![]() |
| Marehemu Askofu Aloysius Balina. |
Askofu Aloysius Balina (67) wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, aliyefariki dunia jana kwa saratani ya ini, anatarajiwa kuzikwa Ngokolo, Shinyanga.
Kwa mujibu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, Mhashamu Tarsicius Ngalalekumtwa, Askofu Balina alifariki dunia jana mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza ambako alilazwa kwa takribani miezi miwili.
Mapema jana, Mkurugenzi wa Habari wa Jimbo Kuu la Mwanza, Padri Christopher Kubeja akiwa Mwanza alithibitisha kifo cha Askofu Balina na kueleza kuwa mwili wake umehifadhiwa Bugando.
“Ninaomba waumini wa Kanisa Katoliki jijini hapa na mikoa yote nchini waendelee kuwa watulivu wakati huu wa msiba wa kuondokewa na Baba yetu mpendwa Askofu Balina,” alisema Padri Kubeja.
Alisema taratibu za mazishi zinafanywa Ngokolo, ambako alisema pia utaratibu rasmi wa mazishi hayo utafanyika katika Jimbo hilo Jumamosi.
Makamu Msaidizi wa Askofu Jimbo Kuu la Shinyanga, Padri Sospeter Shole, alisema Jimbo limeupokea msiba huo kwa mshituko mkubwa na majonzi.
“Askofu Balina nimemfahamu kama mwalimu wangu nikiwa Katibu wake kwa muda mrefu, huu ni msiba mkubwa kwetu,” alisema.
Alisema kufariki dunia kwa Askofu Balina ni pigo kwa waumini wa Shinyanga na mikoa ya Kanda ya Ziwa kutokana na utume wake uliotukuka wa kuwapenda waumini na kuwaendeleza kielimu vijana wasiokuwa na uwezo kifedha.
“Alikuwa Askofu aliyependa watu na Jimbo lake kwa ajili ya kuliendeleza kielimu, ambapo alisomesha vijana na madaktari zaidi ya watano ambao hawakuwa na uwezo kifedha wamesoma kupitia mikononi mwake. Tutamkumbuka kwa upendo wake kwetu. Alikuwa Askofu aliyejitoa kuendeleza wakazi wake wa Shinyanga na nje ya mkoa kielimu,” alisema.
Padri Shole alisema mipango ya mazishi inaandaliwa jimboni Shinyanga na kutakuwapo na misa ya kumwombea marehemu leo kuanzia saa 10 jioni katika Kanisa Kuu, Ngokolo mkoani Shinyanga.
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Anthony Makunde alisema kifo cha Askofu Balina ni pigo kwa Baraza na hawana uwezo wa kuzuia mapenzi ya Mungu.
Kifo cha Askofu Balina kimekuja miezi michache tangu kifo cha Askofu Pascal Kikoti wa Jimbo la Mpanda mkoani Katavi. Askofu Kikoti alifariki dunia Agosti mwaka huu.
Askofu Balina alizaliwa Juni 21, 1945 katika kijiji cha Isoso Bariadi mkoani Shinyanga (sasa Simiyu) na alipata Daraja Takatifu la Upadri Juni 27, 1971 na kuteuliwa na Baba Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Kwanza wa Jimbo Katoliki la Geita, Novemba 8, 1984.
Aliwekwa wakfu kuwa Askofu wa Geita, Januari 6, 1985 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, Roma, Italia.
Agosti 8, 1997 aliteuliwa na Baba Mtakatifu John Paul II kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga na kusimikwa jimboni humo Novemba 17, 1997 kuwa Askofu wa tatu wa jimbo. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 41 ya upadri na 27 ya uaskofu.

No comments:
Post a Comment