![]() |
| Muonekano wa Jiji la Mwanza kutokea Ziwa Victoria. |
Msichana mwenye umri wa miaka 17 mkazi wa Nyegezi wilaya ya Nyamagana mkoani hapa, amekufa baada ya kubakwa na kisha kunyongwa na watu wanaosadikiwa alifahamiana nao.
Binti huyo ambaye mwaka huu alihitimu kidato cha Nne katika Shule ya Sekondari Nyakurunduma ya mkoani hapa, alikumbwa na mauti baada ya kupigiwa simu na mtu anayedhaniwa kumfahamu.
Baba wa mtoto huyo alisema kwamba akiwa nyumbani kwao usiku wa kuamkia juzi kati ya saa 4 na 5 usiku, aliondoka kwenda kwa mtu huyo na hakurudi nyumbani.
“Walimteka na kumfunga kamba shingoni, maana tumekuta shingo yake ikiwa na alama za kamba halafu walimbaka hadi kufa na mwili wake tumeuhifadhi katika hospitali ya rufaa ya Bugando kwa uchunguzi zaidi…nishukuru jeshi la polisi mkoani Mwanza kwa ushirikiano wanaoendelea kunipatia hadi sasa kuwasaka wauaji wa mwanangu.”
Alisema kulipokucha asubuhi walianza kumtafuta na walifanikiwa kuikuta maiti yake ikiwa karibu na kisima cha kutekea maji katika eneo la Nyegezi akiwa amekufa.
Alisema, “Tuliukuta mwili wake ukiwa karibu na eneo la kisima, akiwa amekufa inaonekana walipomkamata walimbaka kwanza na kisha wakaamua kumnyonga kwa kamba”.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, Liliani Matola alithibitisha kuwepo tukio hilo. Alisema polisi inaendelea kuchunguza kubaini chanzo cha mauaji hayo.

No comments:
Post a Comment