![]() |
| PICHA NDOGO KUSHOTO: Naomi akiwa na mpenzi wake, Doronin. PICHA KUBWA: Sehemu ilipofanyika sherehe hiyo. KULIA: Naomi akiingia kwenye eneo la sherehe. |
Ilipangwa iwe sherehe ya aina yake kutokea katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, lakini mambo hayakwenda kabisa vile yalivyopangwa.
Naomi Campbell alisherehekea siku ya kuzaliwa mpenzi wake, Vladimir Doronin aliyekuwa akitimiza miaka 50 kwa ubadhirifu na pigo kubwa mjini Jodhpur mapema wiki hii, na licha ya kuwepo onesho la Diana Ross na orodha ya marafiki waliofika kutoka kote duniani, majirani hawakusisimka na makelele yote hayo.
Malalamiko ya kelele kutoka kwa wakazi wa eneo hilo la ngome ya karne ya 15 yamesababisha kukamatwa kwa meneja wake aliyesimamia maandalizi ya sherehe hiyo.
Meneja huyo mwenye makazi yake mjini Mumbai, P.K. Pareek alikamatwa kwa madai ya 'usumbufu wa kelele' baada ya sherehe hiyo iliyoandaliwa na Naomi na kufanyika kwenye ngome ya karne ya 15.
"Alikamatwa Alhamisi na kuachiwa kwa dhamana leo (jana)," Kamishna wa Polisi Bhupendra Kumar Dak alisema mjini Jodhpur, jiji la pili kwa ukubwa India lililoko kaskazini mwa Jimbo la Rajastham.
Dak alisema mtu huyo alikamatwa baada ya wakazi wa eneo hilo kulalamikia kelele kubwa ya mafataki yaliyokuwa yakipigwa katika sherehe hizo kwenye Ngome ya Behrangarh, Jumatano iliyopita.
Kamishna huyo alisema waandaaji wa sherehe hiyo walikuwa wameruhusiwa kutumia mafataki na muziki mkubwa hadi Saa 4:00 usiku na kwamba polisis walipelekwa kwenye ngome hiyo majira ya usiku wa manane pale wakazi walipolalamika kuzidi kwa kelele.
"Hadi kufikia usiku mkubwa kulikuwa na sauti kubwa ya muziki kutoka kwenye ngome hiyo na milipuko mikubwa ya mafataki iliyotupa usumbufu wa kiakili," alisema Kamlash Prohit, ambaye anaishi jirani na jengo lililochukua sehemu kubwa ya Jodhpur.
Sherehe hiyo ailihudhuriwa na takribani wageni 200, wakiwamo marafiki wasanii nyota kama Duchess of York Sarah Ferguson na Kate Moss.
Diana Ross alitumbuiza shoo ya kipekee, baada ya kuwa amelipwa Dola za Marekani 500,000 kuchombeza umati uliokuwa ukimetameta.
Mwanamitindo huyo mwenye miaka 42, amekuwa na mahusiano na Doronin tangu mwaka 2008 na wawili hao wamekuwa kwa sasa wanaishi pamoja mjini Moscow.
Wamekuwa na kawaida ya kuandaliana sherehe kwa kila mmoja, ambapo Doronin aliwahi kufanya sherehe kubwa kwa ajili ya kusherehekea miaka 40 ya kuzaliwa Naomi huko Riviera nchini Ufaransa.

No comments:
Post a Comment