Tuesday, November 6, 2012

ASKOFU BALINA WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA AFARIKI DUNIA...



Habari zilizotufikia hivi punde zinasema kwamba Askofu wa Jimbo Kanisa Katoliki mkoani Shinyanga, Aloysius Balina amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza.
Askofu Balina ambaye hadi mauti yakimfika alikuwa na umri wa miaka 67, alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani na kwamba alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili.
Habari zaidi za kina zitakujia baadaye hapa hapa ziro99blog.

No comments: