![]() |
| KUSHOTO: Yasmin baada ya ajali hiyo. KULIA: Yasmin kabla ya ajali. |
Binti wa miaka 9 alivurumishwa futi 15 angani na kubamizwa kwenye uzio wa chuma baada ya kudondoka kutoka kwenye bembea la viwanja vya maonesho lililokuwa likiendeshwa kwa kasi ya mita 50 kwa saa.
Yasmin Vickery alikimbizwa hospitalini baada ya kufyatuliwa kutoka kwenye bembea hilo mbele ya mama yake alijawa na hofu, Kim, ambaye alihofia kwamba alikuwa amepooza.
Binti huyo alitibiwa shingo ambayo ilidhaniwa kwamba imevunjika kufuatia ajali hiyo iliyotokea Novemba 3 lakini katika hali ya kushangaza alinusurika kuvilia damu mwilini.
Jana Kim, mwanasheria wa kampuni alielezea tukio hilo la kutisha kwamba alihofia binti yake kwamba alikuwa amekufa.
Alisema: "YasMin alikuwa kwenye bembea pamoja na binamu yake mdogo Kya na chuma hilo likainuka juu, na alipojaribu kwenda kulirudisha alitupwa mbali.
"Alirushwa angani sababu lilikuwa likienda kasi mno, kisha unaweza kusikia mshindo huu. Alirushwa juu na kuvuka vizuizi.
"Wakati wote nilikuwa nikirekodi mwenendo wa bembea lile hadi pale liliposimama ghafla bila kujua kilichotokea, tulikuwa tukicheka na kutaniana wakati huo.
"Lakini ndipo nilipomwona binti yangu mdogo akiwa ametupwa upande mwingine. Mtoto wangu wa miaka sita alikuwa akitazama huku akibubujikwa machozi, alitishika mno - alidhani dada yake alikuwa amekufa.
"Nilipokimbilia kule na Yasmin alisema alikuwa amepoteza hisia sehemu za miguuni - nilifikiri kwamba amepooza, angeweza kufa kirahisi lakini alipata pigo kubwa kwa upande wake huo kuliko kichwani wakati huo.
"Athari zilikuwa upande kwa upande, lakini madaktari walisema kama angejibamiza kichwani kwanza basi ingekuwa hadithi nyingine, yaani angeweza kufa.
"Imekuwa ndoto mbaya kwa kila mama lakini najua ana bahati sana na ingeweza kuwa mbaya zaidi kuliko hivi ilivyo.
"Watu wengi huwa hawaponi kwenye ajali ya gari kwa spidi ile, kuchomoka peke yake na kutupwa angani mbali na bembea lile."
Mama huyo aliyeolewa mwenye watoto watatu, kim, mkazi wa Sevenoaks, huko Kent, sasa anapigania ukaguzi wa usalama kufanyika kwenye mabembea - ambao anaamini utafanywa na familia zinazosafiri kutoka Northampton.
Kim aliongeza: "Ninachomaanisha kama bembea lile litapelekwa kokote kwingineko basi inaweza kutokea tena ajali."
Yasmin bado yuko kitandani, na amekuwa akitapika kutokana na madhara aliyopata kwenye figo kufuatia ajali hiyo.
Binti huyo alisema: "Hakika inaumiza mno. Siendi tena shule kwa wiki au zaidi. Siweki uzito wowote kwenye mguu mmoja."
Tukio hilo lilishughulikiwa na polisi na huduma za gari la wagonjwa na sasa unafanyika uchunguzi wa afya na usalama.
Mpelelezi Sajenti Gavin Suttie kutoka Polisi wa Northamptonshire, alisema: "Tumeenda eneo la tukio huko Hollowell, ambapo binti wa miaka 9 amejeruhiwa vibaya kufuatia kudondoka kutoka kwenye bembea.
"Alipelekwa kwenye Hospitali Kuu ya Northampton akiwa na maumivu ya ndani kwa ndani na aliruhusiwa Jumapili. Mkuu wa Afya na Usalama ametaarifiwa na atasaidiwa na polisi katika uchunguzi."
Hakuna mtu yeyote kutoka kwenye viwanja hivyo vya maonesho aliyepatikana kuelezea kwa undani tukio hilo.

No comments:
Post a Comment