![]() |
| Kamanda Justus Kamugisha. |
Mtanzania ambaye ni mkazi wa Kitongoji cha Mwara Kijiji cha Nyarwana wilayani Tarime, Samwel Nyangarya (45) ameuawa na polisi nchini Kenya akituhumiwa kuhusika katika jaribio la kutaka kupora fedha katika duka la M-Pesa.
Aidha polisi imewatia mbaroni wanawake wawili raia wa Kenya, Stela Mgaka (32) na Lucy Mgaka (20) kwa tuhuma za kutorosha hospitalini mwili wa Nyangarya na kuusafirisha kwa njia za panya kwenda kijijini kwake kwa ajili ya maziko.
Nyangarya ambaye inadaiwa alikuwa akisakwa na polisi nchini na wa Kenya kutokana na kujihusisha na ujambazi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ikiwemo pia nchini Uganda, aliuawa na polisi katika wilaya ya Nakuru, Kenya. Aliuawa pamoja na Chacha Mkisii wakituhumiwa kutaka kupora katika duka la Joshua Gathuki.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, Justus Kamugisha alithibitisha kuwa alikuwa akisakwa kwa muda mrefu na kwamba aliuawa usiku wa Oktoba 25 katika mtaa wa Shule ya Msingi Mwariko, Nakuru. Walikutwa na bastola aina ya Chinese S/No, RC1964-21 ikiwa na Magazini mbili zenye kubeba risasi nane kila moja.
Kamugisha alisema Nyangarya alipigwa risasi mgongoni na Mkisii alipigwa kifuani na kufariki papo hapo. “Tulipopata taarifa za tukio hilo la kuuawa Nyangarya tarehe 2 Novemba tulituma timu ya wapelelezi kuatilia tukio hilo hadi Nakuru ili kubaini mwili wa Nyangarya,” alisema.
Akizungumzia utoroshwaji wa mwili wa mtuhumiwa huyo, Kamanda alisema “lakini tulikuta mwili ukiwa umechukulia kutoka chumba cha maiti katika Hospitali ya Manispaa ya Nakuru kwa njia ya utata na kuacha mwili wa Chacha Mkisii ukiwa chumba cha maiti.
Kwa mujibu wa kamanda, wanawake hao walidai kwamba marehemu alikuwa akiitwa Sammy Mogaka mwenyeji wa Kisii Kenya. Waliondoka na mwili huo kinyemela kutaka kuuleta Tanzania kwao Nyarwana kwa Maziko, " alisema.
Kamanda alisema katika kufuatilia mtandao wa wahalifu sanjari na waliotorosha mwili wa marehemu, polisi iliweka mtego na Novemba 3 mchana ndipo walikamatwa wanawake hao wawili.
Mwili huo ulivushwa na kuingizwa katika maeneo ya Nyamwaga mpakani kwenye Tarafa ya Ingwe. Wsafirishaji hao walikuwa katika gari aina ya Land Rover yenye Namba za Usajili T T 980 ACG mali ya mkazi wa mjini Tarime. Polisi imesema inaendelea kuwahoji wanawake hao.
Miongoni mwa matukio ya uhalifu ambayo Nyangarya (marehemu) anadaiwa kuhusika ni pamoja na mauaji ya mwenyekiti wa kijiji cha Nyarwana na diwani wa kata Kibasura wilayani. Anadaiwa pia kuhusika katika mauaji ya askari na kujeruhi mwingine katika uvamizi wa Benki ya Stanbick Nyamongo.
Maeneo mengine anayotuhumiwa kuhusika katika ujambazi ni kwenye miji ya Kahama (Shinyanga), Geita, Kisii (Kenya), Mwanza, Tarime, Isebania (Kenya), Kisumu (Kenya), Uganda na Dar es Salaam. Polisi imeomba ushirikiano wa wananchi kwa polisi wa Tanzania, Kenya na Uganda katika kufichua kikosi cha watu waliokuwa wakishirikiana na Nyarwana katika uhalifu ili wakamatwe.

No comments:
Post a Comment