Mkuu wa Jeshi la Wanamaji na Jenerali mmoja walikuwa wakivua samaki pamoja kwenye boti yao. Ghafla boti ikapigwa na wimbi kali na kupinduka huku jamaa hao wakihaha ziwani kujaribu kuokoa maisha yao. Mwishowe Mkuu wa Jeshi akafanikiwa kupanda tena kwenye boti na kufanikiwa kumuwokoa Jenerali. Wakiwa kwenye boti Mkuu wa Jeshi akasema,"Tafadhali usimwambie yeyote kuhusu tukio hili. Kama askari wangu wakijua siwezi kuogelea itakuwa aibu kubwa." Jenerali akajibu, "Usihofu. Nitakutunzia siri yako nawe utunze yangu. Mimi bwana sipendi kabisa watu wangu wafahamu kwamba siwezi kutembea kwenye maji!" Duh...

No comments:
Post a Comment