Friday, November 9, 2012

JERMAINE JACKSON AWASILISHA MAOMBI YA KUBADILI JINA LAKE...

Jermaine Jackson
Jermaine Jackson amefungua madai kisheria kuomba kubadili jina lake la mwisho ... akibadili "Jackson" kuwa "Jacksun" ... imefahamika.
Jermaine amefungua madai hayo ya kubadili jina kwenye Mahakama Kuu ya Los Angeles County juzi akitaka mabadiliko hayo katika mfumo wa majina.
Katika nyaraka, Jermaine amesema anataka kufanya mabadiliko kwa "sababu za kisanii" ... lakini hakutoa ufafanuzi wowote zaidi kuhusu hatua yake hiyo.
Ombi hilo bado halijathibitishwa na Jaji ... lakini shauri hilo limeshawekwa kwenye ratiba za mahakama.
Ili kufanikishwa uamuzi wake huo wa kiwendawazimu, Jermaine katika miezi kadhaa ijayo atatakiwa kutangaza hadharani mabadiliko ya jina lake mara kadhaa kabla ya kukubalika kisheria.
Matangazo kwa umma yanahusisha kuchapishwa kwa jina katika machapisho kashaa ya ndani ya eneo hilo ... kama ilivyofanyika kwa Ron Artest alivyolazimika kufanya pale alipobadili jina lake na kuwa Metta World Peace.

No comments: