Thursday, November 8, 2012

MAJAMBAZI WENYE PIKIPIKI WAPORA MADUKA WAKIWA NA MASHOKA MKONONI...

Tukio hili la aina yake ambapo majambazi sita wakiwa kwenye pikipiki zao waliwatia hofu wateja kwenye maduka wakati walipovamia kwa kasi na kupora.
Wakiwa wamevalia mavazi meusi na kuvaa kofia ngumu, majambazi hao waliendesha kwa spidi ndani ya maduka wakiwa wamepanda pikipiki tatu zenye nguvu mara tu baada ya muda wa kufunguliwa maduka hayo juzi.
Watatu ambao walikuwa wamekaa kiti cha nyuma waliruka na kutumia mashoka na kuvunja madirisha katika duka la vito.
Mashuhuda walisema watu hao walikimbilia eneo la juu la maduka hayo na kuvamia duka la vito la Fraser Hart, lililoko kwenye jengo la Brent Cross Shopping Centre huko North London.
Wanaaminika kuwa wameiba saa aina ya Cartier na Rolex na pia vitu vingine kadhaa vya thamani kabla ya kutokomea kwa kasi kusikojulikana.
Mashuhuda wameelezea jinsi wateja walivyopata mshituko wakati ujambazi huo ulipotokea,  huku wengi wakikimbilia kwenye milango la kutokea. Baadhi ya maduka yalizuia wateja kuondoka wakati ujambazi huo ukifanyika.
Michelle Webber mwenye miaka 36, alikuwa kwenye jengo hilo wakati ujambazi huo ukifanyika. Aliingia kwa kupitia mlango huohuo ambao inadhaniwa kwamba majambazi hao walitumia, karibu na John Lewis na New Look.
Alisema wakati akiingia - takribani dakika kumi kabla ya uporaji kufanyika - alisikia mtu nyuma yake akisema: "wacha burudani ianze".
Muda mfupi baada ya hapo alielezea jinsi wimbi la mashaka lilivyotawala eneo lote la maduka katika jengo hilo.
"Mtu mmoja alitufuata tulipokuwa na kupaza sauti 'kila mtu atoke nje'.
"Wazo langu la kwanza lilikuwa kulikuwa na bomu na nikaanza kufikiri kuhusu watoto wangu na familia yangu, tumbo langu lilivurugika. Watu walianza kukimbilia nje ya maduka wakiwa kwa hofu.
"Kulikuwa na umati mkubwa wa watu ulikuwa ukija kwetu. Wote walikuwa wakikimbia kwa wakati mmoja kujiokoa na kile kilichokuwa kikitokea.
"Nilikamatwa na mtu aliyekuwa akipaza sauti na kusema kwamba kulikuwa na watu wenye pikipiki ghorofani huku wakiwa na mashoka wamevamia na kupora duka la vito."

3 comments:

Anonymous said...

Hеy there! I know this is κinԁa
off toρic but Ӏ ωas wondering if you κnеw
where I cοuld fіnd a caрtchа plugin for my comment
fοгm? І'm using the same blog platform as yours and I'm having
ԁіfficulty finԁіng one?

Thanks a lot!

Неге is mу page Online Payday oan
Here is my homepage ... Online Payday oan

Anonymous said...

It's a pity you don't have a donate button! I'd most certainly donate to this outstanding blog! I suppose for now i'll
settle for book-marking and adding your RSS feed to my Google
account. I look forward to new updates and will share this blog with
my Facebook group. Talk soon!

Feel free to visit my webpage paydayloanshut1b.com

Anonymous said...

Online Payday Loan Payday loans are there willing identity check to payday it, you should pull out immediately?