao anaamini utafanywa na familia zinazosafiri kutoka Northampton.
Kim aliongeza: "Ninachomaanisha kama bembea lile litapelekwa kokote kwingineko basi inaweza kutokea tena ajali."
Yasmin bado yuko kitandani, na amekuwa akitapika kutokana na madhara aliyopata kwenye figo kufuatia ajali hiyo.
Binti huyo alisema: "Hakika inaumiza mno. Siendi tena shule kwa wiki au zaidi. Siweki uzito wowote kwenye mguu mmoja."
Tukio hilo lilishughulikiwa na polisi na huduma za gari la wagonjwa na sasa unafanyika uchunguzi wa afya na usalama.
Mpelelezi Sajenti Gavin Suttie kutoka Polisi wa Northamptonshire, alisema: "Tumeenda eneo la tukio huko Hollowell, ambapo binti wa miaka 9 amejeruhiwa vibaya kufuatia kudondoka kutoka kwenye bembea.
"Alipelekwa kwenye Hospitali Kuu ya Northampton akiwa na maumivu ya ndani kwa ndani na aliruhusiwa Jumapili. Mkuu wa Afya na Usalama ametaarifiwa na atasaidiwa na polisi katika uchunguzi."
Hakuna mtu yeyote kutoka kwenye viwanja hivyo vya maonesho aliyepatikana kuelezea kwa undani tukio hilo.

JICHO LA TATU...


CHEKA TARATIBU...

Mlevi mmoja kapanda daladala na kuanza kuropoka matusi mazito kwa abiria wengine mle ndani. Baada ya kuvumilia kwa muda mrefu, Kondakta akavunja ukimwa na kumwambia yule Mlevi, "Kwa tabia yako hiyo hautaenda mbinguni!" Yule Mlevi kusikia hivyo akashituka na kujibu, "Ebo! Kumbe basi linakwenda mbinguni, nishushe mie naenda Mbagala!" Duh...

Thursday, November 8, 2012

WAPENZI WANASIANA WAKIFANYA MAPENZI GUEST HOUSE MBAGALA...



Hospitali ya Temeke, Dar es Salaam.
Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa umati mkubwa wa wakazi wa jiji umefurika katika Hospitali ya Temeke kushuhudia wapenzi wawili wanaodaiwa kunasiana wakati wakifanya mapenzi kwenye nyumba moja ya kulala wageni iliyoko maeneo ya Mbagala, Dar es Salaam mapema leo.
Kwa mujibu wa watu waliodai kushuhudia tukio hilo wamesema kwamba baada ya juhudi za kujinasua kushindikana, wawili waliomba msaada na kupelekwa katika Hospitali ya Temeke kwa ajili ya kujaribu kutenganishwa.
Inasemekana kwamba mwanamke aliyehusika katika tukio hilo kuwa ni mke wa mtu, na kwamba mumewe anadaiwa kuhusika katika kuwafanyia tukio hilo linalohusishwa na imani za kishirikina.
Mashuhuda wa tukio hilo wamedai kwamba walishuhudia gari moja aina ya Toyota Canter likiingia hospitalini hapo majira ya Saa 4 asubuhi likiwa limewabeba wapenzi hao walionasiana huku wakiwa wamefunikwa shuka la nyumba ya wageni walikokuwa wakiponda raha.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, Mganga Mkuu Mfawidhi wa hospitali hiyo alikanusha madai hayo kwa kusema ni uzushi usio na maana.
Endelea kuperuzi ziro99blog kwa taarifa zaidi za mkasa huu.

SHEKHE PONDA NA SHEKHE FARID WARUDISHWA RUMANDE...

Shekhe Ponda Issa Ponda akiwa mahakamani Kisutu.
Hati maalumu za wakurugenzi wa mashitaka Zanzibar na Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania, zimeendelea kuwaweka rumande Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Shekhe Farid Hadi Ahmed na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Shekhe Ponda Issa Ponda.
Jana katika Mahakama ya Wilaya ya Mwanakwerekwe Zanzibar, masharti ya dhamana ya Shekhe Farid na washitakiwa wenzake katika kesi ya uchochezi na kufanya fujo inayowakabili, yalitolewa na Hakimu Ame Msaraka Pinja.
Hata hivyo, kama angeyatimiza, hati maalumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka  Zanzibar kupinga dhamana ya Shekhe Farid na wenzake katika kesi nyingine inayomkabili katika Mahakama Kuu ya Vuga, ilitosha kumrudisha rumande.
Katika masharti yaliyotangazwa jana na Hakimu Pinja, Shekhe Farid na wenzake walitakiwa kuwasilisha mahakamani Sh milioni moja taslimu kwa kila mmoja pamoja na kuwa wadhamini watatu ambao ni watumishi wa Serikali kwa kila mmoja na wawasilishe barua za kutambulishwa na waajiri wao na vivuli vya vitambulisho vyao vya kazi.
Pia wadhamini hao kila mmoja alitakiwa kuweka dhamana ya Sh milioni moja, kuwasilisha barua kutoka kwa Sheha wa Shehiya anayoishi na kivuli cha vitambulisho vya ukazi na kwa wenye hati za kusafiria pia wawasilishe vivuli vya hati hizo.
Washitakiwa wengine wanaokabiliwa na mashitaka hayo pamoja na Shekhe Farid ni pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Uamsho, Shekhe Mselem Ali Mselem, Mussa Juma Issa, Azan Khalid Hamdani, Khamis Ali Suleiman na Hassan Bakari Suleiman.
Mbali na hati maalumu ya Mkurugenzi wa Mashtaka  Zanzibar kupinga dhamana zao katika kesi nyingine kwenye Mahakama Kuu ya Vuga, washitakiwa hao pia walishindwa kutimiza masharti ya dhamana katika kesi inayowakabili katika Mahakama ya Mwanakwerekwe.
Awali kabla ya washitakiwa hao kurejeshwa rumande, mawakili wao wakiongozwa na Abdalla Juma na Salum Toufiqi waliiomba mahakama kutoa agizo la kuwapa haki zinazostahili wateja wao, ikiwamo askari wa Magereza kuruhusu mahabusu hao waonane na familia zao na wapewe chakula kizuri.
Mawakili hao pia walitaka wateja wao wawekwe katika chumba kimoja na kupinga utaratibu wa kuwaweka kila mtu na chumba chake.
“Tunasikitika sana, si haki na inaonekana wazi kwamba askari wa vyuo vya mafunzo (Magereza) wanapindisha sheria ikiwamo kuwanyima haki ya kuonana na mawakili wao,” alidai Wakili Juma.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 21 itakapotajwa na washitakiwa leo wanatazamiwa kufikishwa katika Mahakama ya Vuga kujibu mashitaka matatu mengine, ikiwamo la uharibifu wa mali, kushawishi na kuchochea, kurubuni watu kufanya fujo na kula njama ya kujificha kwa Shekhe Farid.
Shekhe Azan atasomewa mashitaka pekee yake ambayo ni ya uvunjifu wa mali pamoja na kumshambulia kwa maneno makali Kamishna wa Polisi.
Wakati Shekhe  Ponda akiendelea kusota rumande kwa kunyimwa dhamana na hati ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP),  wafuasi wake 49  wanaokabiliwa na mashitaka ya uchochezi na wizi wa mali zenye thamani ya Sh  milioni 59 wamepata dhamana.
Washitakiwa hao walipata dhamana baada ya kukamilisha masharti yaliyowataka kuwa na mdhamini mmoja anayefanya kazi katika taasisi inayofahamika, atakayesaini hati ya Sh milioni moja.
Hakimu Victoria Nongwa wa Mahakama ya Hakimu Kisutu alitoa dhamana hizo juzi kwa washitakiwa 19 na jana washitakiwa 30.
Washitakiwa walifikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi wakisindikizwa na magari saba ya Polisi likiwamo gari la maji ya kuwasha, na kila aliyeingia mahakamani hapo alikuwa akikaguliwa kwa kifaa maalumu kinachobaini kama amebeba silaha.
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka matano ya kula njama na kuingia kwa nguvu na kujimilikisha kiwanja kinachomilikiwa na kampuni ya AgriTanzania  Ltd, kilichopo katika eneo la Chang’ombe Markasi na kisha kuiba mali zenye thamani ya Sh milioni 59.7. 
Aidha, katika mashitaka ya uchochezi yanayomkabili Shekhe Ponda peke yake, inadaiwa katika eneo hilo kwa maelezo kuwa yeye ni Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu (T) alishawishi  wafuasi wake ambao ni washitakiwa hao kutenda makosa hayo.
Katika hatua nyingine Salum Shaban, Salum Mkuraga, Ernest Sylvester, Josephat Aloyce, Edwin Sadoki, Stanley Nhonya, Athuman Sajuki, Thabit Kombo, Abdully Rashid, Sadick Mustapha, Niga Ndinganya wamefikishwa mahakamani hapo wakishitakiwa kufanya mkusanyiko bila kibali.
Wakili wa Serikali Shedrack Kimaro alidai mbele ya Hakimu Liad Chamshana kuwa Novemba 2 mwaka huu katika Msikiti wa Idrisa uliopo mtaa wa Tandamti, washitakiwa hawakutii amri ya askari iliyowataka wasifanye mkusanyiko wa aina yoyote.
Aliendelea kudai kuwa, siku hiyo washitakiwa walifanya mkusanyiko usio halali wenye lengo la kuvunja amani. Washitakiwa walikana mashitaka na kurudishwa rumande baada ya kukosa wadhamini na kesi hiyo itatajwa Novemba 20 mwaka huu.

CHADEMA YAKANA KUMTUMA TUNDU LISSU KUMSHITAKI RAIS KIKWETE...

Tundu Lissu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kutokana na kuwa makini hakiwezi   kumshitaki Rais Jakaya Kikwete bungeni kwa uteuzi wake wa majaji kama anavyotaka Mbunge wake wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Chama hicho kimepinga kumtuma Lissu kutoa kauli hiyo, kikisema si ya chama wala Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.
Juzi Lissu alimtaka Rais Kikwete kufuta uteuzi wa majaji aliowaita hawana sifa, maadili na vihiyo na kutishia kama hatafanya hivyo, ataomba asilimia 20 ya saini za wabunge ambazo ni kati ya 70 na 72, ili awasilishe hoja bungeni Rais ajadiliwe.
Kutokana na kauli hiyo, Chadema imesema amekidhalilisha chama hicho ambacho ni makini mbele ya jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu msimamo wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour Arfi alisema msimamo huo ni wa Lissu na si wa Chadema wala Kambi ya Upinzani.
“Suala la kumwondoa Rais si la mtu mmoja, linahitaji uamuzi wa chama, sisi Chadema tuko 42 pekee bungeni na saini zinazohitajika ni 72 hivyo hii si hoja kwa chama makini … jamii itatuonaje?” Alihoji.
Alisema Lissu ana haki akiwa mbunge, kutoa maoni yake, lakini kauli hiyo si ya Kambi Rasmi ya Upinzani wala Chadema na chama hicho hakiwezi kuchukua uamuzi mgumu wa aina hiyo bila theluthi mbili ya wabunge kuunga mkono.
“Hakuna kikao chochote cha chama au Kambi Rasmi ya Upinzani kilichokaa na kumwidhinisha kutoa tamko hilo. Baada ya kutafakari, tunasema kama mpango wa Lissu hautafanikiwa, utakuwa umekidhalilisha chama,” alisema.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti huyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini alisema kauli ya Lissu itawasilishwa kwenye vikao vya chama kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kuwekana sawa na kufahamishana kuwa tamko lolote la chama lazima lipate ridhaa kabla ya kufikishwa kwa umma.
Katika hoja yake, Lissu alisema mmoja wa majaji anaotaka aondolewe hana sifa za kielimu ya kuwa jaji kwani hana Shahada ya Kwanza katika Sheria, huku Jaji huyo wa Mahakama ya Rufani kwa sasa akiingia darasani kusomea Shahada ya Sheria.
Majaji wengine anaowapinga ni wasiokuwa na uwezo wa Kiingereza, aliyepata ujaji baada ya kuhitimu Shahada yake Chuo Kikuu Huria na kuanza kazi wakati inatakiwa awe amefanya kazi angalau miaka 15.
Pia alikuwa anapinga wastaafu wanaofanya kazi ya ujaji kwa mikataba lakini bila kuapa, hivyo wanafanya kinyume cha sheria. Alisema pia yupo aliyedanganya umri wa kuzaliwa ili aendelee kubaki madarakani kwa muda mrefu.
Lissu alisema Rais asipofuta uteuzi huo haraka, ataanzisha mchakato wa kuwasilisha hoja maalumu ya kumjadili na uteuzi wake wa majaji. Kanuni za sasa haziruhusu kumjadili Rais ndani ya Bunge.
Hata hivyo, pamoja na Rais kuwa na madaraka ya kuteua jaji, hana madaraka ya kumfukuza au kumwachisha kazi, kwani nafasi zao baada ya kuteuliwa hufanya kazi wakiongozwa na Katiba na si kwa ridhaa ya Rais, hivyo hawezi kumfukuza kazi Jaji Mkuu au jaji yeyote.
Akizungumzia kauli ya Lissu ya kumtaka Spika Anne Makinda kutangaza bungeni uchunguzi uliofanywa dhidi yake na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi baada ya kutoa tuhuma bungeni dhidi ya majaji, Arfi alisema Lissu anatakiwa kufuata sheria inayokataza kuzungumzia uchunguzi huo na kuongeza mamlaka ya mbunge yana kikomo.
Alipotafutwa Lissu kwa njia ya simu jana kuzungumzia kauli ya chama chake, alisema hakuzungumza kama chama bali alitoa kauli kama Mbunge na ni msimamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani.
“Nimezungumza kama Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika masuala ya Katiba na Sheria na Kiongozi wa Upinzani (Freeman Mbowe) na Naibu wake (Kabwe Zitto) wanafahamu. Huo si msimamo wangu ni wa wabunge pia wa upinzani.
“Yeye (Arfi) ni mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hivyo anaunga mkono kuzimwa ripoti ya Ngwilizi au Katiba? Ukiukaji Katiba si suala dogo, mimi ndiye msemaji wa masuala ya sheria na hili lilianza tangu Bunge lililopita kwa nini wakati ule asiseme iwe sasa?” Alihoji.

MAJAMBAZI WENYE PIKIPIKI WAPORA MADUKA WAKIWA NA MASHOKA MKONONI...

Tukio hili la aina yake ambapo majambazi sita wakiwa kwenye pikipiki zao waliwatia hofu wateja kwenye maduka wakati walipovamia kwa kasi na kupora.
Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kuvaa kofia ngumu, majambazi hao waliendesha kwa spidi ndani ya maduka wakiwa wamepanda pikipiki tatu zenye nguvu mara tu baada ya muda wa kufunguliwa maduka hayo juzi.
Watatu ambao walikuwa wamekaa kiti cha nyuma waliruka na kutumia mashoka na kuvunja madirisha katika duka la vito.
Mashuhuda walisema watu hao walikimbilia eneo la juu la maduka hayo na kuvamia duka la vito la Fraser Hart, lililoko kwenye jengo la Brent Cross Shopping Centre huko North London.
Wanaaminika kuwa wameiba saa aina ya Cartier na Rolex na pia vitu vingine kadhaa vya thamani kabla ya kutokomea kwa kasi kusikojulikana.
Mashuhuda wameelezea jinsi wateja walivyopata mshituko wakati ujambazi huo ulipotokea,  huku wengi wakikimbilia kwenye milango la kutokea. Baadhi ya maduka yalizuia wateja kuondoka wakati ujambazi huo ukifanyika.
Michelle Webber mwenye miaka 36, alikuwa kwenye jengo hilo wakati ujambazi huo ukifanyika. Aliingia kwa kupitia mlango huohuo ambao inadhaniwa kwamba majambazi hao walitumia, karibu na John Lewis na New Look.
Alisema wakati akiingia - takribani dakika kumi kabla ya uporaji kufanyika - alisikia mtu nyuma yake akisema: "wacha burudani ianze".
Muda mfupi baada ya hapo alielezea jinsi wimbi la mashaka lilivyotawala eneo lote la maduka katika jengo hilo.
"Mtu mmoja alitufuata tulipokuwa na kupaza sauti 'kila mtu atoke nje'.
"Wazo langu la kwanza lilikuwa kulikuwa na bomu na nikaanza kufikiri kuhusu watoto wangu na familia yangu, tumbo langu lilivurugika. Watu walianza kukimbilia nje ya maduka wakiwa kwa hofu.
"Kulikuwa na umati mkubwa wa watu ulikuwa ukija kwetu. Wote walikuwa wakikimbia kwa wakati mmoja kujiokoa na kile kilichokuwa kikitokea.
"Nilikamatwa na mtu aliyekuwa akipaza sauti na kusema kwamba kulikuwa na watu wenye pikipiki ghorofani huku wakiwa na mashoka wamevamia na kupora duka la vito."

JICHO LA TATU...


CHEKA TARATIBU...

Jamaa alikuwa porini mara akatokea simba mbele yake. Kwa woga jamaa akapiga magoti na kuanza kusali huku kafumba macho. Ile kufumbua macho akamuona yule simba naye kafumba macho akisali. Jamaa kwa mshangao akauliza, "Ebo, kumbe na wewe Mkristo?" Simba akamjibu kwa ukali, "Funga domo lako. Kwani wewe huwa husali kabla ya kula?" Kasheshe...

Wednesday, November 7, 2012

MAZISHI YA ASKOFU BALINA KUFANYIKA SHINYANGA...

Marehemu Askofu Aloysius Balina.
Askofu Aloysius Balina (67) wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, aliyefariki dunia jana kwa saratani ya ini, anatarajiwa kuzikwa Ngokolo, Shinyanga.
Kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Tarsicius Ngalalekumtwa, Askofu Balina alifariki dunia jana mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza ambako alilazwa kwa takribani miezi miwili.
Mapema jana, Mkurugenzi wa Habari wa Jimbo Kuu la Mwanza, Padri Christopher Kubeja akiwa Mwanza alithibitisha kifo cha Askofu Balina na kueleza kuwa mwili wake umehifadhiwa Bugando.
“Ninaomba waumini wa Kanisa Katoliki jijini hapa na mikoa yote nchini waendelee kuwa watulivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na Baba yetu mpendwa Askofu Balina,” alisema Padri Kubeja.
Alisema taratibu za mazishi zinafanywa Ngokolo, ambako alisema pia utaratibu rasmi wa mazishi hayo utafanyika katika Jimbo hilo Jumamosi.
Makamu Msaidizi wa Askofu Jimbo Kuu la Shinyanga, Padri Sospeter Shole, alisema Jimbo limeupokea msiba huo kwa mshituko mkubwa na majonzi.
“Askofu Balina nimemfahamu kama mwalimu wangu nikiwa Katibu wake kwa muda mrefu, huu ni msiba mkubwa kwetu,” alisema. 
Alisema kufariki dunia kwa Askofu Balina ni pigo kwa waumini wa Shinyanga na mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na utume wake uliotukuka wa kuwapenda waumini na kuwaendeleza kielimu vijana wasiokuwa na uwezo kifedha.
“Alikuwa Askofu aliyependa watu na Jimbo lake kwa ajili ya kuliendeleza kielimu, ambapo alisomesha vijana na madaktari zaidi ya watano ambao hawakuwa na uwezo kifedha wamesoma kupitia mikononi mwake. Tutamkumbuka kwa upendo wake kwetu. Alikuwa Askofu aliyejitoa kuendeleza wakazi wake wa Shinyanga na nje ya mkoa kielimu,” alisema.
Padri Shole alisema mipango ya mazishi inaandaliwa jimboni Shinyanga na kutakuwapo na misa ya kumwombea marehemu leo kuanzia saa 10 jioni katika Kanisa Kuu, Ngokolo mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde alisema kifo cha Askofu Balina ni pigo kwa Baraza na hawana uwezo wa kuzuia mapenzi ya Mungu.
Kifo cha Askofu Balina kimekuja miezi michache tangu kifo cha Askofu Pascal Kikoti wa Jimbo la Mpanda mkoani Katavi. Askofu Kikoti alifariki dunia Agosti mwaka huu.
Askofu Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika kijiji cha Isoso Bariadi mkoani Shinyanga (sasa Simiyu) na alipata Daraja Takatifu la Upadri Juni 27, 1971 na kuteuliwa na Baba Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Geita, Novemba 8, 1984.
Aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Geita, Januari 6, 1985 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Roma, Italia.
Agosti 8, 1997 aliteuliwa na Baba Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga na kusimikwa jimboni humo Novemba 17, 1997 kuwa Askofu wa tatu wa jimbo. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 41 ya upadri na 27 ya uaskofu.

MTANZANIA AUAWA NCHINI KENYA AKIJARIBU KUPORA...

Kamanda Justus Kamugisha.
Mtanzania ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Mwara Kijiji cha Nyarwana wilayani Tarime,  Samwel Nyangarya (45) ameuawa na polisi nchini Kenya akituhumiwa kuhusika katika jaribio la kutaka kupora fedha katika duka la M-Pesa.
Aidha polisi imewatia mbaroni wanawake wawili raia wa Kenya, Stela Mgaka (32) na Lucy Mgaka (20)  kwa tuhuma za kutorosha hospitalini mwili wa Nyangarya na kuusafirisha kwa njia za panya kwenda kijijini kwake  kwa ajili ya maziko.
Nyangarya ambaye inadaiwa alikuwa akisakwa na polisi nchini  na wa Kenya kutokana na kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ikiwemo pia nchini Uganda,  aliuawa na polisi katika wilaya ya Nakuru, Kenya. Aliuawa pamoja na Chacha Mkisii wakituhumiwa kutaka kupora katika duka la Joshua Gathuki.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Justus Kamugisha alithibitisha kuwa alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na kwamba  aliuawa usiku wa Oktoba 25 katika mtaa wa Shule ya Msingi Mwariko, Nakuru. Walikutwa na bastola aina ya Chinese S/No, RC1964-21 ikiwa na Magazini mbili zenye kubeba risasi nane kila moja.
Kamugisha alisema  Nyangarya alipigwa risasi mgongoni na Mkisii  alipigwa kifuani na kufariki papo hapo. “Tulipopata taarifa za tukio hilo la kuuawa  Nyangarya tarehe 2 Novemba tulituma timu ya wapelelezi kuatilia tukio hilo hadi Nakuru ili kubaini mwili wa Nyangarya,” alisema.
Akizungumzia utoroshwaji wa mwili wa mtuhumiwa huyo, Kamanda alisema “lakini tulikuta mwili ukiwa umechukulia kutoka chumba cha maiti katika Hospitali ya Manispaa ya Nakuru kwa njia ya utata na kuacha mwili wa Chacha  Mkisii ukiwa chumba cha maiti.
Kwa mujibu wa kamanda, wanawake hao  walidai kwamba marehemu alikuwa akiitwa Sammy Mogaka mwenyeji wa Kisii Kenya. Waliondoka na mwili huo kinyemela  kutaka kuuleta Tanzania kwao Nyarwana kwa Maziko, " alisema.
Kamanda alisema katika kufuatilia mtandao wa wahalifu sanjari na waliotorosha mwili wa marehemu, polisi iliweka mtego na Novemba 3 mchana ndipo walikamatwa wanawake hao wawili.
Mwili huo ulivushwa na kuingizwa katika maeneo ya Nyamwaga mpakani kwenye Tarafa ya Ingwe. Wsafirishaji hao walikuwa katika gari aina ya Land Rover yenye Namba za Usajili T T 980 ACG  mali ya mkazi wa mjini Tarime. Polisi imesema inaendelea kuwahoji wanawake hao.
Miongoni mwa matukio ya uhalifu ambayo Nyangarya (marehemu) anadaiwa kuhusika ni pamoja na mauaji ya mwenyekiti wa kijiji cha Nyarwana na diwani wa kata Kibasura wilayani. Anadaiwa pia kuhusika katika mauaji ya askari na kujeruhi mwingine katika uvamizi wa Benki ya Stanbick Nyamongo.
Maeneo mengine anayotuhumiwa kuhusika katika ujambazi ni kwenye miji ya Kahama (Shinyanga), Geita, Kisii (Kenya), Mwanza, Tarime, Isebania (Kenya), Kisumu (Kenya), Uganda na Dar es Salaam. Polisi imeomba ushirikiano wa wananchi kwa polisi wa Tanzania, Kenya na Uganda katika kufichua kikosi cha watu waliokuwa wakishirikiana na Nyarwana katika uhalifu ili wakamatwe.

BINTI WA MIAKA 17 ABAKWA KISHA KUNYONGWA KIKATILI MWANZA...

Muonekano wa Jiji la Mwanza kutokea Ziwa Victoria.
Msichana mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Nyegezi wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, amekufa baada ya kubakwa na kisha kunyongwa na  watu wanaosadikiwa alifahamiana nao. 
Binti huyo ambaye mwaka huu alihitimu kidato cha Nne  katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma ya mkoani hapa,  alikumbwa na mauti baada ya kupigiwa simu na mtu anayedhaniwa kumfahamu.
Baba wa mtoto huyo alisema kwamba akiwa nyumbani kwao usiku wa kuamkia juzi kati ya saa 4 na 5 usiku, aliondoka kwenda kwa mtu huyo na hakurudi nyumbani.
“Walimteka na kumfunga kamba shingoni, maana tumekuta shingo yake ikiwa na alama za kamba halafu walimbaka hadi kufa na mwili wake tumeuhifadhi katika hospitali ya rufaa ya Bugando  kwa uchunguzi zaidi…nishukuru jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa ushirikiano wanaoendelea kunipatia hadi sasa kuwasaka wauaji wa mwanangu.”
Alisema kulipokucha asubuhi walianza kumtafuta na walifanikiwa kuikuta maiti yake ikiwa karibu na kisima cha kutekea maji katika eneo la Nyegezi akiwa amekufa.
Alisema, “Tuliukuta mwili wake ukiwa karibu na eneo la kisima, akiwa amekufa inaonekana walipomkamata walimbaka kwanza na kisha wakaamua kumnyonga kwa kamba”.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Liliani Matola alithibitisha kuwepo tukio hilo. Alisema polisi inaendelea kuchunguza kubaini chanzo cha mauaji hayo.

KATIBU WA MUFTI ZANZIBAR AMWAGIWA TINDIKALI...

Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhil Soraga akitolewa katika chumba cha huduma ya kwanza katika Kospitali Kuu ya Mnazi Mmoja, Zanzibar baada ya kumwagiwa tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Viwanja vya Mwanakwerekwe, Zanzibar jana asubuhi.
Licha ya viongozi wa kitaifa na kimataifa kutaka utulivu na amani visiwani Zanzibar, hali inaonekana kutotengemaa na kuzidisha hofu miongoni mwa wananchi.
Kinachoonekana sasa ni wimbi la kutaka kukomoa baadhi ya viongozi wa dini ya kiislamu wanaopingana na msimamo wa kikundi kingine cha waumini wa dini hiyo na sasa kufikia hatua ya kudhuriana kimwili.
Hali inaonekana kuwa hiyo baada ya Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Fadhil Suleiman Soraga (55), kujeruhiwa usoni, kichwani, kifuani, mgongoni na mikononi kwa kumwagiwa tindikali na mtu asiyefahamika.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Aziz Juma Mohammed, alisema jana kwamba Shekhe Soraga, alimwagiwa tindikali hiyo jana asubuhi kwenye viwanja vya Mabata karibu na Msikiti wa Msumbiji akiwa katika mazoezi ya kutembea.
Alifafanua kuwa Shekhe Soraga alikuwa akitoka upande wa uwanja wa Michezo wa Amaan kwenda Mwanakwerekwe na alikutana na mtu ambaye naye alionekana kama mfanya mazoezi mwenzake akitoka upande wa Mwanakwerekwe kwenda Amaan.
Kamanda Mohammed aliyehusisha suala hilo na uhalifu wa kawaida, alisema walipokuwa wakipishana, mtu huyo akiwa na kimiminika hicho kwenye jagi la maji ya kunywa, alimmwagia Soraga usoni.
Alisema baada ya tukio hilo, Shekhe Soraga alikaa chini akiugulia maumivu na baada ya muda wasamaria wema walijitokeza na kumpeleka Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ambako alipatiwa matibabu ya awali na kisha kusafirishwa kwa ndege ya Serikali kwenda Dar es Salaam ambako amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan.
Wakati Polisi wakisisitiza kuwa hawapendi kuhusisha suala hilo na jambo lolote, ndugu wa karibu na baadhi ya viongozi wenzake, wamehusisha suala hilo na kitisho alichopewa baada ya kutoa hotuba ya Iddi el Fitri.
Mkuu wa Shughuli za Dini ya Kiislamu Zanzibar, Thabit Norman Jongo aliliambia gazeti hili akiwa  Aga Khan kuwa kabla ya kufikwa na janga hilo, Shekhe Soraga alipokea vitisho mbalimbali kutoka kwa watu wasiojulikana.
Alisema, alianza kutishwa baada ya kutoa hotuba iliyokemea vitendo vya kuchoma makanisa na kuhatarisha amani visiwani katika Baraza la Iddi el Fitr lililofanyika visiwani humo.
“Lakini pamoja na vitisho hivyo, hatujajua mhusika wa unyama huo ni nani. Hatufahamu kwa kweli na wala hatuhusishi kikundi chochote hadi polisi watakapoweka wazi watakayogundua katika uchunguzi wao,” Jongo alisema.
Mmoja wa ndugu wa familia ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini alisema katika hatua za awali inaonekana wazi kwamba hotuba aliyotoa siku ya swala ya Iddi katika Msikiti wa Muembe Shauri, ndicho chanzo cha matatizo hayo.
“Sisi tunajua, kwamba Shekhe Soraga hana maadui...lakini hotuba ya swala ya Iddi ilikera baadhi ya watu wakiwamo wafuasi wa Uamsho,” alisema.
Katika hotuba hiyo, Shekhe Soraga aliitaka Serikali kuwachukulia hatua kali viongozi wa Uamsho ambao wanaonekana wazi wazi kwamba ndio chanzo cha fujo na vurugu visiwani hapa.
Shekhe Soraga alisema vurugu hizo zimetia hasara kubwa Serikali kwa kuharibu miundombinu ya barabara na wananchi wa kawaida wakiwamo mama lishe.
Alitoa mfano wa mfanyabiashara mwanamke muuza matikiti ambayo yalivamiwa na wafanya vurugu na kuharibiwa kwa kukatwa mapanga.
Hotuba ya swala ya Iddi iliyotolewa na Shekhe Soraga ilihudhuriwa na Rais wa Zanzibar,  Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na viongozi waandamizi wa SMZ.
Baada ya hotuba hiyo, Rais Shein  alisema  hakuna mtu aliye juu ya sheria na kusisitiza kuwa viongozi waliohusika na fujo na vurugu watashughulikiwa na vyombo vya Dola.
Naye Mufti wa Zanzibar, Shekhe Salehe Kabi aliwataka wananchi wa Zanzibar  kuacha visa vya kulipizana visasi  ambavyo vinaweza kuleta vurugu na kuzua mtafaruku Zanzibar.
Alitaka watu wote kuwa wamoja na kushirikiana kwa kila jambo na kuonya kwamba tofauti za rangi, kabila, dini na itikadi za kisiasa zisiwe chanzo cha mfarakano wa umoja wa Wazanzibari.
Mke wa Soraga aliyefuatana na mwanawe wa kiume na Jongo, Aga Khan ambaye hakutaka kutajwa jina gazetini, alisema alibaini kudhurika kwa mumewe baada ya kutaarifiwa na wasamaria wema.
“Nilishangaa kuona muda unakwenda na mume wangu harejei mazoezini, ilikuwa kawaida yake kufanya mazoezi ya kutembea au kukimbia alfajiri lakini jana alipitisha zaidi muda. Kumbe alikuwa amemwagiwa tindikali, inaniumiza kwa sababu tunaumizana binadamu wenyewe,” alisema.
Kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Zanzibar akienda Dar es Salaam, Shekhe Soraga alisindikizwa na Balozi Seif, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Abdallah Mwinyi na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama na mashekhe kadhaa.

CHEKA TARATIBU...

Mkuu wa Jeshi la Wanamaji na Jenerali mmoja walikuwa wakivua samaki pamoja kwenye boti yao. Ghafla boti ikapigwa na wimbi kali na kupinduka huku jamaa hao wakihaha ziwani kujaribu kuokoa maisha yao. Mwishowe Mkuu wa Jeshi akafanikiwa kupanda tena kwenye boti na kufanikiwa kumuwokoa Jenerali. Wakiwa kwenye boti Mkuu wa Jeshi akasema,"Tafadhali usimwambie yeyote kuhusu tukio hili. Kama askari wangu wakijua siwezi kuogelea itakuwa aibu kubwa." Jenerali akajibu, "Usihofu. Nitakutunzia siri yako nawe utunze yangu. Mimi bwana sipendi kabisa watu wangu wafahamu kwamba siwezi kutembea kwenye maji!" Duh...

MSICHANA AFA KWA KUPONDWA NA MAGURUDUMU YA TRENI...

JUU: Georgia Varley. CHINI: Christopher McGee. KULIA: Stesheni ya treni ilipotokea ajali hiyo.
Msichana wa umri chini ya miaka 20 ameangukia kwenye uvungu na kupondwa na magurudumu ya treni iliyokuwa kwenye mwendo kuamriwa na mlinzi ashuke sababu alikuwa amelewa kupita kiasi kinyume cha sheria za usafirishaji, mahakama ilielezwa juzi.
Georgia Varley mwenye miaka 16, alikufa papo hapo mara tu alipotumbukia katikati ya njia ya treni na treni wakati alipokuwa ametoka usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa rafiki yake aliyekuwa akitimiza miaka 18.
Juzi mlinzi aliyemwamuru kushika kwenye treni, Christopher McGee mwenye miaka 45, alifikishwa mahakama ya Liverpool akishitakiwa kwa kusababisha kifo.
Mahakama ilielezwa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita alivyokufa wakati akielekea mjini Liverpool katika matembezi ya usiku akiwa na rafiki zake.
Mapema, alikuwa kwenye sherehe nyumbani kwa rafiki yake aliyekuwa akisherehekea kutimiza miaka 18 ambako alikunywa vodka na anasemekana kuwa 'ndiye aliyekuwa amekunywa mno kupita wote katika sherehe hiyo'.
Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 4:30 usiku wa Oktoba 22, mwaka jana pale Georgia na marafiki zake walipowasili stesheni ya treni ya James Street mjini Liverpool kutoka West Kirby, huko Wirral.
Mwendesha mashitaka, Nicholas Johnson alisema: "Georgia alikuja Liverpool kwa matembezi ya usiku lakini kwa bahati mbaya hakuweza tena kurejea nyumbani. Hakuweza kutoka kwenye stesheni sababu aliachwa na treni aliyokuja nayo.
"Mtu mmoja pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuzuia tukio hilo lisitendeke ambalo limesababisha kifo chake.
"Christopher McGee alikuwa mlinzi katika treni na tunasema alifanya vitu viwili.
"Alimpa ishara dereva wakati hakuwa ameshindwa kutambua kwamba Georgia alikuwa hajaachia treni na alikuwa katika hali ya ulevi.
Alikuwa na uwezo wa kuona kuwa binti huyo alikuwa hajaachia treni na akijua au amnagalau kuhisi kwamba alikuwa amelewa mno, akatoa ishara kuruhusu treni ianze safari.
"Kilikuwa ni kitendo cha makusudi. Alitakiwa afahamu kwamba ingemsababishia Georgia kusukumwa kiasi cha kumfanya ayumbe na kumweka katika hatari ya kudhurika.
"Tunasema kwamba kuondoa treni peke yake kilikuwa ni kitendo cha jinai. Kitu cha pili alichofanya alishindwa kutoa ishara ya kusimamisha treni hali akijua kwamba Georgia angekokotwa chini ya uvungu wa treni ambapo angeingia kwenye hatari ya kifo.
"Hatusemi kwamba alidhamiria kumuua Georgia lakini hatari lazima ifahamike zaidi kwa mtaalamu aliyepata mafunzo ya usalama wa kwenye treni kuliko mtu yeyote yule."
Kesi hiyo inaendelea.

JICHO LA TATU...


Tuesday, November 6, 2012

SERIKALI YAIFUNGA SHULE YA SEKONDARI BAGAMOYO...



Habari zilizotufikia zinasema kuwa Serikali wilayani Bagamoyo leo imetangaza kuifunga Shule ya Sekondari Bagamoyo maarufu kama Magambani kwa muda usiojulikana kutokana na madai ya kuzuka ghasia za kidini.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari, imeelezwa kwamba ulifanyika uchaguzi wa Kiongozi wa wanafunzi shuleni hapo ambapo wagombea walikuwa ni wawili, mmoja wa dini ya Kikristo na mwingine Kiislamu.
Baada ya matokeo kutangazwa na mgombea kutoka dini ya Kikristo kushinda, inadaiwa kwamba wanafunzi wa Kiislamu walipinga matokeo hayo na ndipo ghasia hizo zikazuka.
Pia kulikuwa na madai kwamba wanafunzi wa Kiislamu walipanga kuchoma moto majengo ya shule hiyo, hivyo wanafunzi wa Kikristo kutakiwa kuondoka haraka kwenye maeneo ya shule hiyo.
Lakini chanzo chetu cha habari kimesema baadhi ya wanafunzi wa shule waliohojiwa kwa nyakati tofauti wamekanusha kuwa na tofauti hizo za kidini na kusisitiza kwamba ni kampeni chafu ya baadhi ya walimu wanaopandikiza mbegu mbaya ya udini miongoni mwa wanafunzi ili kuleta mtafaruku shuleni hapo.
Wameendelea kukieleza chanzo chetu kwamba, katika siku za karibuni walimu hao wamefikia hata kuwapachika majina wanafunzi hao kama Al-Shaabab, Al-Qaeda n.k.
Baadhi ya wanafunzi wa Kidato cha Sita wameelezea kusikitishwa kwao na hatua hiyo ya kuifunga shule hiyo hasa kwa kuzingatia kwamba wanakabiliwa na mitihani yao ya mwisho na hivyo kushindwa kujua hatima yao.
Shule hiyo imeelezwa kwamba inamilikiwa kwa pamoja na Wizara ya Elimu na Tamisemi.

ASKOFU BALINA WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA AFARIKI DUNIA...



Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Askofu wa Jimbo Kanisa Katoliki mkoani Shinyanga, Aloysius Balina amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza.
Askofu Balina ambaye hadi mauti yakimfika alikuwa na umri wa miaka 67, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani na kwamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili.
Habari zaidi za kina zitakujia baadaye hapa hapa ziro99blog.

MTUHUMIWA MAUAJI YA KAMANDA BARLOW ALISHIRIKI KUAGA MWILI WAKE...

Mwili wa Kamanda Liberatus Barlow ukiwa umeandaliwa tayari kwa ajili ya kuagwa kwenye Uwanja wa Nyamagana, Mwanza ambapo inasemekana mtu aliyehusika katika mauaji ya Kamanda huyo pia alihudhuria.
Polisi mjini hapa imebaini kuwa mmoja wa watuhumiwa wa mauaji ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow, alikwenda kuaga mwili wa Kamanda huyo katika uwanja wa Nyamagana sambamba na wananchi wengine.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Lily Matola jana alimtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Abdallah Petro ‘Ndayi’  (32) mkazi wa Mjimwema mjini hapa ambaye anashikiliwa Polisi.
Kwa mujibu wa Kamanda Matola, Petro mbali na kutajwa kuhusika na mauaji hayo, pia anadaiwa kuwa na rekodi ya kufungwa miaka 30 jela katika gereza la Butimba kwa unyang’anyi wa kutumia silaha mwaka 2006. Alitoka gerezani mwaka 2010 baada ya kukata rufaa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Petro pia imebainika pia kuwa ni mdogo wa mtuhumiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Muganyizi Peter.
Kamanda Matola alisema mbali na kuwa na uhusiano huo, Petro na mtuhumiwa mwingine, Abdurahim Ismail Athuman ‘Dula’ (28) mkazi wa Mkudi Ghana, pia mjini hapa, baada ya kukamatwa kwa nyakati tofauti Mjimwema na Kilimahewa mwishoni mwa wiki, waliwapeleka polisi mahali walikoficha baadhi ya mali za marehemu.
Mali  wanazodaiwa kuonesha polisi ni pamoja na redio  ya mawasiliano ya Polisi na funguo za gari alilotumia kamanda Barlow siku ya tukio la mauaji yake.
Kamanda Matola alisema watuhumiwa waliwapeleka polisi katika shimo la majitaka kwenye maeneo ya Nyanshana, jijini  Mwanza walipokuwa wameficha vitu hivyo. 
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Joseph Konyo alisema watuhumiwa baada ya kutimiza uhalifu, walitenganisha redio hiyo ya mawasiliano ili isipatikane.
“Damu ya mtu haipotei bure, hayo yote ni pamoja na Mungu mwenyewe, kwani sisi peke yetu hatuwezi, wananchi mmetusaidia sana,” alisema Kamanda Konyo.
Baada ya kuonesha polisi vitu hivyo ambavyo sasa vimechukuliwa kama vielelezo katika kesi ya    mauaji ya Barlow, Kamanda Matola alisema watuhumiwa hao  walipekuliwa na kukutwa pia na kadi tatu za simu za Vodacom na Airtel, simu ya mkononi, viatu vya ngozi na begi dogo.
Pia walikutwa na kofia mbili za kijeshi aina ya bereti; moja ikiwa ya Polisi na nyingine ya kampuni ya binafsi ya ulinzi, sare za kampuni ya ulinzi, mtarimbo, bisibisi, mapanga, televisheni mbili, sub-hoofer na deki. 
Alisema walipohojiwa, walidai wamekuwa wakihifadhiwa na Ryoba Matiku ‘Mama Nyangi’ katika eneo la Nyakabungo Miembeni ambako mipango yote ya uhalifu imekuwa ikisukwa. Mama huyo anashikiliwa pia kwa mahojiano.
Kamanda Konyo alisema suala la ulinzi na usalama huanzwa na wananchi kwenye familia zao na mtaa ili kujihakikishia shughuli za kutafuta riziki halali zinafanyika kwa amani na utulivu.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyanshana Mbugani, Maduhu Lutwenya aliwaomba wananchi kurudisha uhusiano wa kutoa taarifa pale watu wasiojulikana wanapopita kwenye mitaa yao kwani mawasiliano yangekuwapo, wahalifu hao wangekamatwa nao.
“Tuwe kitu kimoja, kwani suala la usalama si la Mwenyekiti peke yake ni la kila mmoja, kwani Kamanda aliyeuawa  hakuwa na hatia na mtu,” alisema.
Kukamatwa kwa watuhumiwa hao kunafanya idadi ya waliokamatwa kuhusika na kifo cha Kamanda Barlow, kuwa wanane na tayari watano wamefikishwa mahakamani.
Kamanda Barlow aliuawa usiku kati ya saa 7 na 8 Oktoba 12, katika eneo la Kitangiri kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi shingoni na kutokea kwenye taya na watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi.

WAFANYABIASHARA WADAIWA KUFICHA PETROLI...

Uhaba wa nishati ya mafuta unaoendelea kuikumba mikoa mbalimbali nchini umedaiwa kusababishwa na wafanyabiashara kuficha nishati hiyo wakisubiri bei mpya itakayotangazwa kesho na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Madini (Ewura).
Akizungumza jana, Mkurugenzi wa Mpango Unaoratibu Uagizaji wa Mafuta (PIC), Michael Mjinja alielezea kushangazwa na kuadimika kwa nishati hiyo na kwamba huenda wafanyabiashara wameficha bidhaa hiyo kusubiri bei mpya.
Kauli hiyo pia imeungwa mkono na mfanyabiashara maarufu nchini, Azim Dewji ambaye alidai kuwa kero ambayo Watanzania wanaendelea kupata, imetokana na  wafanyabiashara wengi kushindwa kuuza bidhaa hiyo kutokana na bei ndogo iliyopo na hivyo kukosa faida.
Wakati mafuta yakiadimika katika vituo vya reja reja, Mjinja aliliambia gazeti hili kuwa kuna mafuta mengi na ya kutosha nchini na akashangaa inakuwaje baadhi ya vituo vya mafuta kukosa nishati hiyo.
Alitoa mfano kuwa kuna meli iliyomaliza kupakua mafuta juzi na kufanya kiasi kilichopo kwenye soko la ndani kuwa ni lita milioni 33 za dizeli na lita milioni 31 za petroli na kwamba kuna meli nyingine ambayo imeanza kupakua mafuta ya ndani jana.
“Takwimu hizi ni kwa mujibu wa kampuni zinazonunua mafuta nje walizotoa jana (juzi)  nashangaa kuelezwa kuwa bado kuna upungufu wa mafuta,” alisema Mjinja na kufafanua kuwa jukumu lao ni kuagiza tu nishati hiyo, ila usambazaji wameachiwa Ewura.
Tatizo hilo limekuwa kubwa mikoani, lakini pia kwa jana katika baadhi ya vituo Dar es Salaam havikuwa na nishati hiyo, jambo ambalo linadaiwa kuwa ni wafanyabiashara kuyaficha kusubiri bei mpya kesho.  
Ewura imeweka utaratibu wa kutangaza bei mpya kila Jumatano  ya mwanzo ya  kila mwezi, hali ambayo inafanya wafanyabiashra walio wengi kuficha bidhaa hiyo kusubiri bei mpya.
Dewji alisema ukosefu wa nishati hiyo kwenye vituo vingi vya mafuta umetokana na wafanyabiashara kuona bei ya sasa haiwalipi na hata wanapotaka kuzungumza na Ewura hawafanikiwi.
“Kero yote hii imetokana na jeuri ya Ewura, hawataki kukutana na wafanyabiashara kuzungumzia suala la bei,” alisema Dewji.
Bei elekezi iliyotolewa na Ewura mwanzoni mwa Oktoba, petroli ilishuka kwa Sh 306 kwa lita na Sh 192 kwa lita moja ya dizeli.
Petroli kwa Dar es Salaam inauzwa Sh 1,994 kwa lita badala ya Sh 2, 300 ya Septemba,  dizeli bei yake ilishuka hadi Sh 1,950 kutoka Sh 2,142. Bei ya mafuta ya taa ilibaki Sh 1,993.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo hakutaka kutoa ufafanuzi wowote juu ya suala hilo la mafuta, kwa maelezo kuwa masuala yote yanazungumzwa na Wizara ya Nishati na Madini.
“Hilo suala liko ngazi ya juu, muulizeni Maswi (Eliakim-Katibu Mkuu wa Wizara) ndiye mwenye uwezo wa kuzungumzia masuala hayo,” alisema Kaguo. Maswi alisema atatoa kauli leo kuhusu suala hilo.
Hata hivyo, baadhi ya watu wanahoji, inakuwaje wafanyabiashara hao wasubiri bei mpya bila kujua kama inashuka au kupanda na kuhisi kuwapo watu ndani ya wizara husika kuvujisha ukokotoaji unaofanyika kabla ya kutangazwa.
Lakini wapo pia wanaosema huenda wafanyabiashara hao wanatumia muda mwingi kufuatilia bei ya soko la dunia na wanapoona mwelekeo ni kupanda bei ndipo nao kidogo kidogo wanaanza kuficha nishati hiyo.

MAMLAKA YA BANDARI VINARA WA RUSHWA KATIKA MANUNUZI...

Bandari ya Dar es Salaam.
Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), imetajwa kuongoza kwa viashiria vya rushwa katika ununuzi wa bidhaa na huduma unaosimamiwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Mkurugenzi Mtendaji wa PPRA, Ramadhani Mlinga alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa ununuzi katika taasisi za umma uliofanyika hadi Juni 30.
Mlinga alisema walipotumia kanuni za kupima rushwa katika ununuzi, TPA ilibainika kuongoza miongoni mwa taasisi za umma zilizokutwa na viwango vya juu vya uwezekano wa kuwapo rushwa kwa zaidi ya asilimia 20 ya shughuli za ununuzi.
Mbali na TPA iliyokuwa na asilimia 44 ya viashiria vya rushwa, ilifuatiwa kwa karibu na Wizara ya Mambo ya Ndani katika mradi wa ujenzi wa makao makuu ya kikosi cha Zimamoto iliyokuwa na asilimia 41 ya viashiria vya rushwa.
Taasisi ya tatu kwa kuwa na viashiria vingi vya rushwa kwa mujibu wa PPRA, ni Wizara ya Maji na Umwagiliaji katika mradi wa maji Chalinze iliyokuwa na asilimia 40.
Nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Kyela (28%), Halmashauri ya Wilaya ya Makete (27%), Halmashauri ya Jiji la Mbeya (28%), Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (20%), Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe (28%), Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (27%) na Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (23%)
Kuhusu ukaguzi wa miradi kwa thamani ya fedha, Mlinga alisema kati ya miradi 137 iliyokaguliwa, ni miradi 63 tu ndiyo ilitekelezwa kwa thamani ya fedha na kwa mujibu wa mkataba.
Alisema asilimia 49 ya miradi hiyo, utekelezaji wake ulikuwa wa wastani ambapo miradi saba sawa na asilimia 5, utekelezaji wake haukuridhisha kabisa.
Kuhusu malipo yanayotia shaka, Mlinga alisema ukaguzi huo umebaini kuwa kuna taasisi kumi zilizofanya malipo yenye shaka ya Sh bilioni 2.1 kwa makandarasi.
Alitaja taasisi hizo kuwa ni Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa, Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga, Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero, Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Nyingine ni Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Wakala wa Vizazi na Vifo (RITA), Mfuko wa Akiba kwa Wafanyakazi wa Serikalini (GEPF) na Halmashauri ya Wilaya ya Chato.
Mlinga alisema PPRA pia imefungia kampuni nne kushiriki zabuni zinazotangazwa na taasisi za umma kwa mwaka mzima baada ya kushindwa kutekeleza masharti ya mikataba yao katika zabuni walizowahi kupewa na kusababisha mikataba yao kuvunjwa.
Kampuni hizo ni pamoja na Shirika la Uzalishaji JKT (SUMA JKT) ya Dar es Salaam, Vector International ya Mwanza, Shy Builders Limited ya Shinyanga na Earthline Construction Limited ya Bukoba.

MTOTO WA MIAKA MIWILI AUAWA NA MBWAMWITU KWENYE BUSTANI YA WANYAMA...

Mtoto wa kiume mwenye miaka miwili ameng'atwa hadi kufa na mbwamwitu wenye njaa kali wakati alipodondoka kutoka sehemu aliposimamishwa na mama yake kwa ajili ya kuwatazama wanyama hao kwenye bustani ya wanyama ya Pittsburgh na Tangi la Samaki.
Waokoaji waliokata tamaa wakisaidiwa na walinzi wa bustani hiyo pamoja na askari polisi wenye silaha walijaribu kuwashusha makali wanyama hao wenye uchu wakati wakimshambulia vikali mtoto huyo, kutoka Pleasant Hills, mjini Pittsburgh, Jumapili asubuhi.
Walinzi wa bustani hiyo walifyatua vishale na maofisa polisi wakafyatua risasi, na kuua mmoja wa mbwamwitu hao, mnyama hatari zaidi, lakini waokoaji bado hawakuweza kumfikia mtoto huyo kwa wakati muafaka.
Gazeti la Pittsburgh Post limeripoti kwamba mtoto huyo alianguka kutoka alipokuwa na kupenya kwenye wavu ambamo mbwamwitu walikuwa wakioneshwa majira ya saa 5:45 asubuhi ya Jumapili.
Mama yake aliyejawa na woga, mwenye miaka 34, ambaye alimpeleka mtoto huyo kwenye bustani, alishuhudia wakati mbwa hao wakimshambulia mtoto wake.
Polisi hawafahamu kama mtoto huyo alikufa kutokana na kuanguka kutoka katika wavu huo wenye urefu wa futi 11 au kufuatia shambulio hilo.
Luteni Kevin Kraus kutoka polisi wa Pittsburgh ameelezea tukio hilo kuwa ni ya 'kuogofya.'
"Kwa bahati mbaya, mbwa hao walielekeza akili zao kwenye shambulio na si kufuata maelekezo ya walinzi wa bustani hiyo kujaribu kuwadhibiti," uongozi wa bustani hiyo ulisema katika taarifa yake.
Walinzi wa bustani hiyo kwa haraka wakafanikiwa kuwatimua mbwamwitu saba, ambao walikuwa wadogo kidogo kuliko Labrador, lakini wengine hawakuweza kuzuilika.
Wafanyakazi walivuka wavu huo na kuwapigia kelele wanyama hao katika juhudi za kuwazuia. Mvua ya vishale pia haikufanikiwa kuwarudisha nyuma wanyama hao.
Pale polisi wa Pittsburgh walipoingilia kati, hasa mbwa mmojawapo alipunguzwa kasi na kuacha kumshambulia mtoto huyo. Alikuwa kapigwa risasi na ofisa mmoja wa polisi.
Maofisa wa bustani hiyo ya wanyama walisema kuna wavu mbele ya sehemu ya kusimamia, lakini Luteni Kraus alisema ulitengenezwa kwa ajili ya kunasa vitu vidogo kama kamera, na sio binadamu.
Wachunguzi hawakusema sababu hasa za kifo, alisema.
Ofisi ya Mkemia ya Allegheny County alisema jina la mtoto huyo halitawekwa hadharani hadi baadaye leo (Jumapili).
Mtoto huyo na mama yake walikuwa wakitembelea bustani hiyo pamoja na jamaa zao - mtu mzima na mtoto mwingine - wakati wa shambulio hilo.
Polisi walisema baba wa mtoto huyo aliwasili mapema baasa ya tukio hilo na kwamba wazazi hao wote wawili wanapatiwa matibabu kufuatia mshituko waliopata.
Bustani hiyo ilifungwa, na haikufahamika mara moja lini hasa itafunguliwa tena, mamlaka zimesema.
"Kelele ziliendelea kusikika kutoka kila upande: "Msaada. Tusaidieni jamani," shuhuda Angela Ciniti mwenye miaka 20, ambaye alitembelea bustani hiyo akiwa na rafiki yake wa kiume amelieleza Gazeti la Pittsburgh-Post.
"Tulikuwa njiani kwenda kutazama dubu ndipo tukasikia kelele kali za kuomba msaada," anakumbuka Ciniti. "Mtu fulani alikuwa akiomba msaada, akiomba mtu yeyote asaidie."
Wamekuwa maarufu kwa kuua kongoni na pundamilia, ingawa kwa kawaida wamekuwa wakishambulia wanyama wasiokuwa na hatari.
Mbwa hao, ambao ni hatari, ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi kwatika Uwanda wa Serengeti.
Katika mawindo yao huishia kufanikiwa kuua asilimia 80 kwa wakati mmoja. Simba hufanikiwa kuua kiwango cha asilimia 30 pekee.

'DOGO' MKALI WA FILAMU YA "KARATE KID" ATIMIZA MIAKA 50!...

KUSHOTO: Ralph Macchio alivyo sasa. KULIA: Ralph akiwa na Pat Morita 'Mr. Miyagi' (kulis) katika filamu ya Karate Kid.
Yule dogo mkali wa filamu ya "Karate Kid", Ralph Macchio sasa ana umri wa miaka 50!
Ni ngumu kuamini, lakini Ralph amesherehekea kutimiza miaka hiyo jana, ikiwa ni miaka 28 tangu filamu hiyo ilipoingia mtaani kwa mara ya kwanza.
Alizaliwa Novemba 4, 1961 na kwamba alicheza filamu ya "Karate Kid I" mwaka 1984 (akiwa na miaka 23) na "Karate Kid II" mwaka 1986 (akiwa miaka 25).
Na kwa kipindi chote hicho tangu kuzinduliwa kwa filamu hiyo aliyocheza kama Daniel-san, Ralph amekuwa mvulana aliye bize mno.
Baada ya kuongoza katika "The Karate Kid" na filamu tatu zilizofuatia katika mfululizo wa filamu hiyo, Macchio aliendelea kufanya kazi katika filamu, akifanya muziki katika Broadway, akiigiza kwenye televisheni na siku za hivi karibuni kabisa alionekana kwenye "Dancing with the Stars."
Lakini wapi mfululizo wa filamu hizo ulipoishia?
Jambo la kuhuzunisha ni kwamba, Pat Morita (Mr. Miyagi) alifariki mwaka 2005, lakini nyota wengine waliocheza kwenye mfululizo wa filamu hiyo wamekuwa na mafanikio makubwa, huku wakitamba kwenye shoo kama "Glee" na "Mad Men" na wamechaguliwa kwenye Tuzo za Oscar na kushinda.

JICHO LA TATU...


CHEKA TARATIBU...

Padri kaingia kwenye baa na kuanza kuwahoji watu aliowakuta mle ndani., "Unataka kwenda mbinguni?" Mtu wa kwanza akajibu, "Ndio Fadha!" Padri akasema, "Simama pale ukutani." Kisha akamfuata wa pili na kumuuliza, "Unataka kwenda mbinguni? Yule mtu akajibu, "Bila shaka Padri." Padri akasema, "Simama pale ukutani." Akamfuata jamaa wa tatu na kumuuliza, "Unataka kwenda mbinguni?" Yule jamaa akajibu, "Hapana, sitaki." Padri kwa mshangao akasema, "Siamini hata kidogo. Unamaanisha kwamba ukifa hutaki kwenda mbinguni?" Jamaa akajibu kwa unyenyekevu, "Ooh, nitakapokufa, sawa. Nilidhani unatukusanya ili tuanze safari sasa hivi!" Duh…