![]() |
| Tundu Lissu. |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kutokana na kuwa makini hakiwezi kumshitaki Rais Jakaya Kikwete bungeni kwa uteuzi wake wa majaji kama anavyotaka Mbunge wake wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Chama hicho kimepinga kumtuma Lissu kutoa kauli hiyo, kikisema si ya chama wala Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni.
Juzi Lissu alimtaka Rais Kikwete kufuta uteuzi wa majaji aliowaita hawana sifa, maadili na vihiyo na kutishia kama hatafanya hivyo, ataomba asilimia 20 ya saini za wabunge ambazo ni kati ya 70 na 72, ili awasilishe hoja bungeni Rais ajadiliwe.
Kutokana na kauli hiyo, Chadema imesema amekidhalilisha chama hicho ambacho ni makini mbele ya jamii.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusu msimamo wa chama hicho, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Said Amour Arfi alisema msimamo huo ni wa Lissu na si wa Chadema wala Kambi ya Upinzani.
“Suala la kumwondoa Rais si la mtu mmoja, linahitaji uamuzi wa chama, sisi Chadema tuko 42 pekee bungeni na saini zinazohitajika ni 72 hivyo hii si hoja kwa chama makini … jamii itatuonaje?” Alihoji.
Alisema Lissu ana haki akiwa mbunge, kutoa maoni yake, lakini kauli hiyo si ya Kambi Rasmi ya Upinzani wala Chadema na chama hicho hakiwezi kuchukua uamuzi mgumu wa aina hiyo bila theluthi mbili ya wabunge kuunga mkono.
“Hakuna kikao chochote cha chama au Kambi Rasmi ya Upinzani kilichokaa na kumwidhinisha kutoa tamko hilo. Baada ya kutafakari, tunasema kama mpango wa Lissu hautafanikiwa, utakuwa umekidhalilisha chama,” alisema.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti huyo ambaye ni Mbunge wa Mpanda Mjini alisema kauli ya Lissu itawasilishwa kwenye vikao vya chama kabla ya mwisho wa mwaka huu ili kuwekana sawa na kufahamishana kuwa tamko lolote la chama lazima lipate ridhaa kabla ya kufikishwa kwa umma.
Katika hoja yake, Lissu alisema mmoja wa majaji anaotaka aondolewe hana sifa za kielimu ya kuwa jaji kwani hana Shahada ya Kwanza katika Sheria, huku Jaji huyo wa Mahakama ya Rufani kwa sasa akiingia darasani kusomea Shahada ya Sheria.
Majaji wengine anaowapinga ni wasiokuwa na uwezo wa Kiingereza, aliyepata ujaji baada ya kuhitimu Shahada yake Chuo Kikuu Huria na kuanza kazi wakati inatakiwa awe amefanya kazi angalau miaka 15.
Pia alikuwa anapinga wastaafu wanaofanya kazi ya ujaji kwa mikataba lakini bila kuapa, hivyo wanafanya kinyume cha sheria. Alisema pia yupo aliyedanganya umri wa kuzaliwa ili aendelee kubaki madarakani kwa muda mrefu.
Lissu alisema Rais asipofuta uteuzi huo haraka, ataanzisha mchakato wa kuwasilisha hoja maalumu ya kumjadili na uteuzi wake wa majaji. Kanuni za sasa haziruhusu kumjadili Rais ndani ya Bunge.
Hata hivyo, pamoja na Rais kuwa na madaraka ya kuteua jaji, hana madaraka ya kumfukuza au kumwachisha kazi, kwani nafasi zao baada ya kuteuliwa hufanya kazi wakiongozwa na Katiba na si kwa ridhaa ya Rais, hivyo hawezi kumfukuza kazi Jaji Mkuu au jaji yeyote.
Akizungumzia kauli ya Lissu ya kumtaka Spika Anne Makinda kutangaza bungeni uchunguzi uliofanywa dhidi yake na Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka inayoongozwa na Mbunge wa Mlalo, Hassan Ngwilizi baada ya kutoa tuhuma bungeni dhidi ya majaji, Arfi alisema Lissu anatakiwa kufuata sheria inayokataza kuzungumzia uchunguzi huo na kuongeza mamlaka ya mbunge yana kikomo.
Alipotafutwa Lissu kwa njia ya simu jana kuzungumzia kauli ya chama chake, alisema hakuzungumza kama chama bali alitoa kauli kama Mbunge na ni msimamo wa Kambi Rasmi ya Upinzani.
“Nimezungumza kama Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika masuala ya Katiba na Sheria na Kiongozi wa Upinzani (Freeman Mbowe) na Naibu wake (Kabwe Zitto) wanafahamu. Huo si msimamo wangu ni wa wabunge pia wa upinzani.
“Yeye (Arfi) ni mjumbe wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge hivyo anaunga mkono kuzimwa ripoti ya Ngwilizi au Katiba? Ukiukaji Katiba si suala dogo, mimi ndiye msemaji wa masuala ya sheria na hili lilianza tangu Bunge lililopita kwa nini wakati ule asiseme iwe sasa?” Alihoji.

No comments:
Post a Comment