Friday, November 9, 2012

WAFIKA KUSHUHUDIA WAPENZI WALIONASIANA HOSPITALI YA TEMEKE...

Polisi wakidhibiti umati wa maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam waliofika kwenye Hospitali ya Temeke kushuhudia wapenzi wanaodaiwa kunasiana wakati wakifanya mapenzi maeneo ya Mbagala, jana.
Maelfu ya wakazi wa Dar es Salaam wakiwa wamekusanyika nje ya lango kuu la kuingia katika Hospitali ya Temeke kushuhudia wapenzi wawili wanaodaiwa kunasiana wakati wakifanya mapenzi ambapo ilidaiwa kwamba waliletwa hospitalini hapo kwa ajili ya zoezi ya kutenganishwa. Hatua hiyo ya wakazi hao kukusanyika hapo ilisababisha huduma katika hospitali hiyo kusitishwa kwa zaidi ya masaa saba jana. Hatahivyo habari ambazo tumezipata jana jioni, Jeshi la Polisi limekanusha vikali uvumi huo na kusema hakuna tukio kama hilo lililotokea. Pia uongozi wa Hospitali ya Temeke nao umekanusha kupokelewa kwa wapenzi hao huku ukisisitiza kwamba taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

No comments: