![]() |
| JUU: Georgia Varley. CHINI: Christopher McGee. KULIA: Stesheni ya treni ilipotokea ajali hiyo. |
Msichana wa umri chini ya miaka 20 ameangukia kwenye uvungu na kupondwa na magurudumu ya treni iliyokuwa kwenye mwendo kuamriwa na mlinzi ashuke sababu alikuwa amelewa kupita kiasi kinyume cha sheria za usafirishaji, mahakama ilielezwa juzi.
Georgia Varley mwenye miaka 16, alikufa papo hapo mara tu alipotumbukia katikati ya njia ya treni na treni wakati alipokuwa ametoka usiku kusherehekea siku ya kuzaliwa rafiki yake aliyekuwa akitimiza miaka 18.
Juzi mlinzi aliyemwamuru kushika kwenye treni, Christopher McGee mwenye miaka 45, alifikishwa mahakama ya Liverpool akishitakiwa kwa kusababisha kifo.
Mahakama ilielezwa mwanafunzi huyo wa kidato cha sita alivyokufa wakati akielekea mjini Liverpool katika matembezi ya usiku akiwa na rafiki zake.
Mapema, alikuwa kwenye sherehe nyumbani kwa rafiki yake aliyekuwa akisherehekea kutimiza miaka 18 ambako alikunywa vodka na anasemekana kuwa 'ndiye aliyekuwa amekunywa mno kupita wote katika sherehe hiyo'.
Ajali hiyo ilitokea majira ya Saa 4:30 usiku wa Oktoba 22, mwaka jana pale Georgia na marafiki zake walipowasili stesheni ya treni ya James Street mjini Liverpool kutoka West Kirby, huko Wirral.
Mwendesha mashitaka, Nicholas Johnson alisema: "Georgia alikuja Liverpool kwa matembezi ya usiku lakini kwa bahati mbaya hakuweza tena kurejea nyumbani. Hakuweza kutoka kwenye stesheni sababu aliachwa na treni aliyokuja nayo.
"Mtu mmoja pekee ndiye aliyekuwa na uwezo wa kuzuia tukio hilo lisitendeke ambalo limesababisha kifo chake.
"Christopher McGee alikuwa mlinzi katika treni na tunasema alifanya vitu viwili.
"Alimpa ishara dereva wakati hakuwa ameshindwa kutambua kwamba Georgia alikuwa hajaachia treni na alikuwa katika hali ya ulevi.
Alikuwa na uwezo wa kuona kuwa binti huyo alikuwa hajaachia treni na akijua au amnagalau kuhisi kwamba alikuwa amelewa mno, akatoa ishara kuruhusu treni ianze safari.
"Kilikuwa ni kitendo cha makusudi. Alitakiwa afahamu kwamba ingemsababishia Georgia kusukumwa kiasi cha kumfanya ayumbe na kumweka katika hatari ya kudhurika.
"Tunasema kwamba kuondoa treni peke yake kilikuwa ni kitendo cha jinai. Kitu cha pili alichofanya alishindwa kutoa ishara ya kusimamisha treni hali akijua kwamba Georgia angekokotwa chini ya uvungu wa treni ambapo angeingia kwenye hatari ya kifo.
"Hatusemi kwamba alidhamiria kumuua Georgia lakini hatari lazima ifahamike zaidi kwa mtaalamu aliyepata mafunzo ya usalama wa kwenye treni kuliko mtu yeyote yule."
Kesi hiyo inaendelea.

No comments:
Post a Comment